Wafanyakazi Tanzania ivunjeni TUCTA!! | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi Tanzania ivunjeni TUCTA!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Allen Kilewella, Apr 17, 2017.

 1. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #1
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,227
  Likes Received: 10,086
  Trophy Points: 280
  Chama chochote cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu, ni mhimili ulio kati kuangalia maslahi ya Mwajiriwa na Mwajiri. Lakini kwa kuwa vyama vya wafanyakazi hapa nchini mwetu Historia yake inafungamanishwa na siasa za nchi hii, vimekuwa kama ni sehemu ya Mwajiri na kazi yake kubwa imekuwa ni "kuwaelewesha" wafanyakazi ni kwa nini jambo fulani linashindikana kutekelezwa na Mwajiri.

  TUCTA ambayo ni kama shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania, imekuwa haionekani kama inafanya jambo lolote la maana kwa maslahi ya wafanyakazi zaidi ya kuandaa sherehe za Mei Mosi na kuandika risala ndeefu ambayo atasomewa "Mgeni Rasmi" ambaye mara nyingi kama si zote hutoka serikali na aghalabu huwa Rais wa Nchi!

  Baada ya "majibu" ya Mgeni Rasmi TUCTA huondoka na kusubiri tena mwaka unaofutia kuleta tena malalamiko yao kwa "Mwajiri Mkuu" na kama kawaida hutolewa ahadi na mwisho wa siku hakuna kinachobadilika! Hivi TUCTA kazi yake ni hiyo tu ya kuandaa sikukuu ya Mei Mosi?

  Msimamo wa TUCTA kuhusu kwa mfano kwa mambo kama kusimamishwa kwa wafanyakazi kutokupandishwa daraja, kuzuiwa kubadili aina yaka kazi, kutumiwa kwa fedha za mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa miradi ambayo wafanyakazi hawafaidiki nayo, wafanyakazi wa sekta binafsi kukosa mikataba inayoeleweka na kazi zinazotakiwa kufanywa na watanzania kufanywa na watu wa nchi za nje ukoje?

  Hivi leo TUCTA ikivunjwa ni kitu gani ambacho wafanyakazi wa Tanzania watakikosa kwa kutokuwepo kwa TUCTA? Wakati naangalia Mgomo wa Madaktari na Waalimu kule Kenya, nikajiuliza kama sisi Tanzania tuna vyama vya wafanyakazi imara kama vya wenzetu Kenya ambavyo vinaweza kuendesha migomo kwa siku zaidi ya 100 bila ya kutetereka!!
   
 2. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #41
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,227
  Likes Received: 10,086
  Trophy Points: 280
  Watoke tu!!
   
 3. lightning

  lightning JF-Expert Member

  #42
  Apr 17, 2017
  Joined: Jan 22, 2017
  Messages: 288
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 80
  Tulipo bado panakupa shida kuelewa sina uhakika kama waweza kutuelezea historia japo ya miaka 40 nyuma juu ya vyama vya wafanyakazi!
   
 4. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #43
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,227
  Likes Received: 10,086
  Trophy Points: 280
  Historia ni msingi na leo ni nyumba yenyewe. Kwani TUCTA ipo kwa maslahi yepi hasa ya wafanyakazi wanayoyapigania?
   
 5. m

  mugosha JF-Expert Member

  #44
  Apr 17, 2017
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 560
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 60
  Ni ngumu sana kwa zama hizi kumpata kiongozi yeyote kwenye taasisi yoyote ya ki hiari ambaye hana mlengo wa ki vyama vya kisiasa. Na after all watu wengi wengi wenye uthubutu wa kugombea huwa wana vielement vya politics. Na hiki hasa ndo kitakachoua nguvu ya vyama kama TUCTA. Labda ifikie mahali viwe matawi ya kisiasa ili wakati mgombea urais akijinadi awe akitueleza ni kwa namna gani TUCTA ya chama chake itatufanyia akishaingia madarakani. Vinginevyo ni hovyo kabisa.
   
 6. T

  Toosweet JF-Expert Member

  #45
  Apr 17, 2017
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 1,170
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 280
  Kweli tupu
   
 7. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #46
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,227
  Likes Received: 10,086
  Trophy Points: 280
  Usichokielewa ni kwamba kama una maslahi kuwili (Conflict of interest) ni lazima kwanza utangaze ni maslahi yepi uliyo nayo kwneye jambo husika. Kwa mfano Marekani maslahi ya kila Jaji yanajulikana lakini haipunguzi wala kuondoa kwamba wao ni Majaji na hukumu zao huwa zinajulikana kabla ya kutolewa.

  Kwa muktadha huo huwezi kuniambia huyu Katibu Mkuu wa TUCTA maslahi yake ndani ya CCM hayawezi kuathiri msimamo wake litakapokuja suala la kuamua kusimamia maslahi ya wafanyakazi dhidi ya Serikali inayoongozwa na chama chake!!
   
 8. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #47
  Apr 17, 2017
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,468
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  Dogo soma upya sheria ya ajira na mahusiano kazini 2004
   
 9. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #48
  Apr 17, 2017
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,468
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  Hujajibu swali. Nioneshe kifungu cha sheria kinachomlazimisha mfanyakazi kujiunga na chama cha wafanyakazi
   
 10. p

  peno hasegawa Member

  #49
  Apr 17, 2017
  Joined: Feb 24, 2016
  Messages: 64
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  Hat
  Hata cwt Ni ya kuvunja pia
   
 11. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #50
  Apr 18, 2017
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,586
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
 12. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #51
  Apr 18, 2017
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  hivi wabunge wana fao la kujitoa?
   
 13. p

  pambe samanini Senior Member

  #52
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 27, 2015
  Messages: 174
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Wao wenyewe wanaogopa kufukuzwa kazi
   
 14. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #53
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,586
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Sasa TUCTA wameongea nini na Rais? Watuambie

  Je Fao la Kujitoa? nini msimamo wa Rais?
   
 15. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #54
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,227
  Likes Received: 10,086
  Trophy Points: 280
  Siri yao!!
   
 16. G

  Glycel JF-Expert Member

  #55
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 14, 2017
  Messages: 275
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Mh
   
 17. m

  mawelewele JF-Expert Member

  #56
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 17, 2016
  Messages: 274
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Tucta in takakata kabisa na mtoto wao Cwt ,pumbavu kabisa hawa watu.
   
 18. m

  mawelewele JF-Expert Member

  #57
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 17, 2016
  Messages: 274
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Hakuna uhiyari wowote,ukiingia tu kwenye automatically pesa yako inaanzwa kukatwa km cwt
   
 19. p

  peno hasegawa Member

  #58
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 24, 2016
  Messages: 64
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  cwt umesahau ni ya kufuta
   
 20. p

  peno hasegawa Member

  #59
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 24, 2016
  Messages: 64
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  cwt ni pepo
   
 21. M

  Mwisenge1993 JF-Expert Member

  #60
  Apr 21, 2017
  Joined: Jul 2, 2016
  Messages: 903
  Likes Received: 561
  Trophy Points: 180
  Kama unajua watakusaidia unalalamika nini sasa au shida yako unataka wewe wanaitukana serekali hizo ni Trade Unions za kizamani
   
Loading...