Wafanyakazi tunataka Mkurugenzi SSRA ajiuzuru, TUCTA iongoze mgomo huo

Sasa Irene akijiuzulu ndio nini? Je unajua yeye katika ngazi za mamlaka ni mtu mdogo sana?
Mbali na Rais, kuna waziri, naibu waziri, katibu mkuu, bodi nk......je hao kwa nini huoni wanapaswa kubebeshwa zigo.

Je unajua huyu Irene ni bangu silo?

Lazima mtoke hapo mlipo kama mnataka maisha bora. Ukombozi wa fikra ni lazima uende sambamba na mabadiliko ya nje i.e. kisiasa na kiuchumi
 
hapana kama amejirudi it is okay

Alisemaje Makamba Senior kuhusu mtu mzima na msuli unaomvuka? Kuwa huwa anachuchumaa siyo.

Na akichuchumaa watu wazima wengine humpa staa siyo? Ni watoto tu wataanza kumzomea na kupiga miluzi.
 
Sisi wafanyakazi kwa umoja wetu kama ambavyo mmetusikia kwenye vyombo vya habari tunataka Irene ajiuzuru mara moja. Kutokana na kushindwa na kuonesha hana uwezo wa kufikiria kwa ajili ya jamii ya wafanyakazi.

Ni wazi ameshindwa kuijua jamii ambayo anapaswa kuijua vizuri na kuiongoza ktk kuhimili maisha na changamoto zake.

Tunamuomba Irene heri apishe ili wafanyakazi tuwe na imani na SSRA, suala la kutoa mafao ya kujitoa ni jaribio la mauaji ya halaiki, mtanzania huyu asiye na mtaji atasubiri vipi umri wake ufike 55 ili achukue mafao yake ile hali life spana yake ni miaka 47??? Irene unakopi visivyokopika, umeshindwa kuonesha una uwezo kiakili wa kufikiri na kupanga kwa ajili ya watanzania, achia ngazi.

Tunaomba TUCTA isimame kitede kutuwakilisha wafanyakazi ktk sekta zote kuwa hatumtaki DG wa aina hii, pia hatuna muda wa kumwacha ajifunzie kazi maisha yetu. Aondoke mara moja, kama ni njaa anaganga ni heri akasubiri mme wake alete msosi au kama hana ni vema akaolewa mapema, lakini hili la kutunyima haki watanzania halikuballiki.

Mtanzania mwenye akili timamu, aliyesoma, wazazi wake ni watanzania hawezi kukaa na kufikiri kuwa mafao ya kujitoa yasiwepo, hawezi hata kidogo, je Irene hili kalitoa wapi???? Tunataka kuanzia sasa turuhusiwe kuchukua mafao yetu tena kama kawaida sio ndani ya miezi sita bali mitatu tu.

Nawasilisha.

Mkuu sio rahisi hivyo. Anza na mbunge wako aliyekubali kupitisha sheria hiyo. Kama mmechagua wawakilishi pumbafu ina maana na nyie ni pumbafu. Ngoja mburuzwe mpaka mjifunze. Wanafiki waseme ndiyoooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Mswada ulipelekwa bungune kwa kificho, nilipitia na kuwauliza wadau kusoma harnsad hapakuwepo na uwazi kabisaa. nawaunga mkono wabunge kwa kiganja!
SSRA na serikali hawawezi kukwepa hili, wao ndio wadau wakubwa wa mswada huo na walifanya kwa lugha isiyo ya moja kwa moja.
Irene aondoke sina imani naye kwa vyovyote vile. imagine mie huyu hata baada ya mkopo bank sijawahi kushika hata 20M, ila hifadhi nina zaidi ya 80M, huyu mama ananiambia - clouds FM eti wafanyakazi msilalame kwani 90% mnalipwa mshahara, mnayokatwa ni only 10%, hivyo kama hujaendelea na 90%, hio 10% itakusaidia nini?!
Irene Ni dhaifu tena mbumbumbu, 90% hio hakumbuku kwamba nailipia 30-40 PAYE, nalipia nyumba, nalipa tena kodi kwa 18% kwa kila nitachonunua.
aondoke, labda ajaribu ajira nyumbani kwangu kuna nafasi yake. Yes, naamini japo kazi moja ataweza
 
