Wafanyakazi tunataka Mkurugenzi SSRA ajiuzuru, TUCTA iongoze mgomo huo

Ama hujielewi au huishi Tz, Irene Kissaka chali, mbangusillo ama laa lakini chali! hujamsoma vizuri JPM wewe?!

Sasa Irene akijiuzulu ndio ni
ni? Je unajua yeye katika ngazi za
mamlaka ni mtu mdogo sana?

Mbali na Rais, kuna waziri, naibu waziri, katibu mkuu, bodi nk......je hao kwa nini huoni wanapaswa kubebeshwa zigo.

Je unajua huyu Irene ni bangu silo?

Lazima mtoke hapo mlipo kama mnataka maisha bora. Ukombozi wa fikra ni lazima uende sambamba na mabadiliko ya nje i.e. kisiasa na kiuchumi
 
Ama hujielewi au huishi Tz, Irene Kissaka chali, mbangusillo ama laa lakini chali! hujamsoma vizuri JPM wewe?!
1546058279712.png

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka - JamiiForums
 
Maono huchelewa tu lakiniu lazima yatimie; TANGU SIKU HIZO TULIONA ANAKOPI MAMBO AMBAPO HANA PA KUPASTE ANATUMIA WAFANYAKAZI TZ KAMA SEHEMU YA KUJIFUNZIA KAZI.

Sisi wafanyakazi kwa umoja wetu kama ambavyo mmetusikia kwenye vyombo vya habari tunataka Irene ajiuzuru mara moja. Kutokana na kushindwa na kuonesha hana uwezo wa kufikiria kwa ajili ya jamii ya wafanyakazi.

Ni wazi ameshindwa kuijua jamii ambayo anapaswa kuijua vizuri na kuiongoza ktk kuhimili maisha na changamoto zake.

Tunamuomba Irene heri apishe ili wafanyakazi tuwe na imani na SSRA, suala la kutoa mafao ya kujitoa ni jaribio la mauaji ya halaiki, mtanzania huyu asiye na mtaji atasubiri vipi umri wake ufike 55 ili achukue mafao yake ile hali life spana yake ni miaka 47??? Irene unakopi visivyokopika, umeshindwa kuonesha una uwezo kiakili wa kufikiri na kupanga kwa ajili ya watanzania, achia ngazi.

Tunaomba TUCTA isimame kitede kutuwakilisha wafanyakazi ktk sekta zote kuwa hatumtaki DG wa aina hii, pia hatuna muda wa kumwacha ajifunzie kazi maisha yetu. Aondoke mara moja, kama ni njaa anaganga ni heri akasubiri mme wake alete msosi au kama hana ni vema akaolewa mapema, lakini hili la kutunyima haki watanzania halikuballiki.

Mtanzania mwenye akili timamu, aliyesoma, wazazi wake ni watanzania hawezi kukaa na kufikiri kuwa mafao ya kujitoa yasiwepo, hawezi hata kidogo, je Irene hili kalitoa wapi???? Tunataka kuanzia sasa turuhusiwe kuchukua mafao yetu tena kama kawaida sio ndani ya miezi sita bali mitatu tu.

Nawasilisha.
 
Hayakwenda bure

Wabunge wanapelekewa tena nikisema ukweli wote sometimes wanapelekewa kijanjajanja, ndo maana wamesituka na kupitisha irejeshwe bungeni ili watengue kifungu hicho chenye wizi kwa mali halali ya mtanzania kwa njia ya kisasa zaidi.

Tunawashukuru wabunge kwa kupitisha hilo, Je aliyesimamia na mwenye dhamana ya hifadhi ya jamii SSRA achukuliwe hatua gani baada ya bunge kuona udhaifu huo??? Irene Isaka ajihudhuru hatuna imani naye, sasa atafanyaje kazi na sisi wenye mali/michango ambao hatumtaki na imani hatuna??? kama sio shida za dunia hii, njaa na kama sio ulafi wa madaraka angeomba kuachia ngazi mwenyewe kimya kimya kwa kosa ambalo yeye na ssra wamelifanya kwa watanzania.

Leo hii wafanyakazi wanalia kwenye TV is it normal in Tz?? machozi hayo hayaendi bure.
 
Mengine umeandika walao vizuri lakini uliposema kuchukua pesa mapema kutaongeza nguvu ya soko,sasa soko gani ? Na kwa bidhaa ipi m? akili nyongine bhana hahahahahaha
Ana uwezo labda katikati ya wajinga...
Fikra ndogo tu, ni upuuzi kufikiria dundulizo za 10% kuwaclaimed at 50's, moja pesa za mifuko ya jamii hazina riba

mbili hizo investment zinazofanyika bila kushirikisha washikadau ni ukiukwaji mkubwa sana, failure ikitokea Serikali itaanza kulia njaa si unajua Serikali yako?

Tatu kuchukua hiyo pesa mapema kunaongeza nguvu ya soko, mwingine ataanzisha biashara, atajenga nyumba na mengineyo

Naomba kuwasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! Miaka sita Baadaye.. hii nnji hii!
Halafu fhala fhulani anasema kuna uhuru hadi vyama vya wafanyakazi vimesikilizwa!
 
Mengine umeandika walao vizuri lakini uliposema kuchukua pesa mapema kutaongeza nguvu ya soko,sasa soko gani ? Na kwa bidhaa ipi m? akili nyongine bhana hahahahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app

Assume kuna "wastaafu" 50 kila mwaka "wanaostaafu" Dar (idadi ambayo ni ndogo) wanaochukua kwa wastani 50mn kwa kikokotoo cha zamani...hio kwenye mzunguko ni ongezeko la sh 2.5bn kila mwaka ambazo huweza ingia kwenye ujenzi, manunuzi mengineyo nakadhalika. Soko ndio hilo, siku nyingine kabla ya kubeza uliza na Hiyo ni hesabu ya watu 50 tu.
 
Back
Top Bottom