Wafahamu nyoka hatari Zaidi duniani

Wafahamu nyoka hatari Zaidi duniani

Kuna kipindi flani, kwenye channel ya 'Nat geo wild' kinaitwa 'snake in the city' jamaa mmoja na demu wake, wanawakamata hao akina black mamba 'kama hawana akili nzuri.
 
Kuna kipindi flani, kwenye channel ya 'Nat geo wild' kinaitwa 'snake in the city' jamaa mmoja na demu wake, wanawakamata hao akina black mamba 'kama hawana akili nzuri.
Huyo jamaa anakamata koboko wadogo wadogo tena kila ukimuita unamlipa dola arobaini lakini koboko waliokomaa wako nchi ya Zimbabwe na Msumbiji.
 
1. TAIPAN WA ARDHINI:

Nyoka huyu ni wa kwanza kuwa na sumu kali duniani, anaeishi ardhini tu. aking'ata kitu chochote hutoa sumu kiasa cha milligram110 iliyo na uwezo wa kuua binadamu 100 au panya 250,000.

2. NYOKA WA BRAUNI KUTOKA MASHARIKI:

Nyoka huyu anayepatikana kwa wingi Australia anashikilia nafasi ya pili kwakuwa na sumu kali sana ambayo 1/14,000 ya tone la sumu humuua mtu mzima kwa muda mfupi, anasifika pia kwa kuwa na spidi sana ya kukimbia.

3. KRAIT WA BLUU

Nyoka huyu anayepatikana Kusini mashariki mwa bara la Asia na indonesia anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na sumu kali, 50% ya kung'ata kwake husababisha kifo au kuparalyse na ni vigumu kupona hata kwa matumuizi ya dawa ya kumaliza makali sumu ya nyoka(Antivenin).
Nyoka huyu pia ana sifa ya kuwashambulia na kuwauwa nyoka wenzake hata wa jamii yake

4. TAIPAN

Nyoka huyu anaeshikilia nafasi ya nne anaptaikana nchini Australia, ana sumu kali iliyo na uwezo wa kuua nguruwe wa guinea 12,000, pia katika ung'ataji wake husababisha kifo ndani ya lisaa limoja.

5. BLACK MAMBA

Nyoka huyu anayepatikana sehemu nyingi ya Africa anashika nafasi ya tano huku akiwa anaogopeka sana kwa ukali wa sumu yake na ushambuliaji wake.
Ana uwezo wa kushambulia kwa kurusha sumu hadi mara 12 kwa wakati mmmoja ambayo huweza kuuwa binadamu 10 hadi 25 kwa wakati mmoja. Ung'ataji wake mmoja hutoa sumu kiasi cha milligram 100 hadi 120.
Huwa anasifika sana duniani kwa kuwa nyoka wa kwanza mwenye mbio ardhini akiwa na uwezo wa kukimbia kilometa 20 kwa lisaa limoja.
Nyoka huyu anapatikana pia Tanzania hivyo si vibaya tukimjua zaidi ili ukisikia yupo sehemu utafute namna ya kujihami nae...
MAMBAS ni aina ya nyoka wakali wapatikanao ktk dunia ya leo. Ni nyoka wenye sumu kali na wenye kasi ktk mwendo na wana sifa ya kutaga mayai (oviparous).
Kuna aina mbili za mambas :
1. GREEN MAMBAS.
2. BLACK MAMBAS.
Green mamba wanasumu aina ya NEUROTOXIC na HAEMOTOXIC. Wanaishi miaka 12 hadi 14 (makadirio kulingana na takwimu za sayansi) wanataga mayai na kuanguliwa kwa siku 80 hadi 90.
BLACK MAMBA pia wanauwezo wa kupanda miti wakati wakitafuta chalula na wanaurefu kati ya sentimita 220 hadi 320. Ni kati ya nyoka wenye sumu kali wapatikanao Afrika. Wanataga mayai kati ya 12 na 18,na kuangua kati ya siku 80 hadi tisini.
Mambas ni nyoka wakali na wenye kung'ata zaidi ya mara moja kwa sababu meno yao hayang'oki wakati wakigonga kitu. Meno yanayong'oka kwa nyoka yanaitwa FRONT FANGED MOVABLE na yasiyong'ooka yanaitwa FRONT FANGED FIXED.
Iwapo nyoka hawa wata kung'ata utaweza kuishi kati ya dakika 20 (kwa mujibu wa utafiti) Na kupoteza maisha...
Nutnux
Asante sana kwa hili uliloleta.
Norshad na upepo wa pesa nimependa sana mchango wenu katika nyuzi hii ya aina za Nyoka.
Hizi ndizo presentations that JF deserves, kama wengi wetu tungelikuwa hivi tungelikuwa mbali. Keep it up!
 
Nakumbuka nilikuwa natoka kuokota kuni porin huko kijijin (kwa wa dar kuni ni miti iliyokauka kwa ajil ya kupikia) nimejitwika kuni zangu nateremka kurudi mara naona nyasi zinatingishika kwa kas mara paaap naona nyoka mrefu anakimbia balaa kuja upande wangu sikutaka kujiuliza nikatupa mzigo chini hizo spidi nilizotoka nazo sikumbuk ila nikajikuta niko kulekule nilikookotea kuni kuwafuata wengine akiri haikuwa ya kawaida mpaka nikapewa togwa (juice ya mahindi na ulezi)
 
Nakumbuka nilikuwa natoka kuokota kuni porin huko kijijin (kwa wa dar kuni ni miti iliyokauka kwa ajil ya kupikia) nimejitwika kuni zangu nateremka kurudi mara naona nyasi zinatingishika kwa kas mara paaap naona nyoka mrefu anakimbia balaa kuja upande wangu sikutaka kujiuliza nikatupa mzigo chini hizo spidi nilizotoka nazo sikumbuk ila nikajikuta niko kulekule nilikookotea kuni kuwafuata wengine akiri haikuwa ya kawaida mpaka nikapewa togwa (juice ya mahindi na ulezi)
Una bahati sana ungezubaa angekuja kukusimamia usoni huku amepanua mdomo wake mweusi.
 
2604842108_85d57ac987_b.jpg

Koboko huwa na miujiza fulani hivi,tazama huyo ndege anavyomshangilia.
 
Kama ingelikuwa ni kweli, basi angekuwa nyoka muoga kuliko wote duniani.
Black Mamba kamwe hakimbii Hatariii NEVER... Jamaa huwa anaikimbiza hatarii!! Afuu koboko mkubwa anaweza toa sauti kubwaa kama kufoka hivi... Wanyama wakiisikia mbioo... Ni nyokaa anaegongaa bila Kuacha meno soo anaweza gonga watu hata 100 kwa muda mchache sanaaa...Na speed yake sio ya nchi hii
 
Ushahidi wa koboko kukimbiza watu huu hapa tena koboko mwenyewe bado mdogo.
paul-mamba3.jpg
 
Mimi nafuga black mamba (koboko) hapa nyumbani....huyu niliyenaye ni mwanamme kwa hiyo kama kuna mtu ana jike lake tafadhali naomba tuwasiliane.
 
C
mayai ya black mamba ni matamu sana, ila upatikanaji wake ndio changa moto. mie kuna sehemu tulikua kambi maeneo ya tabora tukawa pale ambapo tunapumzika , kwa juu yake palikua ni makazi yake jioni, wakati anarudi nae kupumzika ibabi muiache njia kwa mda apite , tofauti na hapo ugovi unakua umeutafuta mwenyewe na mmoja tulimuua
Yo makoboko kweli(ni jina la utani la hcho kijiji)
 
Mkuu mleta hii thread kwakweli umenikumbusha mbaaali sana. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimevaa IRIZI shingoni pale Tabora wilaya moja inaitwa SIKONGE. Hakika sitosahau huyu nyoka anayeitwa KOBOKO(MAMBERS). Nilifika pale kufanya tafiti maalum hivyo ilinilzimu kufika hadi maeneo yasiyofikika kirahisi. Baada ya kuripoti kwa m/kiti wa kijiji nikapokelewa vizur tuu ila nilipomwambia sehemu ninazohitaj kufika alishtuka na kushika kichwa baadae akanambia ngoja nimuite mtaalamu mmoja aje ili twende nae. Kwa bahat mbaya sana hilo pori hatari linaloogopwa ndipo kuna hawa wadudu na hakuna njia ya gari hvyo ni lazma kupita kwa mguu. Basi mtaalamu tuliekuwa tunamsubiria akafika akiwa na kabegi kadogo cha ngozi ubavuni kwake. Heee,si alivyokafunua hivi akatoa nyeusi NNE(4)!!!? Akasema kila mmoja avae thn twende tuanze kazi,yan mimi 1,dereva wangu 1 na wenyewe moja moja. Mimi nikagoma nikasema tapita hivyohvyo huko porini mana hvyo vitu siviamini. Na dereva alivyojua kuwa kule gari halipiti akasema yeye hatoenda porini maana inabd alinde gar akat sisi tunaingia porini.Asee,NLIKUWA NIKITEMBEA KAMA HATUA 15 HADI 20 haijulikani wanatokea wapi wale wadudu(tuliambiwa tusiwaite koboko tuseme mdudu) unamuonea hapa tit4tat. Ile hali ilitokea mara nne maana mbele alitangulia mganga,thn mwenyekit na mimi ndo nlikuwa nyuma kabisa. Nkaona mara ya tano atanivaa bure ikabid NIMUITE YULE MGANGA TENA KWA UPOLE WA HALI YA JUU. NIKAMUOMBA HIRIZI MOJA NA MM NIVAE. Hyo nadhan ndo ilikua ponea yangu kwa vitu nlivyokutana navyo pale baada ya kuvaa hyo kitu.
 
Sio huko tu hata hapa nyumban tanzania ndani ya JWTZ kuna kikosi maalumu( Special force) Kinaitwa BLACK MAMBA( KOBOKO) ndicho kilichowezesha kumuondoa Idd Amin na majeshi yake TZ na UG...na Pia ndicho kilichoongoza mapigano ya kukiondoa kikundi naweza kukiita cha wahauni (M23) huko Congo chini ya mwanaume Maj gen Mwakibolwa!!!
Hata waSouth wana kikosi cha special forces kinaitwa koboko.
 
Back
Top Bottom