Kuna umuhimu wa wananchi kuchukua hatua dhidi ya maamuzi au vitendo vyovyote vile vinavyowakandamiza iwe vimepitishwa kisheria ama la. Wafanyakazi wenye akili inayofanya kazi vizuri ambao sheria hii imewaathiri siyo tu watataka ajiuzulu, bali watataka apate pia adhabu itakayomuumiza yeye pamoja na wengine wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine kupitisha hiyo sheria ili iwe fundisho kwao na pia kwa wengine watakaofanya maamuzi baadaye.
Ni majuha tu watakaomtetea mtu yeyote yule aliyehusika na kadhia hii kama imewaathiri.
Tatizo hapa siyo umri, jinsia wala vinavyofanana na hivyo bali ni maamuzi yanayotesa wengi.
Watu wa tabaka la chini wanatakiwa kujua kwamba hakuna mtu anayewajali kwa uhalisia na hivyo jukumu la kujitetea ni lao wenyewe na wakati mwingine inahitajika kutumia vitendo kuwaadabisha watu walio kwenye nafasi za juu badala ya kulalamika tu. Woga ni umasikini!
 
Atoke tu, asisingizie bunge, mara alipoona hiyo sheria kandamizi kwanini asingejiuzulu kwani kama kweli yeye ni compitent na amewekwa pale ni dhahiri anaufahamu ubaya wa hiyo sheria kuliko hata sisi. kwakweli atoke tena haraka
 
Na hii ndiyo Tz bana mtalia mpaka machozi ya damu na hakuna anayesikia watu wengi wamepewa nyadhifa kwa kiapo cha kuitetea serikali iliyopo madarakani,Iwe kwa mabaya ama mazuri.
So nadhani inahitajika wananchi wachini tunaoumia na mfumo huu tuache kumalizia hasira zetu kwenye keyboard tu bali tujaribu kuchek na plan B.

Tehe Tehe Tehe plan (B)???? Mtanzania yupi? Ulimboka kachungulia kaburi na sasa kabaki na maumivu+scar face na mark za kutosha mwilini nani anamjali Leo Hii? Walimu walipinga mgomo hatimaye ni asilimia 30% tuu Ndio waliogoma wengine wakaendelea kupiga mzigo. Watz hasira na Maandamano Yao ni kwenye keyboard tuu eti wanadai chezea kazi uone ni jinsi gani kupata kazi. bado sana kwa Wabongo tena wanavoogopa kengeza za kova
 
Mimi nashangaa sana, hivi huyu dada kwanza nani alimpatia cheo kikubwa sana kama chake? Du mimi kila nikimwangalia simumalizi hata kidogo. Sasa kwa mara ya kwanza kabisa naomba mwenye CV yake aimwage maana kati ya watu walionichefua mwaka huu mpaka nikatamani kwenda kutubu kanisani ni huyu dada.Nimeshamtukana matusi yote ya duniani na sitatubu mpaka hapo atakaporejesha fao la kujitoa. Kama vipi mimi mniambie kama kaolewa nataka nimuweke nyumba ndogo ili aone jinsi maisha ya bila mtaji yanavoumiza



Wabongo bwana wacheni uvivu wa kufikiri unadhani CV au degree Ndio akili? Mbona Jk ni Dr JIULIZE kasomea wapi? Pr. Maji marefu Hana ata cv na ni mbunge cv sio weledi wala akili degree au PHD sio akili kuna za kununua kwa cash na ngono na kuna za kupewa pia sio Kila ktu eti mwaga cv Yake hapa uo ni uvivu wa kufikiri hao wabunge wenu wasomi Ndio waliopitisha Leo mnamtoa kafara Irene kwani yeye Ana mamlaka zaidi ya Bunge????? Huitaji PHD kufikiri kosa la Irene ni kuwa kiongozi na sio vinginevo iyo tucta yeyewe ni air polusion tuu ata ukibasili Kuni moto ni ule ule waadabisheni wabunge wenu pamoja na ccm kwenye uchaguzi Ndio mtafanikiwa japo kwa asilimia chache Roger
 
.......Sipendi kumtetea dada Irene lakini pia tusimfanye "bangusilo" au mbuzi wa kafara peke yake kama tunataka kuelekea kwenye nchi ya ahadi.

kwenye bold...umenikumbusha mbali sana back in 2008 pale Rich Monduli ilipolipuka kwenye bunge la tisa.

hivi yuko wapi ex-mheshimiwa Msabaha siku hizi???
 
Ana uwezo labda katikati ya wajinga...
Fikra ndogo tu, ni upuuzi kufikiria dundulizo za 10% kuwaclaimed at 50's, moja pesa za mifuko ya jamii hazina riba

mbili hizo investment zinazofanyika bila kushirikisha washikadau ni ukiukwaji mkubwa sana, failure ikitokea Serikali itaanza kulia njaa si unajua Serikali yako?

