Wafanyakazi Tanzania ivunjeni TUCTA!! | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi Tanzania ivunjeni TUCTA!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Allen Kilewella, Apr 17, 2017.

 1. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #1
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,796
  Likes Received: 11,127
  Trophy Points: 280
  Chama chochote cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu, ni mhimili ulio kati kuangalia maslahi ya Mwajiriwa na Mwajiri. Lakini kwa kuwa vyama vya wafanyakazi hapa nchini mwetu Historia yake inafungamanishwa na siasa za nchi hii, vimekuwa kama ni sehemu ya Mwajiri na kazi yake kubwa imekuwa ni "kuwaelewesha" wafanyakazi ni kwa nini jambo fulani linashindikana kutekelezwa na Mwajiri.

  TUCTA ambayo ni kama shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania, imekuwa haionekani kama inafanya jambo lolote la maana kwa maslahi ya wafanyakazi zaidi ya kuandaa sherehe za Mei Mosi na kuandika risala ndeefu ambayo atasomewa "Mgeni Rasmi" ambaye mara nyingi kama si zote hutoka serikali na aghalabu huwa Rais wa Nchi!

  Baada ya "majibu" ya Mgeni Rasmi TUCTA huondoka na kusubiri tena mwaka unaofutia kuleta tena malalamiko yao kwa "Mwajiri Mkuu" na kama kawaida hutolewa ahadi na mwisho wa siku hakuna kinachobadilika! Hivi TUCTA kazi yake ni hiyo tu ya kuandaa sikukuu ya Mei Mosi?

  Msimamo wa TUCTA kuhusu kwa mfano kwa mambo kama kusimamishwa kwa wafanyakazi kutokupandishwa daraja, kuzuiwa kubadili aina yaka kazi, kutumiwa kwa fedha za mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa miradi ambayo wafanyakazi hawafaidiki nayo, wafanyakazi wa sekta binafsi kukosa mikataba inayoeleweka na kazi zinazotakiwa kufanywa na watanzania kufanywa na watu wa nchi za nje ukoje?

  Hivi leo TUCTA ikivunjwa ni kitu gani ambacho wafanyakazi wa Tanzania watakikosa kwa kutokuwepo kwa TUCTA? Wakati naangalia Mgomo wa Madaktari na Waalimu kule Kenya, nikajiuliza kama sisi Tanzania tuna vyama vya wafanyakazi imara kama vya wenzetu Kenya ambavyo vinaweza kuendesha migomo kwa siku zaidi ya 100 bila ya kutetereka!!
   
 2. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #21
  Apr 17, 2017
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,990
  Likes Received: 2,667
  Trophy Points: 280
  Huulizi wafanyakazi soma sheria ya ajira na mahusiano kazini ya 2004. Unajenga hoja kwa hisia? Bavicha bana
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #22
  Apr 17, 2017
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,825
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Hawasemi lolote kuhusu FAO LA kujitoa
   
 4. Y

  Yesu anaokoa Member

  #23
  Apr 17, 2017
  Joined: Mar 9, 2017
  Messages: 11
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 5
  Yalikuwa ni makosa makubwa sana kumpa uenyekiti wa TUCTA NDGU GRATION MKOBA,ambaye ameshindwa miaka mingi kuwatetea walimu.Yupo tu kula hela za michango ya wafanyakazi ya kila mwezi, huku hafanyi chochote.Sijui ni Mhaya wa wapi! HANA UBUNIFU WOWOTE WA KUWATETEA WAFANYAKAZI. Yeye na Kamati yake Ilitakiwa wapigwe chini kimadaraka. Wanachama wa CWT wanalia, hawana mtetezi, tena huyu bwana anaenda TUCTA kuwa rais wa TUCTA, matatizo matupu. Anataka afurahishe ccm ili siku moja apewe nafasi ya kuteuliwa serikalini. Hadi sasa uone wafanyakazi tunavyowalisha hawa viongoz Wa CWT na TUCTA :KILA KATIBU WA CWT WILAYA ANAPATA MSHAHARA 3,600,000 kwa mwezi. Makatibu wa mikoa ndo usiseme, wenyeviti wanajilipa maposho ya kumwaga na vikao vya hapa na pale vya kujilipa. Sasa PAMOJA NA HAYA YOTE WANASHINDWA KUTUTETEA. WAKIANDAA MGOMO,HUWA WANAUANDAA STRATEGICALLY ILI UKIFIKIA MAHALI FULANI UFELI.
   
 5. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #24
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,796
  Likes Received: 11,127
  Trophy Points: 280
  Umesoma na swali ama umekimbilia kuangalia sare za chama na kugombea Ubunge? Likija suala ambalo litaiondoa CCM Madarakani atasisimama upande gani. Atasimama upande wa serikali ama wa wafanyakazi?

  Huoni nimetoa mfano wa COSATU na ANC. Unadhani misimamo ya COSATU zama za Apartheid na sasa inafanana?
   
 6. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #25
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,796
  Likes Received: 11,127
  Trophy Points: 280
  Usilete nadharia zako kwenye mambo ya msingi. Unadhani bila ya kulazimishwa na sheria kuna mfanyakazi angekuwa ni mwanachama wa hivyo vyama vya wafanyakazi legelege!
   
 7. MLA PANYA SWANGA

  MLA PANYA SWANGA JF-Expert Member

  #26
  Apr 17, 2017
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 2,996
  Likes Received: 3,004
  Trophy Points: 280
  Mapungufu yote yasababishayo hayo yapo ktk katiba ya nchi unategemea lipi litokee na watunga katiba unawajua.
   
 8. m

  mbogyo JF-Expert Member

  #27
  Apr 17, 2017
  Joined: Dec 16, 2012
  Messages: 229
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Inaelekea wewe ndo huna akili timamu juu ya sheria inayotumika kuanzisha na uendeshaji wa vyama vya wafanyakazi nchini
   
 9. h

  huko kwenu vipi JF-Expert Member

  #28
  Apr 17, 2017
  Joined: Jun 4, 2015
  Messages: 1,337
  Likes Received: 1,123
  Trophy Points: 280
  Hawa viongozi wa TUCTA ni watu wa ajabu sana....

  Yaan wapo wapo tu kama vigogo,yaan wanakera sana

  Kuna siku Mwenyekiti wa TUCTA alikuwa anahojiwa kwenye TV aliulizwa swali jinsi wafanyakaz wake wanavyokatwa kodi kwa maana ya zile calculations

  Yaan hajui jins wafanyakaz wake wanavyokatwa kodi nikamwona n mtu wa ajabu sana

  Je kama wafanyakaz wake wanaibiwa kwenye calculations nan atawatetea?
   
 10. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #29
  Apr 17, 2017
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,990
  Likes Received: 2,667
  Trophy Points: 280
  Ni sheria gani inatumika?
   
 11. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #30
  Apr 17, 2017
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,990
  Likes Received: 2,667
  Trophy Points: 280
  Niambie kifungu cha sheria kinachomlazimisha mfanyakazi kujiunga na chama cha wafanyakazi
   
 12. lightning

  lightning JF-Expert Member

  #31
  Apr 17, 2017
  Joined: Jan 22, 2017
  Messages: 362
  Likes Received: 579
  Trophy Points: 180
  Sina uhakika kama wewe ni mfanyakazi....na kama ni mfanyakazi basi ndio wale ambao wanakimbia kuwa hata viongozi wa wafanyakazi mahali pa kazi kwa visingizio vya kuogopa kupoteza ajira.
  Lete hoja ya kuimarisha umoja wa wafanyakazi na sio kubomoa. UMETUMWA??
  Kabla ya kuuliza chama cha wafanyakazi kitakufanyia nini, jiuliza binafsi utakifanyia nini?
  Ukijitenganisha kuwa kuna chama kisha kuna wewe unajipotosha.
  Amka mfanyakazi!!!
   
 13. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #32
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,796
  Likes Received: 11,127
  Trophy Points: 280
  Kwenye sheria kuna kitu kinaitwa hiyari yenye shurti. Kwa mfano ni hiyari kujiunga na chama cha siasa nchini lakini ni lazima ukitaka kugombea nafasi za uongozi za kisiasa ni lazima uwe mwanachama chama cha siasa. Kwa hivyo "Hiyari" ya kujiunga na chama cha siasa inageuka kuwa lazima kwani huwezi kugombea nafasi kama Uenyekiti wa mtaa/kijiji, Udiwani, Ubunge ama Urais bila kwanza kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Sijui umenielewa??
   
 14. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #33
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,796
  Likes Received: 11,127
  Trophy Points: 280
  Mi si mfanyakazi bali muuza Premende al Maaruf kama "Machinga" ila hoja yangu hapa nimeijenga juu ya msemo wa kichina usemao "Mimi siyo kuku kwa hivo siwezi kutaga mayai, lakini yai bovu nalijua".

  Vyama vya wafanyakazi duniani kote haviimarishwi kwa maneno bali kwa matendo. Kama vyenyewe matendo yake si ya kutetea wafanyakazi basi hata muwe mnavisifia mwaka mzima vitakufa tu.
  Vyama vya wafanyakazi huanzishwa kutetea maslahi ya wafanyakazi na wala wafanyakazi kuvitetea vyama bila ya vyama hivyo kuwatetea!
   
 15. lightning

  lightning JF-Expert Member

  #34
  Apr 17, 2017
  Joined: Jan 22, 2017
  Messages: 362
  Likes Received: 579
  Trophy Points: 180
  Hapo ndo mnapokosea, chama cha wafanyakazi kinaundwa na wafanyakazi wenyewe. Rejea Employment and Labour Relations Act, No. 6/2004 kifungu 8 na 9 pamoja marekebisho yake ya mwaka 2017.
  Subirini waajiri waendelee kuwaanzishia vyama ili waendelee kuwatawala.
   
