figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,493
- 54,900
Salaam Wakuu
Teknolojia ya bandarini haitamuacha mtu salama. Inabidi watu wakarudi kusoma pale chuo cha bandari Temeke ambacho kinaenda kuwekewa vifaa vya kisasa vya kufundishia.
Hivi karibuni Kampuni ya AD Ports Group ilisaini mkataba na kampuni ya Adani na SEZ Ltd kwa ajili ya uwekezaji wa pamoja wa kimkakati unaohusisha reli, huduma za baharini, uendeshaji wa bandari, huduma za kidijitali, eneo la ukanda wa viwanda na uanzishaji wa vyuo vya elimu ya baharini hapa nchini.
Yaani sasa Bandari za Tanzania kuwa za kisasa na za mfano Afrika. Mitambo tu ndo inayofanya kazi.
Rais Samia(Mwanamke Shupavu) alienda kutafuta wawekezaji huko United Arab Emirates (UAE) na wameonesha nia kuwekeza.
Sasa utakuwa ukienda Bandari hukutani na mtu, Mitambo tu ndo itakuwa inapishana. Wewe unasubiri getini mzigo wako unaletwa na gari lisilo na dereva.
Sasa zile nyodo za bandarini kuisha.
Zamu anaingia mdada mdogo tu na remote control.
Tayari Bandari ya Dar ishaanza kupanuliwa na kuondoa mchanga ili Meli kubwa ziingie.
Kwa wale Matomaso ambao hawaelewi hadi picha, angalieni hapa chini kazi zitavyo fanyika