Wafahamu nyoka hatari Zaidi duniani

Wafahamu nyoka hatari Zaidi duniani

Ugomvi wa nyoka anayepoteza timing ndiye anakuwa msosi..
King cobra michezo hii anaiweza sana japo si wa kudhaminika kirahisi kwa Koboko...

King cobra anaubavu wa kumla koboko aliyekomaa labda awe mtoto wa koboko black mamba ni ambari nyingine
 
Watu wengine mumekaririsha aina fulani ya upuuzi,koboko akisha kasirika anakufata na kukushambulia kwa kukunng'ata zaidi ya mara moja.
Hakuna koboko huyo duniani


Ni simba ,chui,nyati,kiboko wanaokimbiza watu na wanyama wengine kama faru

Koboko akikuona unamfuata anaondoka zake hata ukimkaribita mita 4 atajirudi nyuma akijitayarisha kukugonga na hapo hapo anatafuta njia ya kusepa ,na atafanya juu chini aku avoid utamuona anakimbia ukimfuata kushoto anaenda kulia ila akiwa stand by

Koboko akikasirika anakukimbiza narudia tena hakuna koboko huyo ,koboko uliyemuona ndio mzuri kuliko koboko usiyemuona
 
Niliwahi kuskia nyoka wakigombana na mmoja kuuwawa! Mwenzie anakwenda kuchuma dawa na kumuekea mwenzie..kama binadamu utafanikiwa kuiona dawa basi ni dawa nzuri mno kwa mtu alie umwa na nyoka ..ila nyoka akikuona akiwa anachuma umekwisha..
Stori za abunuwasi
 
Hakuna nyoka anayekimbiza watu huyo nyoka hayupo duniani labda kwa baadae nyoka wa aina hio atokee .

Mamba kama walivyo nyoka wengine hawapendi usumbufu wakiona unafanya approach kuwasogelea hujiondokea zao

Nyoka mbaya na hatari ni yule hujamuona ukapita jirani yake hapo atafanya striking kama defensive mechanism ila kuhusu kukimbiza hayupo nyoka wa aina hio duniani.
Siongelei duniani, siongelei tafiti maslahi, naongelea ukweli na uhalisia wa Koboko mkubwa kama huyo alieonyeshwa na mdau katika picha. ni uhalisia wa kua nimekaa katika maeneo husika yaliyosheheni nyoka huyo. Unapokua porini ukakutana nae mara nyingi yeye ndio anakua amesogea kutoka huko alipo. Akiona ni binadamu na kama kama kuna kaumbali kiasi ata back off na kuondoka. Lakini mkikutana katika distance fupi uso kwa uso na uanze kukimbia Black mamba hasa wa ukubwa huo niliousema anakukimbiza kwa speed na hauta fikisha hata mita tano atakugonga several time na atakimbia. Anafanya hivo kw amifugo na anafanya hivo kwa binadamu, consult your books again pal
 
Black-mamba-on-the-ground.jpg

Koboko aliyekomaa kama huyu hana mpinzani huwa analaza kundi la ng'ombe,sasa wataalam wanakuambia eti huwa akikuona anakimbia...wataalam wengi walishakufa sasa wanataka na sisi raia wema tuwafuate huko waliko.
 
Taipan na desert viper ni hatari.pia king cobra wa kuogopwa!jana nilikuwa naangalia documentary ya anaconda nilishangaa sana wale nyoka wanafanya mapenzi kwa wiki nne bila kuachiana.wamenatana tu huku dudu zao zipo ndani.ni shida
Duuh wiki nne,!! wakitoka hapo kukutana tena baada ya muda gani!?
 
King cobra anaubavu wa kumla koboko aliyekomaa labda awe mtoto wa koboko black mamba ni ambari nyingine
King cobra ameitwa king sababu hio anawala cobra wenzie na nyoka wengine wenye sumu halafu king anakuwa na ukubwa kuliko nyoka wengine wote ..,puffadder na nyoka wengineo wapo kwenye diet ya king cobra

Koboko na king wapo mazingira tofauti hivyo hawawezi kukutana lakini youtube kuna video kadhaa ikionyesha king akimla koboko mkubwa wakiwa kwenye farm.
 
Kuna kile kipindi cha Snakes In the City,yule mchizi na mke wake wanayakamata haya madude vibaya mno halaf wanawardish msituni. Wanakamataga had Black Mamba hawa aisee mpka mtazamaj unaogop jins wanavywakamata
 
Huyu ni nyoka mwenye hadithi nyingi sana na anaegopwa kuliko wote kwa sababu tofauti na nyoka wengine ambao hujihami, Black Mamba hua anashambulia. kwa Tanzania nyoka hawa wapo sana katika mapori ya Tabora na Mwanza na jina lake la asili ni Koboko. Siku zote nasema nyoka huyu angekua anapatika ulaya wazungu wangempa promo sana ila sisi waswahili tunawaua sana kiasi ambacho sasa hivi ni nadra kumpata Black Mamba mwenye ukubwa wa chatu mkubwa
Kumbe anaitwa ngoboko?
 