 16. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #35
  Apr 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,796
  Likes Received: 11,127
  Trophy Points: 280
  Sijui kwa nini huelewi mantiki rahisi namna hii. Kwa kabla ya hiyo sheria wafanyakazi walikuwa wanaendeshaje hali zao za ajira? Hivi unafahamu nguvu aliyo nayo msajili wa vyama vya wafanyakazi na unajua idadi ya wafanyakazi wanaoweza kuunda chama chao cha wafanyakazi na wakifikisha idadi kiasi fulani inakuwa kama ni lazima kwa watu wa kada hiyo kuwa wanachama wa hicho chama? Unafahamu kuna mgogoro kati ya CWT na waalimu wengi wa sekondari.

  Kuna vyama huundwa kwa shinikizo la wafanyakazi na kuna vyama huundwa kwa maslahi ya watawala. Unataka kutuambia kwamba ni wafanyakazi wenyewe waliamua kuiua TLA na kuanzisha NUTA na walipoona NUTA haiwafai wakaanzisha JUWATA kisha wakaitupitilia mbali JUWATA na kuanzisha OTTU kabla ya kuishia kwenye TUCTA?
   
 17. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #36
  Apr 17, 2017
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,905
  Likes Received: 1,305
  Trophy Points: 280
  PESA za PPF Na NSSF ni kwa masilahi ya CHama cha Mapinduzi..

  Kujenga viwanda kisiasa halafu vinakufa

  Wapi General Tyre Arusha? Wapi Kibo March Moshi?

  Wabunge wa CCM kwa wingi wao wameamua wafanyakazi waporwe haki zao (FAO la KUJITOA)

  Kwa mazingira ya Tanzania, FAO LA KUJITOA ni muhimu sana

  Dawa Hospitalini hakuna

  Vifaa vya ujenzi ghali sana

  Mtaji ni ngumu sana kupata maana riba za benki ni kubwa sana na masharti hayabebeki

  FAO La Kujitoa ni Mtaji wa kujiajiri na kujenga nyumba ya kuishi

  Maswali: Mtu akistaafu akiwa na miaka 60, ataishi miaka mingapi tena? Una guarantee na Mwenyezi Mungu?

  Hayo mafao ya Pension ya Kila mwezi (Utalipia matibabu, chakula au Kodi ya Nyumba) is it enough?

  FAO LA KUJITOA Ni muhimu sana kwa kima cha chini

  Ajira zenyewe ziko wapi? Uchumi umedorora
   
 18. frank nyantu2

  frank nyantu2 JF-Expert Member

  #37
  Apr 17, 2017
  Joined: Jun 26, 2016
  Messages: 306
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 60
  We ndio umesema ukweli!! Viongozi wengine n mapandikizi kutoka serikalini!!
   
 19. frank nyantu2

  frank nyantu2 JF-Expert Member

  #38
  Apr 17, 2017
  Joined: Jun 26, 2016
  Messages: 306
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 60
  Kuna nini tena hapa! Maumivu matupu!!
  Wafanyakazi bado kilio kipo tena cha muda mrefu sana! We unadhani huyu atasimama kidete kuzuia sheria ya kuxuia fao la kujitoa kweli!!
   
 20. Dongo La Kiemba

  Dongo La Kiemba JF-Expert Member

  #39
  Apr 17, 2017
  Joined: Nov 5, 2013
  Messages: 1,542
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Asilimia 15 ya bodi ya mikopo ndio wangeweza kuisemea,lakini kimya mpaka Leo
   
 21. m

  mugosha JF-Expert Member

  #40
  Apr 17, 2017
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 614
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  Acha kuongopea watu, vyama vya wafanyakazi ni vya lazima siyo hiari. Hiari gani ambayo kulipa michango ni lazima? Hivi vyama vinatakiwa viwe vya hiari kwa maana kwamba wachukue tu michango ya wanachama. Ok wanajitetea eti ni lazima kuchangia kwa sababu eti lolote watakalolitetea litafaidisha wote NONSENSE. Huu ni wizi wa mchana kweupe, hakuna lolote wanalofanya zaidi ya kila mwaka kulalamikia kima cha chini utadhani watumishi wote tuko kima cha chini. Kwenye sekta binafsi pengine % kubwa ya waajiriwa wako kcc. Serikalini kcc nadhani hawawezi kuwa zaidi ya 20% ya watumishi wote na kwa hivyo it brings no sense kutupotezea muda kwa masuala ya kima cha chini kila mwaka. Halafu kuna hii issue ya CBA, tangu serikali ya 5 imeingia madarakani kumekuwa na dalili zote kwamba haiko interested na Mikataba ya hali bora makazini. TUCTA wala hawaonekani kusema lolote, wamejawa uoga kuliko hata watumishi wenyewe. Watoke ili tuanze upya.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...