Wafanyakazi tunataka Mkurugenzi SSRA ajiuzuru, TUCTA iongoze mgomo huo

Sisi wafanyakazi kwa umoja wetu kama ambavyo mmetusikia kwenye vyombo vya habari tunataka Irene ajihudhuru mara moja. Kutokana na kushindwa na kuonesha hana uwezo wa kufikiria kwa ajili ya jamii ya wafanyakazi.

Ni wazi ameshindwa kuijua jamii ambayo anapaswa kuijua vizuri na kuiongoza ktk kuhimili maisha na changamoto zake.





Tunamuomba Irene heri apishe ili wafanyakazi tuwe na imani na SSRA, suala la kutoa mafao ya kujitoa ni jaribio la mauaji ya halaiki, mtanzania huyu asiye na mtaji atasubiri vipi umri wake ufike 55 ili achukue mafao yake ile hali life spana yake ni miaka 47??? Irene unakopi visivyokopika, umeshindwa kuonesha una uwezo kiakili wa kufikiri na kupanga kwa ajili ya watanzania, achia ngazi.

Tunaomba TUCTA isimame kitede kutuwakilisha wafanyakazi ktk sekta zote kuwa hatumtaki DG wa aina hii, pia hatuna muda wa kumwacha ajifunzie kazi maisha yetu. Aondoke mara moja, kama ni njaa anaganga ni heri akasubiri mme wake alete msosi au kama hana ni vema akaolewa mapema, lakini hili la kutunyima haki watanzania halikuballiki.

Mtanzania mwenye akili timamu, aliyesoma, wazazi wake ni watanzania hawezi kukaa na kufikiri kuwa mafao ya kujitoa yasiwepo, hawezi hata kidogo, je Irene hili kalitoa wapi???? Tunataka kuanzia sasa turuhusiwe kuchukua mafao yetu tena kama kawaida sio ndani ya miezi sita bali mitatu tu.

Nawasilisha.

Anganlia umejikwa wapi siyo ulipo angukia Mkuu! Dada Iren anatekeleza sheria ilipitishwa na Bunge Mwezi March 2012. Nakuomba mwajibishe Mbunge wako aliyesiinzia sheria hii ikapita!
 
Anganlia umejikwa wapi siyo ulipo angukia Mkuu! Dada Iren anatekeleza sheria ilipitishwa na Bunge Mwezi March 2012. Nakuomba mwajibishe Mbunge wako aliyesiinzia sheria hii ikapita!

Utaratibu wa kutunga sheria ni kuwa mswada hutayarishwa na timu ya wataalam (hapa manaa yake SSRA, Wizara ya Kazi, Wizara ya Fedha, Wizara ya Sheria), na baadaye za la Mawaziri, Kamati husika ya Bunge, na baadaye hujadiliwa Bungeni. Mwishoni huwekwa saini na Rais ili kuwa sheria. Katika mlolongo huu, tujiulize ni Taasisi gani imeonyesha udhaifu na kuleta kisicho na maslahi kwa watu / walengwa???
 
Naunga mkono hoja...hatufai huyu binti kwani alitakiwa awe pro active na ajue hii sheria ni ya uonevu kwa wafanyakazi, wabunge nao yabidi tuwalaumu maana kama ingekua inawagusa hii sheria am double sure lazima wangeikataa...
 
Hapa naona mnataka kwenda mbali zaidi, ile nafasi aliyo nayo yaweza kuwa ndiyo mahari na posa iliyotolewa na Kiongozi anayesemekana amemfanya nyumba yake ndogo. Mimi simo
 
ikiwa serikali ndio yenye njaa na kutaka kutumia pesa zetu basi yeye ni mtu mdogo sana kupinga hillo hata angekuwa na akili kama nini.
ila ikiwa yeye ndio aliyoanzisha kitu hii kwa kweli hatufai tena atoke tu katika hiyo nafasi
 
Umeshasema Private Sector,kule wanapatikana kwa kushindanishwa na hakuna uchakachuaji.Sasa huyu mwenzetu kashindanishwa na nani yeye si kateuliwa tu kuongoza hiyo SSRA

ndo unavyodanganyika ivyo! kuwa kule wanashindanishwa sio, hahaha!
 
