Wafanyakazi ( staffs) wa NMB bank wanapwaya sana kujua huduma za mwajiri wao

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,526
Habari wadau.

Kwa zaidi ya mara 1. Nimegundua bank yetu ya makabwela inapwaya sana kwenye training za staff wao.

Zamani kidogo Kuna siku nilienda kuprocess refund ya malipo online. Staff wote niliowakuta kila mmoja alikuwa haelewi process zilivyo. Na manager alikuwa ametoka. Ilibidi nimsubiri Mpaka manager alivyokuja ndipo akanielekeza cha kufanya.

Mwaka huu tena wamenishangaza tena.. nilipita msiba wa mzazi wangu ambaye ni mteja wao wa miaka mingi. Tangu enz za nbc na nmb ni same bank.

Baada ya msiba nikaenda toa taarifa ya msiba ili wa freeze account wakati taratibu za mirathi zinaendelea mahakamani. Nikaambiwa kufunga account kunahitaji cheti cha kifo barua ya mahakama , maana mahakama ndiyo yenye haki ya kufunga account baada ya kumteua msimamiz wa mirathi . Na wakaongezea bank itatoa mkono wa pole kwa ajili ya kurudishia gharama za mazishi za mteja wao.. maana hii ipo kwenye vipengele vya benefit za account ya marehemu. Wakanionesha vipengele vyao vyote. Nikaona hicho kipengele kinaitwa NMB faraja.

Mimi nikaondoka nikarudi na kuendelea taratibu za mahakama za mirathi.

Baada ya miezi 7 mahakama ikamteua msimamiz wa mirathi. Na akaelekezwa kwenda bank zote ambazo marehemu alikuwa anazitumia akapeleke barua za mahakama na kufunga account.

Siku msimamiz wa mirathi aliyoenda nmb akakumbushia kuhusu hicho kipengele cha NMB faraja. Bank wakajibu hicho kipengele huwa kinalipa ndani ya miezi sita tu toka marehemu afariki. Sasa miezi 7 halipwi tena..

Tukauliza why wasiweke maelezo clear toka mapema kama ni miezi sita tu. Ama hata kwenye website yao walipokielezea kwa nini wameficha huo muda wa miezi sita kama kweli wana nia ya kulipa wateja wao? Wakajibu wao hawajui .

Nikagundua staffs wengi wa NMB hawatoi maelezo sahihi kwa wateja sababu hawajui huduma zao zinaendeshwaje.

Wameishia kuandika maelezo nusu tu na wakaficha miezi sita

Eligible for Free NMB Faraja Insurance cover up to TZS 2,000,000*

Nmb kwenye hili mbadilike..

Screenshot_20210821-142729_Firefox.jpg
 
Me niliwahi kuwaeleza kwenye uzi wao kuwa wafanyakazi wao hawazijui products vizuri. Halafu wengi wazee, yani wamechoka. Hata ukiwapa training unawasumbua tu.

Wanatakiwa hao wazee wawekwe back office, kazi yao iwe kuprocess cheque za wateja na kuhesabu hela jioni. Lakini kuhudumia wateja moja kwa moja ni kutudanganya.

Komaa nao mkuu, maana baada ya mzee kufariki ulitoa taarifa. Sasa kwanini hawakuweka hiyo hela miezi 6 ilipofika?

Kuna Benki flani, ukitoa taarifa ya msiba ya mtu anaemiliki akaunti katika benki hiyo, faster wanaflag hiyo akaunti kwaajili ya usalama wa pesa. Hata ikitokea mtu hajafariki siku akihitaji pesa zake atazipata na ataambiwa kuwa watu walireport umefariki
 
Hata NMB huduma zao nyingi zinauficho Ili ukatwe kimya kimya

Wanaficha ficha taarifa kwa nia gani? Ndio maana nikashangaa hata hilo fao la nmb faraja mbona wameficha taarifa ya miezi sita isizidi kwenye website yao pia

Wameishia kuandika

Eligible for Free NMB Faraja Insurance cover up to TZS 2,000,000*
 
Wanaficha ficha taarifa kwa nia gani? Ndio maana nikashangaa hata hilo fao la nmb faraja mbona wameficha taarifa ya miezi sita isizidi kwenye website yao pia

Wameishia kuandika

Eligible for Free NMB Faraja Insurance cover up to TZS 2,000,000*
Labda ukisoma mwisho utaona imeandikwa "vigezo na masharti kuzingatiwa"..
Pia pole sana kwa msiba wa mzee
 
Maelezo mengi wanawekwa kwenye TERM & CONDITION/ viandishi vidogodogo Wateja wengi hawasomi wanasaini harakaharaka pasi kuelewa wanachosainia
Wabongo wengi hatumaga muda wa kuchunguza ni kusaini tu
 
Uchawi wa Jambo huwa unakuwa kwenye Terms and Conditions,na Majority yetu huwa hatupendi kuzisoma.

Ukiuliza hapa nani alisoma terms & conditions za software za simu kabla ya ku-accept na kuendelea kutumia katika 100 unaweza kukuta 1-Maelezo ya Terms and conditions ni mengi alafu yana font ndogo ambazo zinachosha kusoma 🤣 🤣 🤣 .

Hii kitu ya NMB ipo kila mahali mpaka kwenye insurance-Na makampuni yanaelewa what they are doing na ni very legal
 
Uchawi wa Jambo huwa unakuwa kwenye Terms and Conditions,na Majority yetu huwa hatupendi kuzisoma.Ukiuliza hapa nani alisoma terms & conditions za software za simu kabla ya ku-accept na kuendelea kutumia katika 100 unaweza kukuta 1-Maelezo ya Terms and conditions ni mengi alafu yana font ndogo ambazo zinachosha kusoma 🤣 🤣 🤣 .Hii kitu ya NMB ipo kila mahali mpaka kwenye insurance-Na makampuni yanaelewa what they are doing na ni very legal
Issue ya competence ya staffs ni tatizo la Tanzania nzima-watanzania wengi hatupendi kusoma wala kujiongeza the same applies to staffs.

Example-Kwa mtu mwenye uelewa wa sheria na uelewa mpana wa kikodi akifika TRA anaweza kuwa dissapointed sana,Yan unaweza kuta mpaka manager TRA hamna kitu kichwani,TRA hamna wasomi mle ndo maana wanakimbilia kutumia Task force kulazimisha watu kukusanya kodi.

Wakikuona unajua sana mambo wanakuwa wakali sana 🤣 🤣 🤣
 
Wanaficha ficha taarifa kwa nia gani? Ndio maana nikashangaa hata hilo fao la nmb faraja mbona wameficha taarifa ya miezi sita isizidi kwenye website yao pia

Wameishia kuandika

Eligible for Free NMB Faraja Insurance cover up to TZS 2,000,000*
Its obviously hawataki upate hiyo hela, nilifiwa na mama mzazi ambaye alikuwa mteja wa siku nyingi tangu Utumishi wake (Serikalini) the same shit happen tumekuja kufunga account pamoja na kutaka kuomba hilo fao tukapewa story kama hizo na msimamizi wa mirathi akazifuata alivyorudi siku anaulizia akaambiwa muda umeisha.

Akaondoka akasema atarudi kwa ajili ya kufunga account zote mbili (saving na fixed) akaja kutueleza familia aisee kuna kaka zangu zimefyatuka wakasema kwenye hiyo saving tukatoe zote (ATM) maana fixed ilikuwa mpk mama aingie ndani mwenyewe.

Wengi tukahofia sana maana hiyo ni fraud mwisho wa siku tukakubaliana na masharti ila wanakera mnoo
 
Hiyo inaitwa Invitation to treat..wapeleke Mahakamani uone kama utawashinda kisheria..
 
Its obviously hawataki upate hiyo hela, nilifiwa na mama mzazi ambaye alikuwa mteja wa siku nyingi tangu Utumishi wake (Serikalini) the same shit happen tumekuja kufunga account pamoja na kutaka kuomba hilo fao tukapewa story kama hizo na msimamizi wa mirathi akazifuata alivyorudi siku anaulizia akaambiwa muda umeisha. Akaondoka akasema atarudi kwa ajili ya kufunga account zote mbili (saving na fixed) akaja kutueleza familia aisee kuna kaka zangu zimefyatuka wakasema kwenye hiyo saving tukatoe zote (ATM) maana fixed ilikuwa mpk mama aingie ndani mwenyewe. Wengi tukahofia sana maana hiyo ni fraud kilichotokea hao NMB watajua hawajui naishia hapa mkuu.
In short kwendana na regulation za BOT-Kufunga na ku-transfer hela za account ya deceased person ni lazima kuwe na hati ya mahakama-No shortcut on that!, na kuna muda hela ikikaa muda mrefu sana kwenye account bila akaunti kutumika,kisheria akaunti hufungwa na pesa huwa transfered BOT kwenye account maalumu.

Mlichokifanya ni against the law ku-withdraw hela kwenye account ya deceaced person without required procedures.Mkisema mfungue complaints ni lazima mtakuwa implicated na sheria sababu bank wata-rely kwenye ushahd wa financial statment ambao utaonyesha unlawful withdrawal ambayo ni contrary na sheria hvyo mlifanya fraud kama familia.

Lakini ndo hvyo tena bongo mambo mengi 🤣 🤣 🤣
 
In short kwendana na regulation za BOT-Kufunga na ku-transfer hela za account ya deceased person ni lazima kuwe na hati ya mahakama-No shortcut on that!, na kuna muda hela ikikaa muda mrefu sana kwenye account bila akaunti kutumika,kisheria akaunti hufungwa na pesa huwa transfered BOT kwenye account maalumu. Mlichokifanya ni against the law ku-withdraw hela kwenye account ya deceaced person without required procedures.Mkisema mfungue complaints ni lazima mtakuwa implicated na sheria sababu bank wata-rely kwenye ushahd wa financial statment ambao utaonyesha unlawful withdrawal ambayo ni contrary na sheria hvyo mlifanya fraud kama familia. Lakini ndo hvyo tena bongo mambo mengi 🤣 🤣 🤣
Na mambo yalikuwa mengi indeed 🤣
 
Its obviously hawataki upate hiyo hela, nilifiwa na mama mzazi ambaye alikuwa mteja wa siku nyingi tangu Utumishi wake (Serikalini) the same shit happen tumekuja kufunga account pamoja na kutaka kuomba hilo fao tukapewa story kama hizo na msimamizi wa mirathi akazifuata alivyorudi siku anaulizia akaambiwa muda umeisha. Akaondoka akasema atarudi kwa ajili ya kufunga account zote mbili (saving na fixed) akaja kutueleza familia aisee kuna kaka zangu zimefyatuka wakasema kwenye hiyo saving tukatoe zote (ATM) maana fixed ilikuwa mpk mama aingie ndani mwenyewe. Wengi tukahofia sana maana hiyo ni fraud mwisho wa siku tukakubaliana na masharti ila wanakera mnoo
Oops, Pole kwa kufiwa na mama. Ila mngeingia matatizoni sana. Kufunga account ya marehemu ni lazima muwe na hati ya mahakama na cheti cha kifo.

Hakimu anayesikiliza kesi ya mirathi atatoa order kwa barua kwenda kwa manager wa bank kumtaka afunge account ya marehemu.

Baada ya account kufungwa zile pesa zitahamishiwa BOT kuna account za mirathi za mahakama wakati mkiwa mnasubiri shauri la msingi la mirathi kumalizika mahakamani.

Ila kuna rafiki yangu alilipwa hiyo milion mbili ya mazishi ya baba yake yeye aliwahi kupeleka hati ya mahakama mienzi mitatu tangu walipomaliza msiba.

Unalipwa ukiwahi kupeleka taarifa, Muhimu muwe wa wazi mnapofungua mirathi mahakamani munaweza kumuomba hakimu hati ya dharula ili mnufaike na iyo offer.
 
Oops, Pole kwa kufiwa na mama. Ila mngeingia matatizoni sana. Kufunga account ya marehemu ni lazima muwe na hati ya mahakama na cheti cha kifo.

Hakimu anayesikiliza kesi ya mirathi atatoa order kwa barua kwenda kwa manager wa bank kumtaka afunge account ya marehemu.

Baada ya account kufungwa zile pesa zitahamishiwa BOT kuna account za mirathi za mahakama wakati mkiwa mnasubiri shauri la msingi la mirathi kumalizika mahakamani.

Ila kuna rafiki yangu alilipwa hiyo milion mbili ya mazishi ya baba yake yeye aliwahi kupeleka hati ya mahakama mienzi mitatu tangu walipomaliza msiba.

Unalipwa ukiwahi kupeleka taarifa, Muhimu muwe wa wazi mnapofungua mirathi mahakamani munaweza kumuomba hakimu hati ya dharula ili mnufaike na iyo offer.
Asante mkuu,
 
Back
Top Bottom