Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,844
- 39,577
Chama chochote cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu, ni mhimili ulio kati kuangalia maslahi ya Mwajiriwa na Mwajiri. Lakini kwa kuwa vyama vya wafanyakazi hapa nchini mwetu Historia yake inafungamanishwa na siasa za nchi hii, vimekuwa kama ni sehemu ya Mwajiri na kazi yake kubwa imekuwa ni "kuwaelewesha" wafanyakazi ni kwa nini jambo fulani linashindikana kutekelezwa na Mwajiri.
TUCTA ambayo ni kama shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania, imekuwa haionekani kama inafanya jambo lolote la maana kwa maslahi ya wafanyakazi zaidi ya kuandaa sherehe za Mei Mosi na kuandika risala ndeefu ambayo atasomewa "Mgeni Rasmi" ambaye mara nyingi kama si zote hutoka serikali na aghalabu huwa Rais wa Nchi!
Baada ya "majibu" ya Mgeni Rasmi TUCTA huondoka na kusubiri tena mwaka unaofutia kuleta tena malalamiko yao kwa "Mwajiri Mkuu" na kama kawaida hutolewa ahadi na mwisho wa siku hakuna kinachobadilika! Hivi TUCTA kazi yake ni hiyo tu ya kuandaa sikukuu ya Mei Mosi?
Msimamo wa TUCTA kuhusu kwa mfano kwa mambo kama kusimamishwa kwa wafanyakazi kutokupandishwa daraja, kuzuiwa kubadili aina ya kazi, kutumiwa kwa fedha za mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa miradi ambayo wafanyakazi hawafaidiki nayo, wafanyakazi wa sekta binafsi kukosa mikataba inayoeleweka na kazi zinazotakiwa kufanywa na watanzania kufanywa na watu wa nchi za nje ukoje?
Hivi leo TUCTA ikivunjwa ni kitu gani ambacho wafanyakazi wa Tanzania watakikosa kwa kutokuwepo kwa TUCTA? Wakati naangalia Mgomo wa Madaktari na Waalimu kule Kenya, nikajiuliza kama sisi Tanzania tuna vyama vya wafanyakazi imara kama vya wenzetu Kenya ambavyo vinaweza kuendesha migomo kwa siku zaidi ya 100 bila ya kutetereka!!