Don't drag unfounded allegations(sp) to this issue, yaani kila mtu kapata cheo alichonacho kwa kutoa chochote?!

That's full of lies and u know it!

She is capable of handling SSRA you should task paliamentarians for passing it

SIUNGI MKONO HOJA !

Irene Songa !

Nsiande, engineer mwenzangu, habari ya Tanesco?
 
Nsiande, engineer mwenzangu, habari ya Tanesco?

Kama kweli huyo ni engineer basi hana tofauti na akina Fundi Mchundo Stella Manyanya!

Masikini hajui hata miswaada huandaliwa vipi hadi kufikishwa bungeni.

BTW, Wabunge kama walisinzia wakapitisha huo mswaada (Ingawa tunafahamu ulikuwepo mchezo mchafu wa HIDE AND SEEK). Kulingana na katiba yetu tunajua jinsi ya kuwaa adabisha i.e in the ballot box.

Sasa huyu Mama aliyekuwa picked with a single handed of one person, tutamuadabisha vipi, kama sio hii pressure kwamba sisi anatuongoza hatumtaki because ameshindwa kusimamia masilahi yetu, ili yule aliyemchangua amutoe hapo na kama anampenda zaidi amepeleke IKULU akampikie CHAI, lakini sisi wafanyakazi HATUMTAKI.

Kama atagoma kumtoa tutamu adabisha yeye (read Chama chake) kwenye ballot box!
 
• Wote mliopinga hoja ya mtoa mada ni wachumia tumbo! Hamjui maisha,ni kula kulala kwa baba zenu,mnategemea wazazi wenu wafe mrithi mali,kwa kijana mchakarikaji hawezi kuhafiki wazo la ssra la kuzia fao la kujitoa!
•Irene anatumika vibaya,hata kama mama una njaa,ulivyofanya sio kabisa,kama unazuia fao la kujitoa basi weka unemployment benefit basi tuone wewe ni mtaalamu wa mambo ya hifadhi ya jamii,inaonyesha umeperuzi madesa tu lkn upeo ni zero kabisa
•Wabunge tunawaomba huo mswada ukiletwa tena october ondoeni kile kipengele kandamizi(kuzuia fao la kujitoa),hatukitaki paseee! Wale wabunge waliosema Siooo kwenye hoja ya seleman jafo tunawajua wote,dawa yao ipo 2015 kwa sasa tunaichemsha jikoni,wabunge ambao walio support na wanaosuport neema izi kutiririka 2015 tutawapa mashavu inshallah.
•Mgaya wa TUCTA unakula fedha bure za wafanyakazi,kazi tuliyokutuma hauiwezi,kama mlishirikishwa na ssra mbona haujaja kutupa feedback? Tucta alikuwepo rwegasila tu ndio maana mmemuua!! Jana ITV uliulizwa kama mlipinga kipengele kwanin msingetoka na kuja kuwaeleza wananchi? Ukajibu blabla tu!! Acha kutumika utamuumiza hadi mwanao fikiria mbele!
•Mwisho naungana na mtoa mada,dada irene hatufai kabisa,ameonyesha failure ktk uongozi,hana busara wala hawezi ku-fore-see jambo,tunakuomba u-resign vyeo kama hivyo vinahitaji busara na taaluma sio vyeo vya fadhira wala vya kukuta ma-hotelini kugawana umaskini.
 
Hii nchi imeshapoteza muelekeo,na hawa viongozi wa hii serikali wasubiri 2015 ndio watajua hasira ya wanachi wa nchi hii,hawataki kuamini kitakachotokea lakini muda utafika they will believe it.Wananchi wameshachoshwa na haya manyanyaso yanayo fanywa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi.Hawana huruma hata kidogo wanajiona kama wako kwenye pepo ambayo no body can touch it,Mungu yupo and their judgement is just around the corner.
 