1. TAIPAN WA ARDHINI:

Nyoka huyu ni wa kwanza kuwa na sumu kali duniani, anaeishi ardhini tu. aking'ata kitu chochote hutoa sumu kiasa cha milligram110 iliyo na uwezo wa kuua binadamu 100 au panya 250,000.

2. NYOKA WA BRAUNI KUTOKA MASHARIKI:

Nyoka huyu anayepatikana kwa wingi Australia anashikilia nafasi ya pili kwakuwa na sumu kali sana ambayo 1/14,000 ya tone la sumu humuua mtu mzima kwa muda mfupi, anasifika pia kwa kuwa na spidi sana ya kukimbia.

3. KRAIT WA BLUU

Nyoka huyu anayepatikana Kusini mashariki mwa bara la Asia na indonesia anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na sumu kali, 50% ya kung'ata kwake husababisha kifo au kuparalyse na ni vigumu kupona hata kwa matumuizi ya dawa ya kumaliza makali sumu ya nyoka(Antivenin).
Nyoka huyu pia ana sifa ya kuwashambulia na kuwauwa nyoka wenzake hata wa jamii yake

4. TAIPAN

Nyoka huyu anaeshikilia nafasi ya nne anaptaikana nchini Australia, ana sumu kali iliyo na uwezo wa kuua nguruwe wa guinea 12,000, pia katika ung'ataji wake husababisha kifo ndani ya lisaa limoja.

5. BLACK MAMBA

Nyoka huyu anayepatikana sehemu nyingi ya Africa anashika nafasi ya tano huku akiwa anaogopeka sana kwa ukali wa sumu yake na ushambuliaji wake.
Ana uwezo wa kushambulia kwa kurusha sumu hadi mara 12 kwa wakati mmmoja ambayo huweza kuuwa binadamu 10 hadi 25 kwa wakati mmoja. Ung'ataji wake mmoja hutoa sumu kiasi cha milligram 100 hadi 120.
Huwa anasifika sana duniani kwa kuwa nyoka wa kwanza mwenye mbio ardhini akiwa na uwezo wa kukimbia kilometa 20 kwa lisaa limoja.
Nyoka huyu anapatikana pia Tanzania hivyo si vibaya tukimjua zaidi ili ukisikia yupo sehemu utafute namna ya kujihami nae...
MAMBAS ni aina ya nyoka wakali wapatikanao ktk dunia ya leo. Ni nyoka wenye sumu kali na wenye kasi ktk mwendo na wana sifa ya kutaga mayai (oviparous).
Kuna aina mbili za mambas :
1. GREEN MAMBAS.
2. BLACK MAMBAS.
Green mamba wanasumu aina ya NEUROTOXIC na HAEMOTOXIC. Wanaishi miaka 12 hadi 14 (makadirio kulingana na takwimu za sayansi) wanataga mayai na kuanguliwa kwa siku 80 hadi 90.
BLACK MAMBA pia wanauwezo wa kupanda miti wakati wakitafuta chalula na wanaurefu kati ya sentimita 220 hadi 320. Ni kati ya nyoka wenye sumu kali wapatikanao Afrika. Wanataga mayai kati ya 12 na 18,na kuangua kati ya siku 80 hadi tisini.
Mambas ni nyoka wakali na wenye kung'ata zaidi ya mara moja kwa sababu meno yao hayang'oki wakati wakigonga kitu. Meno yanayong'oka kwa nyoka yanaitwa FRONT FANGED MOVABLE na yasiyong'ooka yanaitwa FRONT FANGED FIXED.
Iwapo nyoka hawa wata kung'ata utaweza kuishi kati ya dakika 20 (kwa mujibu wa utafiti) Na kupoteza maisha...
Huyo mdudu namba tano hafai kabisa.. Alishasababishaga kilombero, morogoro.
 
King cobra ameitwa king sababu hio anawala cobra wenzie na nyoka wengine wenye sumu halafu king anakuwa na ukubwa kuliko nyoka wengine wote ..,puffadder na nyoka wengineo wapo kwenye diet ya king cobra

Koboko na king wapo mazingira tofauti hivyo hawawezi kukutana lakini youtube kuna video kadhaa ikionyesha king akimla koboko mkubwa wakiwa kwenye farm.
**** rattle snake nae balaa ukute yule ana pembe kubwa km za mbuzi
 
4858774.jpg

Koboko wadogo wakipambana,hawa wakikomaa hakuna mnyama wa kuwasogelea na wanauwezo wa kusimamia mikia.
 
Back
Top Bottom