Kuna shida kubwa Bandarini, Serikali ipo kimya!

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
Je Hii ndio DW Word imeanza kazi? au bado bandari wanasuasua?

Kuna wakati ilitoka habari humu kuwa meli zinakaa muda mrefu bila kushusha mizigo mpaka ikafikia hatua meli zinahama bandari lakini Mamlaka ya Bandari wakakanusha pengine ni ukweli ambao ulifichwa.

Hii dhambi ya kukanusha taarifa ambazo zinatoa tahadhari kwenye uchumi wa nchi italiangamiza Taifa letu.

Nchi inapata hasara kubwa sana na wafanyabiashara wanapata hasara kubwa sana kwa meli kuchelewa kushusha mizigo lakini pia mizigo kuchukua muda mrefu kufanyiwa clearance. Mwaka jana mwishoni zilianza kelele za wateja kuwalaumu mawakala wa kusafirisha mizigo kwamba wanachelewesha mizigo yao. Mawakala hawakuwa wazi ila waliendelea kutoa majibu ya wateja kusubiri na pengine walikuwa wanaogopa kusema ukweli. Hali ilikwenda mpaka ikafika hatua na wao wakaanza kuomba msaada kwa serikali iingilie kati ucheleweshwaji wa mizigo. Walifikia hatua ya kupost in public kuwa mizigo inakaa muda mrefu haijatoka na meli pia zinakaa muda mrefu hazijashusha mizigo.


Nitatoa mfano.
Kipindi cha mwanzo, meli ilikuwa ikiondoka China tarehe 1 January 2024 basi tarehe 1 February 2024 mizigo inakuwa imefika Tanzania na imetoka na mfanyabiashara ana mizigo yake. Kwa sasa Mizigo ikitoka China tarehe 1 January 2024 itafika tarehe 1 February meli imefika DSM lakini haijashusha, itafika tar 1 March 2024 bado mizigo haijatoka. Mizigo ambayo ilikuwa ikichukua siku 30 kufika inachukua zaidi ya siku 60 kwa sasa. Hii ni hasara kwa wafanyabiashara na Hasara kwa serikali.

Ukiingia link hii ya Marine Traffic utakuta kuna meli zina wiki 2 zinasubiri kwenda kushusha Mizigo.
Screen.png

Kila kidoti cha kijani ni meli, ukibonyeza kidot inaleta taarifa za meli na ipo hapo tangu lini bado haijashusha.
https://www.marinetraffic.com/en/ais/home/centerx:39.435/centery:-6.798/zoom:12

Ukifuatilia vizuri utaona pia kuwa Meli za magari ndio zinashusha kwa haraka na kuondoka na kwa akili ya kawaida ni kwa sababu Meli hizo hazitegemei mitambo kushusha magari, magari yanashuka yakiendeshwa au kuvutwa na magari mengine.

Hii inamaanisha kuwa mitambo ya kushusha makontena haikidhi uhitaji wa bandari yetu.
Hii ni Taa nyekundu kwa Serikali. TRA watuambie makusanyo ya kodi kwa upande wa bandari kama hayajashuka.
Kuna Taa nyekundu imewaka ila watu wanaiziba na mandoo ya kijani isionekane. Serikali ifanye kila iwezalo kuinusuru Bandari.

Wasipoinusuru, Hasira ya Mungu iko Karibu.

Narudia Hasira ya Mungu iko karibu kwa ajili ya kuokoa maslahi ya Watanzania.
 
Shida bongo tunaingiza siasa hata kwenye vitu visivyohitaji siasa hata kidogo.
Kuna magazeti ya leo ukiyasoma yanavopingana na ukweli unaoendelea pale bandarini utastaajabu na kujiuliza maswali mengi sana yasiyo na majibu.
Bandarini tutaona vimbwenga vingi sanaa, ule mkataba wa kuforce lazma utaleta mengi!
 
Hapo kwenye hasira ya Mungu!!

Kwanini Kila uchwao mnampangia safari za nje , ofisini atahimiza vp team yake?
 
Mkurugenzi wa bandari Yuko wapi kujibu haya maswali, waandishi wa habari wafanye kazi yao kupata majibu ya vitu muhimu sio kutuletea kina Lokole na Mwijaku Kila siku
 
Mzigo wangu Nimepokea leo, meli ikifika bongo trh 10 Feb ineshusha trh 3 march. China to bongo
 
Back
Top Bottom