Wafanyakazi Tanzania ivunjeni TUCTA!!

Wafanyakazi Tanzania ivunjeni TUCTA!!

Hahaha nliandikaga kuhusu TUCTA watu wakapinga vita ila hii ni moja ya vibaraka wa serikali ili iweze kumanyuva bila resistance yoyote ,kuhusu swala la 15% jamaaa aliongea na kukaaa kimya mpaka Leo sijui tarehe moja wana kuja na slogan gan
 
TUCTA inatakiwa izaliwe upya kama TLS.Wafanyakazi angalieni namna ya kutoa hao makada ili mpate watetezi wa kweli.
Ingine msimamo wa wenzenu mawakili,,ikipindi wafukuzeni hao viongozi ili mchague wenye msimamo,wasio makada
Nilidhani tumemtoa Mgaya Maneno tutafaidi sasa ameingia visa na mkasa
 
Tanzania sio Chama cha madactari, cwt, erb,tuico vyote serikali huakikisha vinaweka makada ili serikali isipate upinzani kwenye mambo yake ni kawaida sema hapa kwetu too much
 
Sina uhakika kama wewe ni mfanyakazi....na kama ni mfanyakazi basi ndio wale ambao wanakimbia kuwa hata viongozi wa wafanyakazi mahali pa kazi kwa visingizio vya kuogopa kupoteza ajira.
Lete hoja ya kuimarisha umoja wa wafanyakazi na sio kubomoa. UMETUMWA??
Kabla ya kuuliza chama cha wafanyakazi kitakufanyia nini, jiuliza binafsi utakifanyia nini?
Ukijitenganisha kuwa kuna chama kisha kuna wewe unajipotosha.
Amka mfanyakazi!!!
Hakuna kitu wanafanya hawa tucta kweli serikali ikiamua jambo linaamua kichama lipo tu limapata 2% zetu bora lipigwe chini tuelewe moja
 
Tujiulize TUCTA kila tarehe moja wamefanya nini kikafuatwa na serikali na wao kama wao wamechukua hatua gani yani hiki ni hewa kabisa na matawi yao wanasubiri tu 2% za wafanyakazi, wanasubiri tarehe moja wawape wafanyakazi matumaini ta uwongo washangiliiie ipite afu hakuna kinachofanyika mpaka mwaka ni tena waongea kingine yani business as usual no changes na hakuna namna hata ya kupima ufanisi wa haya machama ya kinyonyaji
 
Yani MTU anakula hela yako na inajulikana kabisa hafanyi chochote hata ukifukuzwa kazi usipoenda na hela tena ili wakutete imekula kwani namwimba Magu angalia sana bora hata hela tunayokatwa iende kwenye maendeleo ya nchi
 
Kama unajua watakusaidia unalalamika nini sasa au shida yako unataka wewe wanaitukana serekali hizo ni Trade Unions za kizamani
Wapi nimesema kuwa TUCTA iwe inaitukana Serikali? Novemba mwaka jana Marubani wa shirika la Ndege la Lufthansa la Ujerumani waligoma na wakaongezewa mshahara wao. Wewe unasema eti ni "Trade Unions" za Kizamani. Huo usasa unafanyikaje kwenye kudai maslahi?
 
Haina umuhimu wa kuendelea kuwepo hii. Hakuna lolote wanalolifanya kutetea wafanyakazi nchini.

Chama chochote cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu, ni mhimili ulio kati kuangalia maslahi ya Mwajiriwa na Mwajiri. Lakini kwa kuwa vyama vya wafanyakazi hapa nchini mwetu Historia yake inafungamanishwa na siasa za nchi hii, vimekuwa kama ni sehemu ya Mwajiri na kazi yake kubwa imekuwa ni "kuwaelewesha" wafanyakazi ni kwa nini jambo fulani linashindikana kutekelezwa na Mwajiri.

TUCTA ambayo ni kama shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania, imekuwa haionekani kama inafanya jambo lolote la maana kwa maslahi ya wafanyakazi zaidi ya kuandaa sherehe za Mei Mosi na kuandika risala ndeefu ambayo atasomewa "Mgeni Rasmi" ambaye mara nyingi kama si zote hutoka serikali na aghalabu huwa Rais wa Nchi!

