Wafanyakazi Tanzania ivunjeni TUCTA!!

Wafanyakazi Tanzania ivunjeni TUCTA!!

TUCTA ni tawi la ccm linalowanyonya wafanya kazi,
Haijawahi kuwatetea zaidi ya kuitetea serikali
 
Hata kwenye siasa hulazimishwi kujiunga. Ushiriki wa vyama vya wafanyakazi ni hiyari. Hoja yako ya kuivunja TUCTA ni mufilisi
Acha kujibu pumba mkuu jenga hoja. Hajasema kuvunja TUCTA, hoja suala ni kukosekana option kama wakati wa chama kimoja watu wasiokua CCM walikosa mbadala na wala sio kuivunja CCM
 
Chama chochote cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu, ni mhimili ulio kati kuangalia maslahi ya Mwajiriwa na Mwajiri. Lakini kwa kuwa vyama vya wafanyakazi hapa nchini mwetu Historia yake inafungamanishwa na siasa za nchi hii, vimekuwa kama ni sehemu ya Mwajiri na kazi yake kubwa imekuwa ni "kuwaelewesha" wafanyakazi ni kwa nini jambo fulani linashindikana kutekelezwa na Mwajiri.

TUCTA ambayo ni kama shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania, imekuwa haionekani kama inafanya jambo lolote la maana kwa maslahi ya wafanyakazi zaidi ya kuandaa sherehe za Mei Mosi na kuandika risala ndeefu ambayo atasomewa "Mgeni Rasmi" ambaye mara nyingi kama si zote hutoka serikali na aghalabu huwa Rais wa Nchi!

Baada ya "majibu" ya Mgeni Rasmi TUCTA huondoka na kusubiri tena mwaka unaofutia kuleta tena malalamiko yao kwa "Mwajiri Mkuu" na kama kawaida hutolewa ahadi na mwisho wa siku hakuna kinachobadilika! Hivi TUCTA kazi yake ni hiyo tu ya kuandaa sikukuu ya Mei Mosi?

Msimamo wa TUCTA kuhusu kwa mfano kwa mambo kama kusimamishwa kwa wafanyakazi kutokupandishwa daraja, kuzuiwa kubadili aina yaka kazi, kutumiwa kwa fedha za mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa miradi ambayo wafanyakazi hawafaidiki nayo, wafanyakazi wa sekta binafsi kukosa mikataba inayoeleweka na kazi zinazotakiwa kufanywa na watanzania kufanywa na watu wa nchi za nje ukoje?

Hivi leo TUCTA ikivunjwa ni kitu gani ambacho wafanyakazi wa Tanzania watakikosa kwa kutokuwepo kwa TUCTA? Wakati naangalia Mgomo wa Madaktari na Waalimu kule Kenya, nikajiuliza kama sisi Tanzania tuna vyama vya wafanyakazi imara kama vya wenzetu Kenya ambavyo vinaweza kuendesha migomo kwa siku zaidi ya 100 bila ya kutetereka!!
Mfanyakazi wa kuiwajibisha TUCTA yuko wapi?Ndio maana huwa nasema siielewi logic ya Watanganyika wenzangu.Zanzibaris are better.Sijui sisi walizidisha Aluminium na Thimerosal(Mercury)
kwenye chanjo!?
 
Acha kujibu pumba mkuu jenga hoja. Hajasema kuvunja TUCTA, hoja suala ni kukosekana option kama wakati wa chama kimoja watu wasiokua CCM walikosa mbadala na wala sio kuivunja CCM
TUCTA Ni shirikisho la vyama Na Ni hiyari kujiunga. Hujui hata unachotetea Wala kubishia
 
Chama chochote cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu, ni mhimili ulio kati kuangalia maslahi ya Mwajiriwa na Mwajiri. Lakini kwa kuwa vyama vya wafanyakazi hapa nchini mwetu Historia yake inafungamanishwa na siasa za nchi hii, vimekuwa kama ni sehemu ya Mwajiri na kazi yake kubwa imekuwa ni "kuwaelewesha" wafanyakazi ni kwa nini jambo fulani linashindikana kutekelezwa na Mwajiri.

TUCTA ambayo ni kama shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania, imekuwa haionekani kama inafanya jambo lolote la maana kwa maslahi ya wafanyakazi zaidi ya kuandaa sherehe za Mei Mosi na kuandika risala ndeefu ambayo atasomewa "Mgeni Rasmi" ambaye mara nyingi kama si zote hutoka serikali na aghalabu huwa Rais wa Nchi!

Baada ya "majibu" ya Mgeni Rasmi TUCTA huondoka na kusubiri tena mwaka unaofutia kuleta tena malalamiko yao kwa "Mwajiri Mkuu" na kama kawaida hutolewa ahadi na mwisho wa siku hakuna kinachobadilika! Hivi TUCTA kazi yake ni hiyo tu ya kuandaa sikukuu ya Mei Mosi?

