Je, huyu mrithi amepigwa au utaratibu ndio upo hivi?

Jan 13, 2023
92
99
Habari za wakati huu wakuu?

Nimekuja kwenu naomba muongozo juu ya hili jambo. Rafiki yangu alifiwa na Mama yake mwaka jana mwezi wa nne, mama yake alikuwa ni mtumishi wa serikali na alikuwa amebakiza miezi michache kustaafu. Kimsingi huyu binti wa marehemu kwao alizaliwa peke yake na Baba yake pia alifariki mwaka mmoja nyuma kabla ya mama yake. Baada ya msiba wa Mama yake kikao kilikaa na kumteua msimamizi wa mirathi ili afatilie na kumkabidhi mtoto wa marehemu haki za mama yake.

Miezi kadhaa baada ya msiba mtoto wa marehemu baada ya kutoka chuo na kukabidhiwa card za bank za mama yake, alikagua kwenye account za mama yake ili kuona kama mama yake aliacha chochote kwenye account yake, baada ya kukagua kuangalia salio alikuta moja kati ya account aliyokuwa anatumia Mama yake ilikuwa na zaidi ya milioni 70 kwenye account ya mama yake na hakujua zile hela mama yake amezitoa wapi maana hadi mauti yana mkuta Mama hakumwambia mwanae kama alikuwa na kiasi hicho cha fedha kwenye account yake, akaanza kutumia hiyo hela bila kuwaweka wazi ndugu zake akisikilizia process za mirathi zikamilike.

Siku zimepita taratibu za kufatilia mirathi zimeendele chini ya msimamizi wa mirathi, process za kufatilia mirathi zimechukua zaidi ya mwaka kukamilika lakini mwishoni mwa mwezi wa 9 ndio msimamizi wa mirathi amekuja na mrejesho kutoka PSSF, na kumuelezea mrithi ya kuwa mafao ya marehemu tayari yameshatoka (inamaanisha ndio zile milion 70 alizokuta jkwenye account ya mama yake baaada ya msiba) na hakuna hela yoyote amabayo taasisi (PSSF) inatakuwa kutoa kama sehemu ya mirathi, pia wakuwa na taarifa kama mwanachama wao amefariki.

Wasiwasi wangu ulianzia hapa ''Inasemekana marehemu (Mama yake) kabla ya kifo chake alikuwa ameshaanza kufatilia mafao yake na yalitoka miezi kadhaa baada ya kufariki"

Naomba kupata ufafanuzi toka kwenu maana na amini hapa kuna watu wenye uelewa mpana juu ya PSSF na utaratibu wa mirathi kwa ujumla, Mtoto wa marehemu ni msichana mdogo ambaye hana uelewa mpana kuhusu mirathi na utaratibu mzima wa PSSF.

Swali langu ni utaratibu wa kikotoo ukoje kwa wastaafu, na je, kuna hela yoyote mrithi anapaswa kupewa kutoka PSSF kama sehemu ya mirthi?
 
Habari za wakati huu wakuu?

Nimekuja kwenu naomba muongozo juu ya hili jambo. Rafiki yangu alifiwa na Mama yake mwaka jana mwezi wa nne, mama yake alikuwa ni mtumishi wa serekari na alikuwa amebakiza miezi michache kustaafu. Kimsingi huyu binti wa marehemu kwao alizaliwa peke yake na Baba yake pia alifariki mwaka mmoja nyuma kabla ya mama yake. Baada ya msiba wa Mama yake kikao kilikaa na kumteua msimamizi wa mirathi ili afatilie na kumkabidhi mtoto wa marehemu haki za mama yake.

Miezi kadhaa baada ya msiba mtoto wa marehemu baada ya kutoka chuo na kukabidhiwa card za bank za mama yake, alikagua kwenye account za mama yake ili kuona kama mama yake aliacha chochote kwenye account yake, baada ya kukagua kuangalia salio alikuta moja kati ya account aliyokuwa anatumia Mama yake ilikuwa na zaidi ya milioni 70 kwenye account ya mama yake na hakujua zile hela mama yake amezitoa wapi maana hadi mauti yana mkuta Mama hakumwambia mwanae kama alikuwa na kiasi hicho cha fedha kwenye account yake, akaanza kutumia hiyo hela bila kuwaweka wazi ndugu zake akisikilizia process za mirathi zikamilike.

Siku zimepita taratibu za kufatilia mirathi zimeendele chini ya msimamizi wa mirathi, process za kufatilia mirathi zimechukua zaidi ya mwaka kukamilika lakini mwishoni mwa mwezi wa 9 ndio msimamizi wa mirathi amekuja na mrejesho kutoka PSSF, na kumuelezea mrithi ya kuwa mafao ya marehemu tayari yameshatoka (inamaanisha ndio zile milion 70 alizokuta jkwenye account ya mama yake baaada ya msiba) na hakuna hela yoyote amabayo taasisi (PSSF) inatakuwa kutoa kama sehemu ya mirathi, pia wakuwa na taarifa kama mwanachama wao amefariki.

Wasiwasi wangu ulianzia hapa ''Inasemekana marehemu (Mama yake) kabla ya kifo chake alikuwa ameshaanza kufatilia mafao yake na yalitoka miezi kadhaa baada ya kufariki"

Naomba kupata ufafanuzi toka kwenu maana na amini hapa kuna watu wenye uelewa mpana juu ya PSSF na utaratibu wa mirathi kwa ujumla, Mtoto wa marehemu ni msichana mdogo ambaye hana uelewa mpana kuhusu mirathi na utaratibu mzima wa PSSF.

Swali langu ni utaratibu wa kikotoo ukoje kwa wastaafu, na je, kuna hela yoyote mrithi anapaswa kupewa kutoka PSSF kama sehemu ya mirthi?
Kwa uzoefu wangu,ilikuwa marehemu apewe pension ya kila mwezi mpaka anapokufa!Kwa kuwa sasa ni marehemu ,Mrithi hana chake!Labda maokoto yaliyobaki kama yapo.
 
Back
Top Bottom