DOKEZO MSD ilikabidhiwa kiwanda cha madawa Keko lakini kinaelekea kufa…

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ni ajabu ila ni kweli. Bohari ya Dawa (MSD) ambayo ipo chini ya Wizara ya Afya ambayo Waziri wake ni Ummy Mwalimu ilikabidhiwa uendeshaji wa Kiwanda cha Dawa cha Keko na Msajili wa Hazina mwaka 2020, ambacho kinamilikiwa kwa Asilimia 70 na Serikali huku mbia binafsi akimiliki Asilimia 30.

Kiwanda hiki kipindi cha Dorothy Gwajima akiwa Waziri wa Afya kilifanikiwa kupewa zabuni na malipo ya awali ya zaidi ya fedha za Kitanzania Bilioni 6 ili kizalishe dawa za binadamu kwa MSD na hatimaye zisambazwe kwenye hospitali za umma baada ya kubainika kuwa hakina mtaji wa kujiendesha huku kikiwa na uwezo wa uzalishaji.

Ni kweli kwamba zilikuwepo changamoto za uzalishaji wa mahitaji hayo ya dawa kutokana na uongozi uliokuwepo kiwandani hapo kukosa ubunifu kwa kiasi kikubwa hivyo kupelekea uzalishaji kusuasua hata hivyo walifanikiwa kumaliza uzalishaji huo.

Cha ajabu baada tu ya Waziri Ummy kushika hatamu za kuiongoza Wizara ya Afya ni kama kiwanda hiki kinajifia. Hakuna mtaji wa uendeshaji wala malipo ya awali. Izingatiwe kuwa kiwanda hiki hakijawahi kupewa mtaji wa kujiendesha miaka 3 sasa baada ya kumilikiwa rasmi na Serikali kama mbia mkuu ikisaidiana na mbia mdogo binafsi.

Inashangaza kiwanda ambacho kilipiganiwa na hayati John Magufuli Rais wa Awamu ya Tano, kikarejea Serikalini na baadaye kikatembelewa na uongozi wa juu wa nchi huku kikiwa kwenye uzalishaji mzuri leo kinatelekezwa.

Nani anafaidika? Ni baadhi ya Watendaji Serikalini wakisaidiana na mbia binafsi ambaye alishindwa dhahiri kukiendesha na sasa anaona upo upenyo wa kuvuruga mambo baada ya Serikali kukikalia kimya?

Wafanyakazi wa kiwanda hiki nao wamegubikwa na sintofahamu kubwa baada ya mambo kuwa hayaeleweki. Ni sekta ipi hasa inawajibika kuondoa sintofahamu hii?

Ni jambo la ajabu kuona kiwanda kimechukuliwa na Serikali mwaka wa nne huku kikiwa hakisimamiwi kiutendaji na mamlaka za juu za nchi, mbaya zaidi kinajiendesha tu huku "chain of command" ikiishia kwa Wanao kiendesha ambao ni wawakilishi kutoka Serikalini wakiwa wanajiamulia tu waendeje na mambo.

Kama kiwanda hiki kilianza vizuri enzi ya Waziri Gwajima, inakuwaje baadaye kiwanda hiki kinageuzwa kuwa shamba la bibi kwa wanaokisimamia? Serikali inapaswa kuchukua hatua ili kuondoa sintofahamu hii ambayo inaathiri jamii ya wafanyakazi wa kiwanda hicho.
 
Kupotea kwa jiwe kumewarudisha kwenye reli mapanya wote waliozoea kuihujumu nchi. Hata huyo mmriki mbia lazima atambe make alizoea kula nao.

Wateule wa magu waliosimikwa hapo kuiwakilisha serikali hawana guts ya kuripoti madudu make mamlaka za juu ndo wapigaji wenyewe. Kwahiyo kilichobaki hapo ni kufunika kombe mwanaharamu apite kama wasemavyo wazungu "if you can't fight them, join them."
 
Ni ajabu ila ni kweli. Taasisi ya usambazaji dawa na vifaa tiba ya msd ambayo ipo chini ya wizara ya afya ambayo waziri wake ni mheshimiwa Ummy Mwalimu ilikabidhiwa uendeshaji wa kiwanda cha madawa cha Keko na msajili wa hazina mwaka 2020, ambacho kinamilikiwa kwa asilimia 70 na serikali huku mbia binafsi akimiliki asilimia 30.

Kiwanda hiki kipindi cha mheshimiwa Dorothy Gwajima akiwa waziri wa afya kilifanikiwa kupewa zabuni na malipo ya awali ya zaidi ya fedha za kitanzania bilioni 6 ili kizalishe dawa za binadamu kwa msd na hatimaye zisambazwe kwenye hospitali za umma baada ya kubainika kuwa hakina mtaji wa kujiendesha huku kikiwa na uwezo wa uzalishaji.

Ni kweli kwamba zilikuwepo changamoto za uzalishaji wa mahitaji hayo ya dawa kutokana na uongozi uliokuwepo kiwandani hapo kukosa ubunifu kwa kiasi kikubwa hivyo kupelekea uzalishaji kusuasua hata hivyo walifanikiwa kumaliza uzalishaji huo.

Cha ajabu baada tu ya waziri Ummy kushika hatamu za kuiongoza wizara ya afya ni kama kiwanda hiki kinajifia. Hakuna mtaji wa uendeshaji wala malipo ya awali. Izingatiwe kuwa kiwanda hiki hakijawahi kupewa mtaji wa kujiendesha miaka 3 sasa baada ya kumilikiwa rasmi na serikali kama mbia mkuu ikisaidiana na mbia mdogo binafsi.

Inashangaza kiwanda ambacho kilipiganiwa na hayati John Magufuli Rais wa awamu ya tano, kikarejea serikalini na baadaye kikatembelewa na uongozi wa juu wa nchi huku kikiwa kwenye uzalishaji mzuri leo kinatelekezwa.

Nani anafaidika? Ni baadhi ya watendaji serikalini wakisaidiana na mbia binafsi ambaye alishindwa dhahiri kukiendesha na sasa anaona upo upenyo wa kuvuruga mambo baada ya serikali kukikalia kimya?

Wafanyakazi wa kiwanda hiki nao wamegubikwa na sintofahamu kubwa baada ya mambo kuwa hayaeleweki. Ni sekta ipi hasa inawajibika kuondoa sintofahamu hii?

Ni jambo la ajabu kuona kiwanda kimechukuliwa na serikali mwaka wa nne huku kikiwa hakisimamiwi kiutendaji na mamlaka za juu za nchi, mbaya zaidi kinajiendesha tu huku "chain of command" ikiishia kwa Wanao kiendesha ambao ni wawakilishi kutoka serikalini wakiwa wanajiamulia tu waendeje na mambo.

Kama kiwanda hiki kilianza vizuri enzi ya waziri Gwajima, inakuwaje baadaye kiwanda hiki kinageuzwa kuwa shamba la bibi kwa wanaokisimamia? Serikali inapaswa kuchukua hatua ili kuondoa sintofahamu hii ambayo inaathiri jamii ya wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Tatizo wateja kwani kimejificha na uhaba wa umeme na maji.
Kikifa tutampa nabii Suguye awe anawaponya watu hapohapo bila kutegemea umeme.
 
R.I.P Magufuli
 
Tatizo wateja kwani kimejificha na uhaba wa umeme na maji.
Kikifa tutampa nabii Suguye awe anawaponya watu hapohapo bila kutegemea umeme.
Serikali itangaze mnada iuze kiwanda hicho, iache kujifanya inaweza sana biashara,
Mbna kuna Prince, Zenufa, na Shellys wanafanya vema tu, kwanini keko kife ? Serikali itangaze mnada wa hisa zake at least 50% ibaki na 20% tu
 
Watakao uziwa ni hao wanaoiua, bora tumpe nabii Suguye iwe kama Kawe TP uponyaji instant hakuna cha NHIF.
 
Wageni bana. We mtoa taarifa ni wa hukohuko nini? Maana unamwaga data kama upo jikoni kabisa. Au una machungu kuna mahali walikukatili ?
 
Back
Top Bottom