Wafanyakazi: JK Hahitaji kura zetu

Status
Not open for further replies.
Alisema hivi kama hamtakikubaliana na Mimi kuwa serikali hainapesa yakuwalipa mshahara wa 315000/Kila mwezi ni bora hata hizo kura zenu za 2010 basi!!sasa sjui ndokuzikataa au :confused2:

Me sidhani hili jibu unalo litaka hapa ni kuwa mtoto wa Kindagate akujibu au maana mtoto wa std One anaweza jibu hilo na sio tungo tata,

Maana hapa mwataka kututafutia sababu ya kujaribu kulainisha lugha JK aonekane kuwa hajakosea??
 
Immunity inawa potosha sana viongozi wa Kitanzania,

Wao kwao kulopoka ni sawa ila mwananchi wa chini akijaribu ha kukosoa duuuu amefanya kosaaa kubwa saaana na wana li exaggerate kupita maelezo leo viongozi wakikosea wao ati waabudiwe na watu wawasemee ati walikosea wao ni MUNGU au Binadamu kama wengine???

Jamni Uongozi si lelemama ati ni mzigo mzito viongozi wanapaswa kulielewa hilo, na washukuru Media zetu hazijui kupayuka ingelikuwa ni nchi za wenzetu esp UK ndio JK angekoma na ingekuwa mwanzo na mwisho kulopoka tuuuu kujua kuna kinga ya urais.

Na hili liwe fundisho kwa viongozi wajao na vizazi vijavyoo. Msishangae kwa watakao kuwepo huko mbeleni wajukuu zetu watatuuliza ilikuwaje huyo kiongozi alilopoka na wakamwachiaa tuu, najua mtasema KATIBA ilikuwa bado haijarekebishwa.
 
Nafikiri anatamani ile siku irudi abidili kauli yake lakini ndio ameshasema kwa hiyo atarajie alichokisema.
 
Nafikiri anatamani ile siku irudi abidili kauli yake lakini ndio ameshasema kwa hiyo atarajie alichokisema.

There are five things that you cannot recover in life:


(1) The Stone..........after it's thrown,

(2) The Word..............after it's said,

(3) The Occasion......after it's missed,

(4) The Time............after it's gone..

(5) A person...............after they die
 
Hivi Rais hana mtu wa kuhariri hatuba zake kabla hajazimwaga hadharani?

Mkulu nami nisha wahi uliza hili jambo na directly to White Hosue yetu hapo a.k.a IKULU kuwa hotuba za huyu bwana huwa zapitiwa kwanza? na ndipo hapo nawangoje Vijana wenzangu wakina January Makamba walijitolea wasifu wao kuwa walifanya kazi IKULU na walikuwa karibu sana na Rais kila misafara sasa hawakuweza mshauri rais na wao ndio vijana wanojuana na vijana wenzao je kwa hali hiyo huju kijana nae usikute alikuwa anafuata order tuuuu kutoka kwa wakubwa basi. me nawangea huko bungeni
 
Nafikiri anatamani ile siku irudi abidili kauli yake lakini ndio ameshasema kwa hiyo atarajie alichokisema.

Kwa taharifa yako CCM haitong'olewa madarakani kwa kura halali.
Ingekuwa hivyo tungeshaona kwa Zanzibar mwaka 1995 na 2000.
So hata JK leo akisema hataki kura za wananchi wote, still bado October ataibuka mshindi tu.
 
Kweli CCM kuing'oa madarakani ni hadi pale maneno ya Nyerere yatakapotimia, kuwa upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM
Kwa taharifa yako CCM haitong'olewa madarakani kwa kura halali.
Ingekuwa hivyo tungeshaona kwa Zanzibar mwaka 1995 na 2000.
So hata JK leo akisema hataki kura za wananchi wote, still bado October ataibuka mshindi tu.
 
...........bahati nzuri kila kitu alichokisema (kwenye hotuba ileeeeee) tunacho kwenye archive zetu na SIKU ikifika tutaweka hadharani ili wale woooooooooooooooooooote wasioelewa kiswahili watafsiri watakachokielewa! God Bless Tanzania!!!
 
Kwa taharifa yako CCM haitong'olewa madarakani kwa kura halali.
Ingekuwa hivyo tungeshaona kwa Zanzibar mwaka 1995 na 2000.
So hata JK leo akisema hataki kura za wananchi wote, still bado October ataibuka mshindi tu.
Ni kweli kwamba CCM wataiba kura, lakini hofu yangu ni kwamba tunaweza kuishia kwenye kuuana kama wenzetu wakenya walivyofanya 2007, na baada ya hapo utabiri wa Sheik Yahya utatimia wa kuunda serikali ya mseto. Dalili zilizopo nchini siyo nzuri kabisa. Kwa kuwa wengi wanaonekana kuuchoka kabisa mfumo uliopo, wakati mfumo wenyewe unaonekana kutokuwa tayari kukubali halihilisi. Sasa hapo tusipoishia kwenye kuwa wakimbizi!!! Tuombe tu Mungu.

Nadhani JK anaelekea kwenye kuandika historia mbaya zaidi katika Taifa la Tanzania. Hapo tutakapoweka katika vitabu vya historia ya nchi yetu kwamba ndiye Rais aliyesababisha vita nchini. Hapo ndipo yatakapotimia yaliyosemwa na Abiud Misholi. cheki video hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Jakaya Jikaange kwa mafuta yako mwenyewe sasa.
...........bahati nzuri kila kitu alichokisema (kwenye hotuba ileeeeee) tunacho kwenye archive zetu na SIKU ikifika tutaweka hadharani ili wale woooooooooooooooooooote wasioelewa kiswahili watafsiri watakachokielewa! God Bless Tanzania!!!
 
Mgombea wa CCM rais Jakaya Kikwete akiendelea na kampeni zake jijini Mwanza amesema,

"Nilieleza kuwa kama sharti ni kuweka kima hicho cha chini, basi kura hizo tumezikosa. Hatutaweza kulipa kiwango hicho. Leo mbaya mie, wazuri wao, kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.

Kura hata moja kwangu ni muhimu, siwezi kuikataa, lakini kama sharti ni hilo, kura hizo tumezikosa. Watatupa wengine.

"Hata hivyo, naamini katika wafanyakazi wapo wanachama wazuri wa CCM, wapenzi wa CCM, wanaojua chuya au pumba na mchele. Hivyo, tunaamini na sisi CCM tutapata kura za kutosha, kuongoza nchi hii." alisema.
 
Mbona siku ile ya Mei 3 aliongea kwa jazba kuwa hazihitaji kura za wafanyakazi
 
Jioni hii serikali imeuandikia rasmi uongozi wa YANGA Afrika uamuzi wa kuipatia timu hiyo uwanja mpya wa Taifa kama uwanja wao wa nyumbani...hatua hiyo inakuja baada ya SIMBA ambayo nayo iliwasilisha ombi lake kutupwa....hata baada ya wasimamizi wa uwanja wa TAIFA kusema kuwa uwanja unaweza kutumika mara mbili kwa wiki ...hatua ambayo ingewezesha timu zote mbili...kuweza kutumia uwanja huo kama uwanja wake wa nyumbani....Yanga ni moja ya timu zenye washabiki wengi ...sana akiwamo rais kikwete ...na ingeweza kucheza sehemu yeyote Tanzania kama ilivyo kwa simba....

KITENDO CHA SERIKALI KUIPENDELEA YANGA KINAWEZA KUTAFSIRIWA KWA MAANA...NYINGI KAMA MUENDELEZO TU WA YALE AMBAYO YAMEKUWA YAKIONGELEWA ....KWA WATU WALIO KARIBU NA RAIS KUTUMIA MAMLAKA NA RASILIMALI ZA NCHI VIBAYA...
 
this is what I am talking about
JF ibarikiwe na idumu milele kwa kufunua unafiki wa Kikwete na mafisadi wenzake.
 
Bahati mbaya ni kwamba hizi picha haziwezi kurushwa tena ili walau watu wakumbuke na kuwa mbayu wayu wa kweli.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom