DOKEZO TAKUKURU ni kweli hamjui wanachofanya maafisa TRA bandarini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Aug 10, 2023
9
16
Note. Huu ni uhalisia wa kinachoendelea bandarini na sio habari za kuchafuana.

Mimi kama mmoja wa wadau wa kubwa wa sekta ya bandari nachukizwa sana na matendo yanayofanywa na maafisa wa TRA bandarini(TPA) na bandari kavu(ICDs). Wenzetu wa TRA wametugeuza customs agent kama mitaji wameset sheria zao binafsi ambazo kwa tafsiri ya kawaida ni uhalalishaji wa rushwa.

Kuna utaratibu wao ambao upo hivi ili uweze kuandikiwa remarks na kuwa released lazima utoe shilling elfu kumi za kitanzania kwa maana afisa anayeandika remarks 5000 na anaye release 5000 huu ni utaratibu unaofanyika kwa muda mrefu sana muulize custom agent yoyote atakwambia ni kawaida. Je Mkurugenzi wa mamlaka ya mapato anajua kuhusu huu utaratibu? Na kama anajua basi ni vizuri uwekwe wazi ili wateja wajue maana kuna baadhi ya wateja ukimwambia kuhusu hili wanakuona ni tapeli..

Sasa hiyo elfu kumi ni lazima utoe bila ya kujali mzigo wako upo sawa au unachangamoto yoyote.

Incase ikatokea mzigo wako unachangamoto huo ndio mwanya kwao maana hakuna rangi utaacha kuona wanaomba kiwango kikubwa cha pesa ili waweze kuachia mzigo wako inaleta wakati mgumu kwa wateja wenye uwezo mdogo at the same time inakuwa fursa kwa wale wenye uwezo mkubwa kuingiza bidhaa ambazo ni prohibited nchini.

Sisi raia wa kawaida tunaamini maslahi ya wafanyakazi wa TRA ni makubwa katika level ambayo hawapaswi kuwa na tamaa na hela za watu ambao ndiyo walipa kodi wanaojenga uchumi wa nchi.

Tunaomba TAKUKURU kama mnavyowachukulia hatua watu wa sekta nyingine basi wachukulieni hatua maafisa wazembe na walafi pale bandarini.

Binafsi kuanzia sasa nakusanya ushahidi wewe Afisa wa TRA kuwa makini unapo pokea hela kwani utakuja kupokea hela ya dobimaridadi ikutokee puani kwani nina uwezo wa kuwataja majina yote matatu kituo chako cha kazi na ushahidi wa rushwa uliyopokea.
 
Back
Top Bottom