Wafanyabiashara wagoma kuchangia CCM Kampeni Igunga

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
UPEPO wa kisiasa si shwari kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa Igunga baada ya wafanyabiashara mashuhuri walioombwa na chama hicho kuchangia sh milioni 300 kugoma kutoa fedha hizo. Habari za uhakika kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara hao waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina, zinasema wafanyabiashara hao wamegoma kwa sababu wamegundua CCM kinafuja pesa kwa anasa badala ya kampeni.

Mmoja wa hao waliogoma, ambaye yuko ndani ya timu ya kampeni, amesema kikao cha CCM kuchangisha wafanyabiashara hao kilifanyika katika Hoteli ya Peak, Septemba 10, na kilihudhuriwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, na viongozi wengine wa CCM. Kila mfanyabiashara alikubali kuchanga sh milioni 5. Hata hivyo, habari zimesema kuwa sasa wafanyabiashara hao wamegoma kutimiza ahadi zao na wengine waliokuwa wametoa kiasi cha fedha wamechukua fedha hizo.

Mmoja wa wafanyabiashara hao aliliambia Tanzania Daima kuwa uamuzi wa wafanyabiashara hao umekuja baada ya kutoridhishwa na matumizi mabaya ya chama hicho, hasa baada ya mmoja wa viongozi wa kampeni za CCM kukabiliwa na tuhuma za ngono. “Ni kweli tulikutana na Mkapa na Mukama hapo hotelini, tarehe 10, kuanzia saa tatu asubuhi na tulikubali kuchangia. Lakini tumeamua kutoendelea na zoezi hili kwa sababu hatuwezi kutoa fedha zetu ambazo zinatumika hovyo,” alisema.

Imedaiwa kwamba baada ya kudhihirika kwa tukio la fumanizi linalomhusisha kiongozi huyo na tuhuma kwamba baadhi ya viongozi wanagawa fedha kwa wananchi, wafanyabiashara hao waliamua kusitisha michango yao. Wengine waliamua kudai fedha zao kutoka kwa mtu waliyekuwa wakimkabidhi. Habari zinasema fumanizi hilo lililomkumba kigogo huyo, limekigharimu chama chao kiasi cha sh milioni 14 ili kumnyamazisha mume wa mwanamke huyo aliyefumaniwa.
 
Nafikiri wameanza kuona mbali kuwa the fall of magamba is inevitable na wanaanza kuweka Mazingira ya mbeleni sawa!
 
Mfanyabiashara kinyonga, anaangalia upepo unavyovuma na namna ya kuendana na nguvu ya upepo vinginevyo watabaki wenzangu mimi wanaosimamia kwenye mgongo wa Vasco da Gama na mambo yakiwaendea kombo ndo wasalaam.
 
Watahenya sana...zile zama zakuichangia ccm kwasababu ya nidhamu ya woga wakufilisiwa zimepitwa na wakati Magamba lazima walitambue hili.
 
hahaa wanachanga hela za kupikia mapilau na akina mwigulu kulipia gesti wakiwa wanazini na wake za watu
 
Wafanyabiashara waendelee kususia michango isiyo na tija kwa maendeleo ya watanzania.

Mtu anafanya ufuska halafu anatumia pesa kumhonga mume wa mke aliyefanyiwa ufuska ili kumfichia siri
 
wafanyabiashara lazima waamke sisimu ina ng'oka sasa wang'ang'anie kama kupekitawafia...
 
Wengi wao wafanyabiashara magumashi, wanatest kama wenye ndoa. Hawana guts za kugoma kutoa. Wengi hawajiamini wakitishwa kidogo tu watatoa hao.
 
Wamechoshwa kuwa godoro la nyumba ya wageni,Chama kimekuwepo toka 1977,ni umri wa mtu mzima,hakina miradi endelevu,ambayo hata kikikwama namna ya kujikwamua ni ngumu.Kikitokea chama kingine kikachukua hatamu za nchi,tutashuhudia kifo cha chama tawala,mawazo ya viongozi walio wengi ndani ya chama ni kujaza matumbo yao,siasa bora ni kuanza na watu wako,kuwasikiliza na kutatua matatizo ya msingi yanayowakabili km maji,shule,afya na ustawi husika.Ila tutafika,maana hakuna mafanikio rahisi,ila bila CCM,tunaweza na zaidi ya hapo.
 
Jamani CDM tuitishe changizo, ila sisi tusibague, uwe mlala hoi, uwe nazo, I think we can
 
Kuna majibu mawili na yote ni sahihi kwa hili:
  1. Wafanyabiashara ni wajanja, kuna kitu kinaitwa "Cost benefit analysis" wameshapiga mahesabu hata wakitoa hizo hela Magamba hawatashinda, sasa kwa nini wapoteze hela zao.
  2. Hilo wazo kuwa wameona hela zao zinafujwa na vigogo kwa kufanyia anasa kama uzinzi etc. Lakini naona hii haina mashiko kwani CCM ikishinda wanaweza kupata msukosuko kwenye biashara yao.
 
Inasemekana baadhi wana CCM wamekelwa sana na Tabia za ufuska wa viongozi wao na wameapa kutokukipigia kura chama hicho.
 
Pia kuchangia hela kwa ajili ya jimbo la igunga ili ccm ishindi ni sawa na kumsaliti RA ambaye ni mfanyabiashara mwenzake ambaye alijiuzuru sio kwakupenda.
Unajua wafanyabiashara wanachama chao nadhani baada ya kikao na ccm walikaa cha kwao nakuona hawawezi kumsaliti mfanya biashara mwenzao
 
Back
Top Bottom