Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Wakuu,
Katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa mwaka huu mkoani Singida, ujumbe uliobebwa na mabango ya wafanyakazi kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) umenisikitisha sana kama mdau wa ajira.
"Uchaguzi Mkuu 2025 utuletee Viongozi wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote tushiriki."
Kauli hii inaonekana kama ishara ya wazi ya kumuunga mkono Rais Samia kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, jambo linaloibua maswali mengi kuhusu nafasi ya vyama vya wafanyakazi kwenye mchakato wa kisiasa.
Kwa maoni yangu, ujumbe huo unaashiria mwelekeo wa kisiasa usiostahili kujitokeza katika jukwaa la Mei Mosi, siku ambayo kwa kawaida hujikita katika kushughulikia changamoto za wafanyakazi, si kutoa taswira ya kisiasa.
Je, ni kweli kwamba mwaka huu wafanyakazi hawakuwa na malalamiko yoyote ya msingi, hadi wakaamua kutumia jukwaa la Mei Mosi kumfanyia kampeni Rais Samia?
Je, bado tuna uhuru wa kuhoji na kushinikiza maboresho ya haki na maslahi yetu kama wafanyakazi bila kuingiza siasa?
Ni vyema tufikiri kwa makini kuhusu mustakabali wa vyama vya wafanyakazi na wajibu wao wa kweli katika kutetea maslahi ya wanachama wao.