Wafahamu nyoka hatari Zaidi duniani

Wafahamu nyoka hatari Zaidi duniani

Mimi binafsi mwaka 1994 nilikuwa naelekea Bujiumbura nilipofika katikati ya Bwanga na Runazi (wakati huo naendesha lori la mizigo)nikaona kitu kimekaa barabarani, kwa mbali mimi nikafikiria ni ni fito ndeefu imetupwa barabarani,kumbe koboko bhana,kumkaribia akasimama huku amepanua mdomo wake mweusii toba.nikafunga vioo vyote nikajua nimemkanyaga kufika Runazi mwenzangu aliyekuwa nyuma alipofika nikamuuliza kama ameona mzoga wa koboko akasema hajaona chochote.
 
Siongelei duniani, siongelei tafiti maslahi, naongelea ukweli na uhalisia wa Koboko mkubwa kama huyo alieonyeshwa na mdau katika picha. ni uhalisia wa kua nimekaa katika maeneo husika yaliyosheheni nyoka huyo. Unapokua porini ukakutana nae mara nyingi yeye ndio anakua amesogea kutoka huko alipo. Akiona ni binadamu na kama kama kuna kaumbali kiasi ata back off na kuondoka. Lakini mkikutana katika distance fupi uso kwa uso na uanze kukimbia Black mamba hasa wa ukubwa huo niliousema anakukimbiza kwa speed na hauta fikisha hata mita tano atakugonga several time na atakimbia. Anafanya hivo kw amifugo na anafanya hivo kwa binadamu, consult your books again pal
Nilitamani kumjibu huyo jamaa nikafikiria vinginevyo nikaghairi... almost wote tumezungumzia upole wake na pale anapohisi hatari ambush yake sio ya kawaida...
 
View attachment 724186
Koboko aliyekomaa kama huyu hana mpinzani huwa analaza kundi la ng'ombe,sasa wataalam wanakuambia eti huwa akikuona anakimbia...wataalam wengi walishakufa sasa wanataka na sisi raia wema tuwafuate huko waliko.
Ni hulka ya nyoka kadri anavokuwa mkubwa ndivyo anavyojiamini na mkorofi zaidi...
 
Ni hulka ya nyoka kadri anavokuwa mkubwa ndivyo anavyojiamini na mkorofi zaidi...
Nyoka hatari kabisa duniani ni koboko aliyekomaa, maana wakati anashambulia hushambulia kwa kasi ya ajabu, halafu huwa anang'ata juu kuanzia kifuani kwenda kichwani ambayo ni sehemu iliyo karibu na moyo,na hung'ata zaidi ya mara tano hadi kumi kwa speed ya ajabu.
 
King cobra ameitwa king sababu hio anawala cobra wenzie na nyoka wengine wenye sumu halafu king anakuwa na ukubwa kuliko nyoka wengine wote ..,puffadder na nyoka wengineo wapo kwenye diet ya king cobra

Koboko na king wapo mazingira tofauti hivyo hawawezi kukutana lakini youtube kuna video kadhaa ikionyesha king akimla koboko mkubwa wakiwa kwenye farm.
Hapa tuko pamoja...
 
c99f20438154022637e4e93de689e25a--serpenti-black-mamba.jpg

Kitu kinawika hicho.
 
Huyu ni nyoka mwenye hadithi nyingi sana na anaegopwa kuliko wote kwa sababu tofauti na nyoka wengine ambao hujihami, Black Mamba hua anashambulia. kwa Tanzania nyoka hawa wapo sana katika mapori ya Tabora na Mwanza na jina lake la asili ni Koboko. Siku zote nasema nyoka huyu angekua anapatika ulaya wazungu wangempa promo sana ila sisi waswahili tunawaua sana kiasi ambacho sasa hivi ni nadra kumpata Black Mamba mwenye ukubwa wa chatu mkubwa
"Black Mamba mwenye ukubwa wa chatu"???..... Hebu fananua plz
 
Back
Top Bottom