Mi nafikiri wa kujiuzuru ni Mgaya kwani anakiri walishirikishwa katika hatua za mwanzo ingawa kuna mambo wamepitisha kinyume.Hii sheria ilipitishwa mwezi wa nne na wabunge ambao hawana uchungu wowote lakini yeye kama mtendaji wa chombo kinachowakilisha wafanyakazi alikuwa wapi muda wote amekuja kuongea baada ya watu kuanza kupinga hii sheria kwa hiyo ameshindwa kulinda na kusimamia maslahi ya wafanyakazi.
Katika mifuko yote hadi SSRA vyama vya wafanyakazi vinakuwa na wawakilishi labda tumuulize alishawahi kulalamika jinsi pesa za wafanyakazi zinavyowanufaisha wasio wafanyakazi angalia mkopo aliopewa Sumaye,Manji kuwataja kwa uchache
Uwekezaji usio na manufaa kama machinga complex,kiwira mine,general tyre,ujenzi wa nyumba za polisi kutaja kwa uchache.
Pamoja na mfumuko wa bei kufikia nukta mbili bado riba kwa mwaka NSSF ni 1.8% ambayo hata benki huwezi kupata riba hiyo.
Inabidi tujiulize kwanini vyama vya wafanyakazi kama Afrika kusini vinakuwa na nguvu lakini vyakwetu ni dhaifu wamekuwa wanawatoza wafanyakazi pesa bila wafaanyakazi kufaidika na vyama hivyo
 
Mm naona huyu ndio yule sober aliyemwambia Mnyika kapotoka kwa kutetea Wanaochangia mifuko ya mafao wapewe mapema Mafao yao sio wasubiri mpaka miaka 55
namshukuru sana Mh. Jafu Mbunge wa Kisarawe kwa kuliona hili hasa kwa wachimbaji wa Migodini ambao hupewa mikataba ya miaka 2 tu na kuachishwa kazi, na ukikataliwa kupewa Mkataba mwingine ujue hukuna mafao eti mpaka miaka 55
Huu ulikuwa ni Wizi Mkubwa sana fuatila hata mada hizo za sober https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/302777-mh-mnyika-kwa-hili-umepotoka-10.html
 
Naunga mkono hoja.
actually it was supposed to be yesterday, even today is late. she must resign nw.
 
Huyu dada anaongeaongea tu bila kufikiri kwanza amewahi kuona au kusikia wapi CEO,gavana wanaongea na kukanusha Kauli zake hvyhvyo tena kwenye radio mbao(clouds).hana uwezo wakufanya kazi na jamhuri hii anadhahi serikalini ni Kama pale stanbic alipokuwepo,sasa limemganda hili tena amekera sana na Kauli.zake za dharau na kebehi alizotoa alipofanya mahojiano na kibonde..naunga Mkono hoja
 
Irene is just fine. Hastahili kujiuzulu kwa hili.

Siyo mara ya kwanza kwa Tanzania kujaribu kutekeleza hii dhana ya mifuko ya jamii kuwa ni fao la uzeeni kama inavyofanyika ulimwengu wote. Walishajaribu tena miaka ya 2003 - 2005 ikaondolewa kutokana na public outcry ya wafanyakazi wa migodini.

Cha kumpa sifa Irene, ni kwamba yeye ameelewa kosa haraka sana na ameacha kujaribu kutetea hii sera. Ingekuwa vigogo tuliowazoea ungesikia jinsi wanavyojitutumua na kuvimba kuwa sheria lazima itekelezwe.

Kwa maono yangu, Irene anaweza kuja kuwa kiongozi bora kwani amebatizwa na moto
 
Irene-Isaka1.jpg
 
Back
Top Bottom