Tatu kuchukua hiyo pesa mapema kunaongeza nguvu ya soko, mwingine ataanzisha biashara, atajenga nyumba na mengineyo

Naomba kuwasilisha
 
hii nchi sijui kuna shida gani,hata ubadilishe viongozi mambo yanabaki vile vile au yanazidi kuwa mabaya zaidi kama wizara ya nishati na madini,Msabaha,Karamagi,Ngeleja na sasa Muhongo still no tremendous difference.Why?
 
Don't drag unfounded allegations(sp) to this issue, yaani kila mtu kapata cheo alichonacho kwa kutoa chochote?!

That's full of lies and u know it!

She is capable of handling SSRA you should task paliamentarians for passing it

SIUNGI MKONO HOJA !

Irene Songa !

I don't know cz ur Irene too or what? its better aachie ngazi kwa kuwajibika!
 
Mkuu Fikirikwanza,
1. Hivi unajua maana ya SSRA na misingi ya kuanzishwa kwake?
2. Aliyeipitisha Sheria hiyo mpya ambayo haswa issue ya fao la kujitoa ndiyo imekuwa gumzo ni Irene au ni Bunge?
3. Yeye anatekeleza sheria inavyomtaka, yaani sheria ya kuanzishwa kwa SSRA, sheria ya bunge ya mambo ya mafao, lakini niseme tu kuwa anatekeleza Job Description yake.
4. Kwamba yeye kupewa u- DG wa SSRA, jamani huo ni wadhifa aliyoteuliwa nao na Mh. Rais.
5. Kwamba SSRA wanalipata mshahara mkubwa, si kosa la Irene, yeye alitengeneza Scheme of Service na madokumenti kibao na yakapitishwa na Msajili wa Hazina na Utumishi na wafanyakazi wa SSRA wanalipwa, kosa lake ni lipi hapo?
6. Mwisho wa siku, Irene ni mwajiriwa wa SSRA akama alivyo mhudumu, mlinzi, Karani nk.

"Dont Hate The Player; Hate The Game"

Kwa hili, tusimuonee bure.

if that's the case no one will be held responsible for his / her actions cz the system is always the big excuse! bt all in all sh was wrong n for that she'll be answerable for ha actions!
 
Irene tokaaaaa tena ushindwe kwa jina la Yesu! Mimi napata kichefu chefu kusikia hata jina lake! hatumtaki jamani sisi!!!
 
Watapana sana lakini tucta ikisimama vema, ataondoka. Wafanyakazi ndo tunakazi ya kufanya.
 
Sisi wafanyakazi kwa umoja wetu kama ambavyo mmetusikia kwenye vyombo vya habari tunataka Irene ajiuzuru mara moja. Kutokana na kushindwa na kuonesha hana uwezo wa kufikiria kwa ajili ya jamii ya wafanyakazi.

Ni wazi ameshindwa kuijua jamii ambayo anapaswa kuijua vizuri na kuiongoza ktk kuhimili maisha na changamoto zake.

Tunamuomba Irene heri apishe ili wafanyakazi tuwe na imani na SSRA, suala la kutoa mafao ya kujitoa ni jaribio la mauaji ya halaiki, mtanzania huyu asiye na mtaji atasubiri vipi umri wake ufike 55 ili achukue mafao yake ile hali life spana yake ni miaka 47??? Irene unakopi visivyokopika, umeshindwa kuonesha una uwezo kiakili wa kufikiri na kupanga kwa ajili ya watanzania, achia ngazi.

Tunaomba TUCTA isimame kitede kutuwakilisha wafanyakazi ktk sekta zote kuwa hatumtaki DG wa aina hii, pia hatuna muda wa kumwacha ajifunzie kazi maisha yetu. Aondoke mara moja, kama ni njaa anaganga ni heri akasubiri mme wake alete msosi au kama hana ni vema akaolewa mapema, lakini hili la kutunyima haki watanzania halikuballiki.

Mtanzania mwenye akili timamu, aliyesoma, wazazi wake ni watanzania hawezi kukaa na kufikiri kuwa mafao ya kujitoa yasiwepo, hawezi hata kidogo, je Irene hili kalitoa wapi???? Tunataka kuanzia sasa turuhusiwe kuchukua mafao yetu tena kama kawaida sio ndani ya miezi sita bali mitatu tu.

Nawasilisha.
Nnaamini mumewake huko aliko anafuraha ya hali ya juu
 
Back
Top Bottom