Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
UPEPO wa kisiasa si shwari kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa Igunga baada ya wafanyabiashara mashuhuri walioombwa na chama hicho kuchangia sh milioni 300 kugoma kutoa fedha hizo. Habari za uhakika kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara hao waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina, zinasema wafanyabiashara hao wamegoma kwa sababu wamegundua CCM kinafuja pesa kwa anasa badala ya kampeni.
Mmoja wa hao waliogoma, ambaye yuko ndani ya timu ya kampeni, amesema kikao cha CCM kuchangisha wafanyabiashara hao kilifanyika katika Hoteli ya Peak, Septemba 10, na kilihudhuriwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, na viongozi wengine wa CCM. Kila mfanyabiashara alikubali kuchanga sh milioni 5. Hata hivyo, habari zimesema kuwa sasa wafanyabiashara hao wamegoma kutimiza ahadi zao na wengine waliokuwa wametoa kiasi cha fedha wamechukua fedha hizo.
Mmoja wa wafanyabiashara hao aliliambia Tanzania Daima kuwa uamuzi wa wafanyabiashara hao umekuja baada ya kutoridhishwa na matumizi mabaya ya chama hicho, hasa baada ya mmoja wa viongozi wa kampeni za CCM kukabiliwa na tuhuma za ngono. Ni kweli tulikutana na Mkapa na Mukama hapo hotelini, tarehe 10, kuanzia saa tatu asubuhi na tulikubali kuchangia. Lakini tumeamua kutoendelea na zoezi hili kwa sababu hatuwezi kutoa fedha zetu ambazo zinatumika hovyo, alisema.
Imedaiwa kwamba baada ya kudhihirika kwa tukio la fumanizi linalomhusisha kiongozi huyo na tuhuma kwamba baadhi ya viongozi wanagawa fedha kwa wananchi, wafanyabiashara hao waliamua kusitisha michango yao. Wengine waliamua kudai fedha zao kutoka kwa mtu waliyekuwa wakimkabidhi. Habari zinasema fumanizi hilo lililomkumba kigogo huyo, limekigharimu chama chao kiasi cha sh milioni 14 ili kumnyamazisha mume wa mwanamke huyo aliyefumaniwa.