Wafanyakazi Tanzania ivunjeni TUCTA!!

Wafanyakazi Tanzania ivunjeni TUCTA!!

Kati ya uongozi uliofeli wa chama cha wafanyakazi kimojawapo pamoja na vienzie vinavyoshirikishwa vimekuwa vinaimba ngonjera kila kukicha! Katika association ilisimama ni TLS vingine tunaweza kusema donor association
 
Kuna wakati nawaza sana kuhusu umuhimu wa kuwa na vyama vya wafanyakazi hadi kichwa kinauma. Hivi ilikuwaje Rais wa TUCTA, ndugu Yahaya Msigwa na genge lake wakakubali kushirikiana na serikali kupora mafao ya wastaafu? Nilimsikia mimi mwenyewe akinukuliwa na gazeti la Nipashe na alikiri kuwa TUCTA walipambana sana kuhakikisha kuwa sheria hii kandamizi inatungwa. Sikuamini masikio yangu.

Yaani mfanyakazi ateseke kwa miaka 40 ya kuitumikia nchi kwa uaminifu halafu fedha zake alizodunduliza kwa muda mrefu hivyo, zibaki serikalini alipwe kidogo kidogo? Hivi huu upuuzi unaingia akilini kweli? Miaka 60 sio miaka ya kula maisha. Hii ni miaka ya kujiandaa kufa huku ukijipoza na fedha zako ulizochuma kwa miaka mingi. Sasa serikali inafahamu kuwa wastaafu wengi hawaishi maisha marefu ndio maana ikaamua kutunga hiio sheria ya kishetani (kwa kushirikiana na vyama vya wafanyakazi) ili kufisidi fedha za wastaafu.

Inaaminika kwamba serikali ilitumia nguvu nyingi sana kuchomeka makada wake ndani ya vyama vya wafanyakazi, (including Dr Msigwa wa TUCTA) ili muwasaidie kudhulumu haki za wastaafu. Dhuluma ni mbaya. Wote waliohusika na hujuma hii ovu wamelaniwa pamoja na vizazi vyao vyote. Najua kwamba mimi ni mmoja wa maelfu ya wapiga kelele mnaotuchukulia kama mbwa wabwekao bila kung’ata lakini naamini Mungu anawaona.
 
View attachment 497310

Katibu Mkuu wa TUCTA Yahya Msigwa akikabidhiwa fomu ya Kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kura ya maoni ndani ya CCM mwaka 2015. Jee litakapokuja suala la kuhatarisha maslahi ya chama chake kuendelea kubaki madarakani dhidi ya yale ya wafanyakazi atasisimama upande upi? Kwa sasa ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa.
Asante kwa ushahidi mwanana .
 
Wakati wa mjadala wa sheria hii mpya bungeni, wabunge wa Upinzani walitaka kikokotoo kiwekwe hadharani lakini wabunge wa CCM walikataa na kupiga kura ya NDIYOOOOOOOOOOOOO!! ili kuisadia serikali yao ya kifisadi kupora mafao ya wastaafu. Mpaka hapo mtu muelewa alishajua MBAYA wake ni nani. Halafu uchaguzi ukifika hawa miknd wanakuja kuwahonga walalahoi wawape kura! Inauma sana.
 
Chama chochote cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu, ni mhimili ulio kati kuangalia maslahi ya Mwajiriwa na Mwajiri. Lakini kwa kuwa vyama vya wafanyakazi hapa nchini mwetu Historia yake inafungamanishwa na siasa za nchi hii, vimekuwa kama ni sehemu ya Mwajiri na kazi yake kubwa imekuwa ni "kuwaelewesha" wafanyakazi ni kwa nini jambo fulani linashindikana kutekelezwa na Mwajiri.

TUCTA ambayo ni kama shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania, imekuwa haionekani kama inafanya jambo lolote la maana kwa maslahi ya wafanyakazi zaidi ya kuandaa sherehe za Mei Mosi na kuandika risala ndeefu ambayo atasomewa "Mgeni Rasmi" ambaye mara nyingi kama si zote hutoka serikali na aghalabu huwa Rais wa Nchi!

