Wafanyakazi wa kiwanda cha Nondo Sayona walipukiwa na uji wa moto

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Wafanyakazi wa kiwanda cha Nondo Sayona walipukiwa na uji wa moto

Wafanyakazi 18 wa kiwanda cha Nondo cha Sayona kilichopo Usagara wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, wamejeruhiwa na mlipuko wa moto uliotokea kiwandani hapo oktoba 9, 2023, baada ya kinu cha uji wa moto kulipuka ambapo waliokuwa karibu ndiyo walioathiriwa zaidi na joto la uji wa vyuma.

Wafanyakazi wawili wa kiwanda hicho, wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando BMC wakipatiwa matibabu huku 16 walitibiwa jana hospitali ya wilaya na kuruhusiwa.

Akizungumza leo Oktoba 10,2023, Meneja wa kiwanda cha Sayona Steel Sunny Naker amekiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa ilikuwa bahati mbaya na kwamba kuna jambo halikuwa sawa.

"Watu ambao waliumia sana walikuwa wawili, wengine wote (16) wapo sawa," amesema Sunny Naker.

Naker ameeleza kuwa taratibu zote za kiserikali zimekwisha chukuliwa na kubainisha hakuna jambo baya ambalo lilitokea katika kiwanda na sehemu iliyopata hitlafu tayari inaendelea kufanyiwa matengenezo.

"Baada ya tukio kutokea tulitoa taarifa OSHA ( Wakala wa usalama na afya mahala pa kazi ) na wao wanafahamu hilo jambo hivyo hakuna jambo ndugu yangu," ameeleza Naker.

Ndugu wa majeruhi, Simon Paulo, amesema mpaka sasa ndugu yake hajafungua macho yake kutokana na kuunguzwa na uji wa moto uliokuwa kwenye kinu cha kuyeyesha vyuma.

"Ndugu yetu bado hali yake sio nzuri ingawa anaendelea na matibabu ila kitendo cha kutofumbua macho yake kinatupa wasiwasi ngoja hali itakavyokuwa," amesema Simon.

Simon anasema licha ya hospitali ya Bugando ya jijini Mwanza aliyolazwa mgonjwa huyo kumpa huduma, lakini bado kuna tatizo la upatikanaji wa dawa kwenye duka lililopo nje ya hospitali hiyo.

Afisa Mahusiano wa hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando BMC, Everyne Mahalu amekiri hospitali hiyo kupokea wagonjwa hao ambao wanaendelea kupatiwa matibabu.

"Ni kweli tuliwapokea wagonjwa wawili kutoka Sayona na wawili wote wanaendelea na matibabu na taarifa zaidi nitakupigia baada ya muda mfupi.

Meneja wa Baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira (NEMC) mkoa wa Mwanza, Jarome Kayombo alipoulizwa kuhusu suala hilo alidai yupo nje ya ofisi yake na kuahidi kutuma maafisa wake kufika katika kiwanda cha Sayona kufuatilia taarifa hizo.

"Nipo mkoani Geita na hilo tukio sijapata taarifa zake ila nakushukru kwa kuniambia nakuahid nitalifuatilia na nitakupa majibu," amesema Kayombo.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa usalama na afya mahala pa kazi mkoa wa Mwanza, Mjawa Shenduli, amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanaendelea kuzifanyia kazi.

"Tangu juzi tulipokea taarifa za tukio hilo, idadi ya watu waliojeruhiwa anazifahamu mteja wetu (kiwanda cha Sayona) ukitaka kupata idadi sahihi ya watu walioumia nenda kiwandani," amesema Mjawa Shenduli.

Mkuu wa wilaya ya Misungwi Paulo Chacha, alipotafutwa kwa njia ya simu na kuulizwa kuhusu jambo hilo, alisema hajapokea taarifa za tukio hilo mpaka sasa.

"Naomba nitumie picha za hao watu wliojeruhiwa kiwandani nizione ili nianze kufuatilia hilo jambo, ndo nasikia hizo taarifa kwako,"amesema Chacha.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu tukio hilo alisema,"sijapata taarifa hizo, nitalifuatilia.
 

Attachments

  • IMG_20231012_113108.jpg
    IMG_20231012_113108.jpg
    59.2 KB · Views: 15
  • IMG_20231012_113205.jpg
    IMG_20231012_113205.jpg
    42.4 KB · Views: 13
  • IMG_20231012_113128.jpg
    IMG_20231012_113128.jpg
    42.1 KB · Views: 7
Aiseee Mungu mkubwa! Ilibaki kidogo tu ningekuwa miongoni mwao kuna mtu alikuja kuniunganishia mchongo wa hicho kiwanda kipindi hicho hicho ila nilishindwa kwenda kutokana na umbali na kukosa sehemu ya Karibu ya kukaa ili nipige kazi hapo pia walisema wanaanza na shift ya usiku na mimi kwa wakati huo sikuwa na nafasi kwa kazi za usiku.
 
Wangekuwa na fare juckets na helmets wasingepata madhara kama haya, sasa wabongo tulivyo ndezi nalo tutamwachia mungu
 
Aiseee Mungu mkubwa! Ilibaki kidogo tu ningekuwa miongoni mwao kuna mtu alikuja kuniunganishia mchongo wa hicho kiwanda kipindi hicho hicho ila nilishindwa kwenda kutokana na umbali na kukosa sehemu ya Karibu ya kukaa ili nipige kazi hapo pia walisema wanaanza na shift ya usiku na mimi kwa wakati huo sikuwa na nafasi kwa kazi za usiku.
Hatari sana mkuu,
Chuma inayeyuka katika zaidi ya 1500° C uji wake ukikugusa tu donda la kulitibu ni miezi mpaka mwaka.

Ukiungua Kwa mda huo huwezi kuhisi chochote Kwa sababu Neva za mwili zinakifa mda huohuo ila mtihani ni baada ya wiki kadhaa. Ajali yake unaweza ukafa bila maumivu
 
Hatari sana mkuu,
Chuma inayeyuka katika zaidi ya 1500° C uji wake ukikugusa tu donda la kulitibu ni miezi mpaka mwaka.

Ukiungua Kwa mda huo huwezi kuhisi chochote Kwa sababu Neva za mwili zinakifa mda huohuo ila mtihani ni baada ya wiki kadhaa. Ajali yake unaweza ukafa bila maumivu
Hatari sana
 
Serikali.mara ya mwisho ni lini kuingia viwandani na kukagua usalama kazini?
mnapajua SAMAKI PALE KEREGE?.
Siku nendeni alafu muwaambie tupelekeni SHIMONI KULE WANAPOOSHA MIFUKO NA KUIYEYUSHA.
NINA UHAKIKA MTALIA .
sisemi kuna nini ila nendeni mkajionee
 
Back
Top Bottom