Msimamo wa TUCTA kuhusu kwa mfano kwa mambo kama kusimamishwa kwa wafanyakazi kutokupandishwa daraja, kuzuiwa kubadili aina yaka kazi, kutumiwa kwa fedha za mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa miradi ambayo wafanyakazi hawafaidiki nayo, wafanyakazi wa sekta binafsi kukosa mikataba inayoeleweka na kazi zinazotakiwa kufanywa na watanzania kufanywa na watu wa nchi za nje ukoje?

Hivi leo TUCTA ikivunjwa ni kitu gani ambacho wafanyakazi wa Tanzania watakikosa kwa kutokuwepo kwa TUCTA? Wakati naangalia Mgomo wa Madaktari na Waalimu kule Kenya, nikajiuliza kama sisi Tanzania tuna vyama vya wafanyakazi imara kama vya wenzetu Kenya ambavyo vinaweza kuendesha migomo kwa siku zaidi ya 100 bila ya kutetereka!!

Pia leo hii kuna utata mkubwa kuhusu michango ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii. Inaeleweka kuwa, kwa sababu ya usalama mdodo wa ajira " job insecurity" mifuko mingi iliweka fao la kujitoa " withdrawal benefit". Kwa sasa hali ni mbaya zaidi kuhusu usalama wa ajira sokoni , watu wengi wanasimamishwa kazi, makampuni yanafungwa,- kwa kweli mahitaji ya fao hili ni makubwa zaidi kuliko kipindi chochote kile huko nyuma
 
TUCTA ni janga kama yalivyo majanga mengine. Wafanyakzi wanastaafu fedha zao wanapewa kwa awamu hii ni haki? Fedha mtu akatwe miaka hadi 30 leo unampangia matumizi eti apewe kwa awamu? Mateso kwa mfanyakazi wa nchi hadi lini jamani? Hii inauma sana sana.
 
Duniani hakuna haki, kuna "mazingira pendwa" tu.
 
Wafanyakaz wa nchi gani? Tanzania! Sahau!

The majority of Tanzanian workers ni mazwazwa wasiojitambua....!!!Sijui kama ni NJAA au ni UJINGA...!!
Wewe jaribu tu kulinganisha na wenzetu wa nchi jirani kama Kenya na Uganda, you can really see the difference...!!!
 
Kwa sababu hakuna mbadala na kwa kuwa hakuna uwezekano wa kubadili mfumo uliopo angalau kwa sasa, mimi niliamua kutokuwa mwanachama ili kuokoa vijisenti vyangu ambavyo ningekatwa kila mwezi!
Ni kweli kwamba wanachama wa TUCTA ndio wanaifanya iwepo kuipitia vyama vya kisekta, na sheria ya kazi ya mwaka 2004 ambay ilianza kutumika mwaka 2006 baada ya kukamilika kwa uandaaji wa procedure za utekelezaji wa sheria yenyewe.
Sheria hii imetoa maelekezo ya namna ya kuingia na kutoka kwenye Union - unaingia kwa kujaza fomu ya kuidhinisha makato na unajitoa kwa kujaza fomu maalumu ya kusitisha makato ya asilimia mbili ya mshahara wako kwa kumpelekea Mwajiri na katibu wa Tawi la chama husika mahali pa kazi. Ni rahisi kiasi hicho. Na mara wafanyakazi wengi watakapositisha makato na chama kukosa idadi ya wanachama wanaotakiwa kisheria kuunda TAwi, Tawi hilo linakuwa halipo.
Wafanyakazi tusilalamike tuchukue hatua ili hawa viongozi wa vyama vya wafanyakazi wajitambue, na vinginevyo saa yaja ambayo yatawakuta haya.
Lakini pia uimara wa Union yoyote inatokana na uimara wa wanachama wake pia - wanaojua wajibu wao na haki yao kutoka kwenye chama husika na pia wanajua namna ya kuzidai haki zao. Kiongozi wa chama cha waafanyakazi anakuwa imara pale anapokuwa na wanachama walio imara - kwamba ana backing ya wanachama na anapotangulia mbele anajua ana support kweli ya wanachama wake. Na shida kubwa iko hapo - vyama viko dhaifu kwa sababu ya udhaifu wa wanachama wake.
 
Pia leo hii kuna utata mkubwa kuhusu michango ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii. Inaeleweka kuwa, kwa sababu ya usalama mdodo wa ajira " job insecurity" mifuko mingi iliweka fao la kujitoa " withdrawal benefit". Kwa sasa hali ni mbaya zaidi kuhusu usalama wa ajira sokoni , watu wengi wanasimamishwa kazi, makampuni yanafungwa,- kwa kweli mahitaji ya fao hili ni makubwa zaidi kuliko kipindi chochote kile huko nyuma
Ni kweli kabisa mkuu, yaani dhuluma tuliyofanyiwa kwenye fao la kujitoa basi tu. Sijui haya ma TUCTA kazi yao nini, hotuba ndefuuu kila mwaka pumba tupu. Wameshindwa kabisa kutetea wafanyakazi
 
Endeleeni kutuona machizi sisi tunaotaka muivunje TUCTA, lakini mnaoumia ni nyie!!
 
Back
Top Bottom