Baada ya "majibu" ya Mgeni Rasmi TUCTA huondoka na kusubiri tena mwaka unaofutia kuleta tena malalamiko yao kwa "Mwajiri Mkuu" na kama kawaida hutolewa ahadi na mwisho wa siku hakuna kinachobadilika! Hivi TUCTA kazi yake ni hiyo tu ya kuandaa sikukuu ya Mei Mosi?

Msimamo wa TUCTA kuhusu kwa mfano kwa mambo kama kusimamishwa kwa wafanyakazi kutokupandishwa daraja, kuzuiwa kubadili aina yaka kazi, kutumiwa kwa fedha za mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa miradi ambayo wafanyakazi hawafaidiki nayo, wafanyakazi wa sekta binafsi kukosa mikataba inayoeleweka na kazi zinazotakiwa kufanywa na watanzania kufanywa na watu wa nchi za nje ukoje?

Hivi leo TUCTA ikivunjwa ni kitu gani ambacho wafanyakazi wa Tanzania watakikosa kwa kutokuwepo kwa TUCTA? Wakati naangalia Mgomo wa Madaktari na Waalimu kule Kenya, nikajiuliza kama sisi Tanzania tuna vyama vya wafanyakazi imara kama vya wenzetu Kenya ambavyo vinaweza kuendesha migomo kwa siku zaidi ya 100 bila ya kutetereka!!
Hii Mada ni Kali sana sana Umeandika Nondo madini matupu Aiseee,Basi tuu,sema Bahati Mbaya tumelaaniwa wafanyakazi hawezi Kukusikia Mkuu,labda itokee miujiza,Wafanyakazi Mwenyewe wametungiwa Sheria Kandamizi Mnoo,Wakati Mfanyakazi Hana Mataji,hana Hela,Hana nguvu,anategemea Sheria ndo imlinde,wakati uhalisia Watungaji Sheria ndo wanamkandamiza,Samahani wafanyakazi wa Kiafrika ni wa Kupigwa tuu na Fimbo,kwani watafanyaje?kwani wamewahi kufanya nini!?
Anyway wafanyakazi Bana,Wakuswaga tuu.
 
Chama chochote cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu, ni mhimili ulio kati kuangalia maslahi ya Mwajiriwa na Mwajiri. Lakini kwa kuwa vyama vya wafanyakazi hapa nchini mwetu Historia yake inafungamanishwa na siasa za nchi hii, vimekuwa kama ni sehemu ya Mwajiri na kazi yake kubwa imekuwa ni "kuwaelewesha" wafanyakazi ni kwa nini jambo fulani linashindikana kutekelezwa na Mwajiri.

TUCTA ambayo ni kama shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania, imekuwa haionekani kama inafanya jambo lolote la maana kwa maslahi ya wafanyakazi zaidi ya kuandaa sherehe za Mei Mosi na kuandika risala ndeefu ambayo atasomewa "Mgeni Rasmi" ambaye mara nyingi kama si zote hutoka serikali na aghalabu huwa Rais wa Nchi!

Baada ya "majibu" ya Mgeni Rasmi TUCTA huondoka na kusubiri tena mwaka unaofutia kuleta tena malalamiko yao kwa "Mwajiri Mkuu" na kama kawaida hutolewa ahadi na mwisho wa siku hakuna kinachobadilika! Hivi TUCTA kazi yake ni hiyo tu ya kuandaa sikukuu ya Mei Mosi?

Msimamo wa TUCTA kuhusu kwa mfano kwa mambo kama kusimamishwa kwa wafanyakazi kutokupandishwa daraja, kuzuiwa kubadili aina yaka kazi, kutumiwa kwa fedha za mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa miradi ambayo wafanyakazi hawafaidiki nayo, wafanyakazi wa sekta binafsi kukosa mikataba inayoeleweka na kazi zinazotakiwa kufanywa na watanzania kufanywa na watu wa nchi za nje ukoje?

Hivi leo TUCTA ikivunjwa ni kitu gani ambacho wafanyakazi wa Tanzania watakikosa kwa kutokuwepo kwa TUCTA? Wakati naangalia Mgomo wa Madaktari na Waalimu kule Kenya, nikajiuliza kama sisi Tanzania tuna vyama vya wafanyakazi imara kama vya wenzetu Kenya ambavyo vinaweza kuendesha migomo kwa siku zaidi ya 100 bila ya kutetereka!!
Lazma ujue kuwa tuko kwenye ujima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom