Mkuu mleta hii thread kwakweli umenikumbusha mbaaali sana. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimevaa IRIZI shingoni pale Tabora wilaya moja inaitwa SIKONGE. Hakika sitosahau huyu nyoka anayeitwa KOBOKO(MAMBERS). Nilifika pale kufanya tafiti maalum hivyo ilinilzimu kufika hadi maeneo yasiyofikika kirahisi. Baada ya kuripoti kwa m/kiti wa kijiji nikapokelewa vizur tuu ila nilipomwambia sehemu ninazohitaj kufika alishtuka na kushika kichwa baadae akanambia ngoja nimuite mtaalamu mmoja aje ili twende nae. Kwa bahat mbaya sana hilo pori hatari linaloogopwa ndipo kuna hawa wadudu na hakuna njia ya gari hvyo ni lazma kupita kwa mguu. Basi mtaalamu tuliekuwa tunamsubiria akafika akiwa na kabegi kadogo cha ngozi ubavuni kwake. Heee,si alivyokafunua hivi akatoa nyeusi NNE(4)!!!? Akasema kila mmoja avae thn twende tuanze kazi,yan mimi 1,dereva wangu 1 na wenyewe moja moja. Mimi nikagoma nikasema tapita hivyohvyo huko porini mana hvyo vitu siviamini. Na dereva alivyojua kuwa kule gari halipiti akasema yeye hatoenda porini maana inabd alinde gar akat sisi tunaingia porini.Asee,NLIKUWA NIKITEMBEA KAMA HATUA 15 HADI 20 haijulikani wanatokea wapi wale wadudu(tuliambiwa tusiwaite koboko tuseme mdudu) unamuonea hapa tit4tat. Ile hali ilitokea mara nne maana mbele alitangulia mganga,thn mwenyekit na mimi ndo nlikuwa nyuma kabisa. Nkaona mara ya tano atanivaa bure ikabid NIMUITE YULE MGANGA TENA KWA UPOLE WA HALI YA JUU. NIKAMUOMBA HIRIZI MOJA NA MM NIVAE. Hyo nadhan ndo ilikua ponea yangu kwa vitu nlivyokutana navyo pale baada ya kuvaa hyo kitu.