Baada ya "majibu" ya Mgeni Rasmi TUCTA huondoka na kusubiri tena mwaka unaofutia kuleta tena malalamiko yao kwa "Mwajiri Mkuu" na kama kawaida hutolewa ahadi na mwisho wa siku hakuna kinachobadilika! Hivi TUCTA kazi yake ni hiyo tu ya kuandaa sikukuu ya Mei Mosi?

Msimamo wa TUCTA kuhusu kwa mfano kwa mambo kama kusimamishwa kwa wafanyakazi kutokupandishwa daraja, kuzuiwa kubadili aina yaka kazi, kutumiwa kwa fedha za mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa miradi ambayo wafanyakazi hawafaidiki nayo, wafanyakazi wa sekta binafsi kukosa mikataba inayoeleweka na kazi zinazotakiwa kufanywa na watanzania kufanywa na watu wa nchi za nje ukoje?

Hivi leo TUCTA ikivunjwa ni kitu gani ambacho wafanyakazi wa Tanzania watakikosa kwa kutokuwepo kwa TUCTA? Wakati naangalia Mgomo wa Madaktari na Waalimu kule Kenya, nikajiuliza kama sisi Tanzania tuna vyama vya wafanyakazi imara kama vya wenzetu Kenya ambavyo vinaweza kuendesha migomo kwa siku zaidi ya 100 bila ya kutetereka!!
 
Tarehe moja utaona watu watajavyoanikwa juani na kupewa hopes maskini ndo maana sinaga time na haya masikuukuu yani ni upotezaji muda
 
Kama unajua watakusaidia unalalamika nini sasa au shida yako unataka wewe wanaitukana serekali hizo ni Trade Unions za kizamani

Kazi ya TRADE UNION sio kutukana serikali...Umefikiri vibaya

kazi ya Vyama vya wafanyakazi ni kutetea haki za wafanyakazi...Likizo, madaraja, mafao, haki za kusoma

Inaonekana wewe hujawahi hata kufanya kazi popote (labda ni Form 4 Div 5)

TUCTA wananyamaza kimya pale wafanyakazi wanapoonewa, kuburuzwa na FAO LA KUJITOA
 
hizi trade union kwa africa zingeishiaga kule kule kwenye kudai uhuru sasa hv ni matawi Ya vyama tu
 
hizi trade union kwa africa zingeishiaga kule kule kwenye kudai uhuru sasa hv ni matawi Ya vyama tu
Mbali ya kuwa ni matawi ya vyama vya siasa lakini pia hazina taathira kwa walioko madarakani. Hebu angalia Mgomo huu wa marubani huko Ujerumani na nini kilitokea baada ya mgomo! Jee kuna tishio lilitolewa kuwa watafukuzwa kazi eti kwa kuwa wamegoma?


Lufthansa (LHAG.DE) is cancelling around 1,700 flights over the next two days due to a fresh strike by pilots in a long-running dispute about pay.

Last week, the German carrier canceled nearly 2,800 flights during a four-day walkout from Wednesday that affected more than 350,000 passengers, the 14th walkout in a dispute that since early 2014 has cost the carrier hundreds of millions of euros.

Lufthansa has offered to increase the pilots' pay by 4.4 percent in two installments and make a one-off payment worth 1.8 months' pay over a six year period.

Union Vereinigung Cockpit (VC) wants an average annual pay rise of 3.7 percent for 5,400 pilots over a five-year period backdated to 2012.

VC rejected the latest pay offer from Lufthansa late on Friday.

The pilots announced on Sunday plans to strike on short-haul routes on Tuesday and both short- and long-haul flights on Wednesday. Lufthansa said it was cancelling 816 and 890 flights on those days, respectively, affecting a total of around 180,000 passengers.

The carrier has asked a labor court in Munich to issue a temporary injunction to avert the strike, with a ruling likely due later on Monday. Last week, a labor court in Frankfurt rejected a similar request for an injunction.

Chanzo: Reuters
 
Narudia tena kutoa wito wangu kwa wafanyakazi wa Tanzania kuungana kwa pamoja dhidi ya TUCTA!
 
Kama kusoma hamjui hata picha kutazama tu hamuwezi? Hao TUCTA ingawa ofisi zao haziko Lumumba lakini kuna kila dalili kwamba wanapokea maagizo kutoka huko!
 
Hkuna kuongeza mshahara wala kupandishwa mishahara na mazingira ya wafanyakazi kwenye sekta binafsi ni mabaya sana lakini TUCTA wako kimya tu!
 
Back
Top Bottom