Nilikoswakoswa na huyo koboko, nilitaka kuumua kwa fimbo niliposhusha fimbo nikamkosa kanirukia kaanza kupanda kwenye fimbo kwa kasi, nikaiachia fimbo akawawa anakuja kunigonga nikaruka pembeni,nashukuru jamaa yangu alikua na fyekeo kamkata ndo salimika yangu .siku nyingine king cobra alikuwa amelala anaotea jua la asubuhi,kunamama mmoja alikuwa anakatiza maeneo hayo maana yalikuwa ni Maeneo ya mashamba, mala kamuona king cobra kalala.ikabidi atuite kwani tulikuwa karibu.kwa vile ni wanaume tukaenda tulikuwa wawili ,pia alikuwepo mzee mmoja alikuwa analima eneo hilohilo akaja naye, ko tukawa watatu. Yule mzee alikuwa mganga wa kienyeji, ko nyoka kama hao ni lulu kwake.kufika pale tukamuona king cobra kalala mkubwa balaa. Jamaa yangu kachukua jembe amlime kwa nguvu akiwa amelala, jamaa kamlima kwa nguvu, kwa bahati mbaya kamkosa, akaamka kwa hasira ikabidi tuanze kuchanja mbuga. Kwa bahati nzuri kulikuwa na shimo la kichuguu pembeni kaingia humo.yule mzee akatuomba tumsaidie kuua yule nyoka. Mimi nilisita sana lkn jamaa yangu kanisihi tuende. Tukafika kwenye lile shimo ,tukaziba matundu mengine ili asije kutoka jupitia matundu hayo. Tuchungulia kwa mbali tukamuona, ikabidi mzee aingize fyekeo mule ndani. Kaanza kumkata yule nyoka ,nyoka alitoka mle ndani kwa hasira tukatoka nduki, yule mzee alikuwa anasumbuliwa na mguu ko badala ya kukimbia angaanguka palepale, kwa bahati nzuri yule mzee alikuwa mganga ikabidi autumie uganga wake vizuri kwa kumtemea mate yule nyoka ko akashindwa kumdhuru. Ikabidi aingie tena kwenye shimo .yule mzee hakukoma akaamka na Kuingiza fyekeo kuanza kumkata yule nyoka. Kamkataa wee katuita njoo tusaidiane kumtoa ameshakufa, tukafika pale tukaanza kumvuta, kumbe hajafa walanini, akatoa kichwa ili atufanye kazi, lkn alikuwa amebanwa .nyoka bwana wana akili Sana. Pale ikabidi aturushie mate mengi. Mimi yakanipata kifuani, jamaa yakampata usoni yule mzee akamdhibiti kwa kumkata shingo. Pale ndo ikawa furaha ya yule Mzee. Tukapewa dawa ya ile sumu kwani hatukuwa mbali na nyumbani kwake, .king cobra na black mamba sio wa kuwachezea kabisa.