Kwa nini vyama vya wafanyakazi (TUCTA)vipo kimya kuhusiana na kanuni/sheria mpya ya mafao?

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
653
1,000
Ni karibu wiki ya pili sasa kumekuwa na mjadala kuhusiana na kanuni/sheria mpya za mafao. Mjadala huo ambao ulimuibua Spika wa Bunge Job Ndugai hata kusema kuwa bunge halistahili lawama hizo kwa kuwa wao (bunge) sio waliotunga kanuni hizo, kutokana na wadau wengi kutupia lawama zake kwa bunge, umeangazia zaidi kwenye kile kinachoitwa kikokotoo, kwamba mfanyakazi, mara tu baada ya muda wake wa kustaafu kufika, basi atachukua asilimia 25, wakati asilimia 75 atapewa kidogokidogo kwa miaka 12. Kadhalika, suala la FAO LA KUJITOA nalo limezungumziwa na kulalamikiwa na wengi, nikiwamo mimi mwandishi wa mada hii. Pamoja na malalamiko yote hayo ya wafanyakazi, ambayo chanzo chake ni Mbunge wa CHADEMA, Esther Bulaya, bado vyama vya wafanyakazi chini ya shirikisho lao ambalo ni TUCTA, vimekuwa kimya na kigugumizi kana kwamba hakuna kinachoendelea kwa wanachama wake. Je, hii ina maana gani? Ni kwamba vyama vya wafanyakazi havioni tatizo kwa hicho kinacholalamikiwa, au vinatafuta muda muafaka ili vitoe msimao wake juu ya sheria na kanuni mpya ya pensheni?
 
Prince az

JF-Expert Member
Sep 27, 2018
1,160
2,000
"Ole wake mkurugenzi amtangaze mpinzani"

Napata picha Kama panya yeyote atakae jitokeza kumfunga paka Kengere litakuwa lake ilo

ila ngoja tisubir muda nao utoe hukumu
 
pandagichiza

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
3,533
2,000
Ni karibu wiki ya pili sasa kumekuwa na mjadala kuhusiana na kanuni/sheria mpya za mafao. Mjadala huo ambao ulimuibua Spika wa Bunge Job Ndugai hata kusema kuwa bunge halistahili lawama hizo kwa kuwa wao (bunge) sio waliotunga kanuni hizo, kutokana na wadau wengi kutupia lawama zake kwa bunge, umeangazia zaidi kwenye kile kinachoitwa kikokotoo, kwamba mfanyakazi, mara tu baada ya muda wake wa kustaafu kufika, basi atachukua asilimia 25, wakati asilimia 75 atapewa kidogokidogo kwa miaka 12. Kadhalika, suala la FAO LA KUJITOA nalo limezungumziwa na kulalamikiwa na wengi, nikiwamo mimi mwandishi wa mada hii. Pamoja na malalamiko yote hayo ya wafanyakazi, ambayo chanzo chake ni Mbunge wa CHADEMA, Esther Bulaya, bado vyama vya wafanyakazi chini ya shirikisho lao ambalo ni TUCTA, vimekuwa kimya na kigugumizi kana kwamba hakuna kinachoendelea kwa wanachama wake. Je, hii ina maana gani? Ni kwamba vyama vya wafanyakazi havioni tatizo kwa hicho kinacholalamikiwa, au vinatafuta muda muafaka ili vitoe msimao wake juu ya sheria na kanuni mpya ya pensheni?
Vyama vya wafanyakazi walishiriki katika mchakato mzima wa ufungaji wa sheria hii tangu mwaka 2012
 
CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
653
1,000
Vyama vya wafanyakazi walishiriki katika mchakato mzima wa ufungaji wa sheria hii tangu mwaka 2012
Kama walishiriki tangu 2012, lakini wahusika wakuu ambao ni wafanyakazi hawakubaliani kwa kiasi kikubwa na kanuni/sheria hiyo, huoni hapo kuna tatizo?
 
LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,025
2,000
Vyama Vya Wafanyakazi Vime Paralyse Na Ku Collapse Havina Nguvu Tena Kuikoromea Serikali. Kama Vyama Vya Siasa Haviwezi Je Vya Wafanyakazi Vitaanzaje? Vyama Vingine Vya Kiraia Navyo Havina Ujasiri Wa Kusema Jambo Hilo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom