MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,223
- 22,301
Kwa wiki iliyopita mitandaoni hasa Instagram na Twitter kuliibuka mjadala mkali ikiwemo vita ya maneno miongoni mwa wafanyabiashara wa mjini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyabiashara walimtupia lawama Bi Niffer ambaye ni mfanyabiashara mdogo anayekuwa kwa kasi ya ajabu. Wanamtuhumu Niffer kurukia kila biashara huku akivunja miiko mingi ya biashara hizo. Wanadai Niffer amekuwa akiharibu bei za soko kwa makusudi huku akiponda bidhaa za wafanyabiashara wengine.
Hili suala limekuwa na mitazamo mingi. Watu wengi wamesema Niffer yuko sahihi kwa sababu ni mbunifu na hakuna sheria anayovunja. Upande mwingine unadai sio vema Niffer kuanika bei zake ndogo hadharani kwa sababu zinawaharibia wenye maduka ambao wanalipa kodi nyingi sana. Binafsi baada ya kufuatilia hili sakata nimeona ni sahihi 100% Niffer kuendelea kuwapelekea moto hao wakongwe wasiotaka kubadilika. Pia yeye kuuza vitu kwa bei ya chini ni msaada kwa wananchi wengi. Niffer ni mjasiriamali kamili anayetatua changamoto za raia huku raia wakiweka pesa kwenye wallet ya Niffer.
Ukitoa wauza nguo kwa bei ya jumla hao wafanyabiashara wengine ni wapigaji kwa kuweka bei za juu kupitiliza. Nina ushahidi usiotia shaka. Kwa mfano raba za AirForce zinazouzwa 35 - 50k... ila kuziagiza hadi kukufikia haizidi 15k kila kitu. Sasa kuna sababu zipi za kuuza kwa bei mara 2 au 3? Wanyabiashara wakongwe jueni kabisa kutatokea kina "Niffer" wengi sana na sokoni kutachafuka mno. Mjiandae kisaikolojia.
Ninamshauri Niffer naye asifanye kosa la kuponda bidhaa za wenzake. Apromoti tu bidhaa zake bila kutamka shombo kuhusu wengine. Wafanyabiashara wakongwe wana mbinu nyingi safi na chafu kwahiyo awe makini asije akazimishwa. Ni HATARI. Pia yule boyfriend wa Niffer awekeze zaidi kwenye kukata viuno kitandani maana kwa hali ilivyo Niffer anaenda kuwa mkubwa zaidi na kuna mabaradhuli wenye hela hawawezi kuona mtoto mkali kama yule wakaacha apite hivihivi.