Wafahamu manabii waliokaa mahabusu na kufungwa jela (ikiwamo kwa sababu za kisiasa)

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,890
WAFAHAMU MANABII WALIOKAA JELA , (WENGI SABABU ZA KISIASA)

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Kipimo namba moja cha Nabii au mtumishi wa Mungu ni HAKI, Ikiwa nabii au mtumishi wa Mungu hatakuwa na sifa hiyo basi ni wazi yeye sio nabii wala sio mtumishi wa Mungu, huwaga nawaitaga wahuni tu.

Mtumishi wa Mungu lazima awe mtenda haki na sio hivyo tuu bali mtetezi wa haki ndani ya jamii inayomzunguka. Huwezi kusema unahaki wakati hujawahi kuitetea haki ndani ya jamii yako. Niliwahi kusema na leo nasisitiza, ikiwa kiongozi wako wa dini uliyomo hajawahi kutetea haki katika jamii yako, hama hiyo taasisi(kwa maana madhehebu ni taasisi, dini imo moyoni mwa mtu). Hatuwezi kuwa na wachungaji, masheikhe, maimamu, mapadri, maaskofu na watumishi wa madhehebu kwa aina za majina yao ambao hawezi kutetea haki. Mtu yeyote asiyeweza kutetea haki, jua hana haki, kila mmoja anauwezo wa kutetea haki ndani ya jamii katika mazingira yake.

Hatuwezi kuwa na viongozi wa dini ambao kwao utumishi wa MUNGU ni kubobea katika simulizi za kale za kiyahudi, hatuwezi kuwa na viongozi wa dini ambao kazi yao kubwa ni kusimulia hadithi za kina Yakobo, sijui Daudi, sijui Yesu na wahenga wengine waliomo kwenye Biblia. Tunahitaji watetezi wa haki, watenda haki kwa maana lengo la maisha ni UPENDO, na upendo uwepo sharti haki iwepo.

Ukiona Mtumishi wa Mungu anaogopa wanasiasa ujue huyo sio mtumishi wa Mungu bali MSAKATONGE kupitia mwamvuli wa dini.
Maisha bila haki hayafai kitu, siku hizi dhuluma inaongezeka kwa sababu matapeli ndani ya dini yameongezeka, utapeli ni pamoja na kushindwa kutetea haki ndani ya jamii.

Ukiona kuna wizi serikalini, ukiona mafisadi, ukiona rushwa imekithiri, ukiona viongozi wa kisiasa wanafanya watakavyo pasipo kuogopa, wanadhulumu wananchi, ukiona polisi wanafanya uonevu na viongozi wa dini wapo kimya, na wewe unaenda kusali kwenye taasisi hiyo hiyo ujue unamatatizo tena makubwa sana. Ili jamii iharibike sharti iwe na viongozi wa dini walioharibika. Viongozi wanaoshindwa kukemea kwa nguvu zote uovu.

Haki haikai kwa mtu muoga, hapana haki kwa jamii ya watu waoga. Ukiona mtumishi wa Mungu ni Muoga ujue sio mtumishi huyo bali amejificha tuu katika kichaka cha utumishi.

Uliwahi ona wapi mtumishi wa Mungu akaogopa Jela?
Uliwahi ona wapi mtumishi wa Mungu akaogopa Polisi?
Uliwahi ona wapi mtumishi wa Mungu akaogopa Kufa?

Kibinadamu kuna wakati woga unakuwepo lakini kwa vile roho wa Mungu anakaa ndani yao woga unaondoka automatic.

Niwe muwazi, sipendi kuona mtu anayejiita mchungaji au sheikhe alafu ashindwe wajibu wake, kuitetea jamii yake, kutetea haki. Alafu wanakazania kutisha watu na mafundisho ya kutia watu hofu.

Tunahitaji viongozi watakaosema kuwa, hatuwezi kuzitii mamlaka ambazo hazitendi haki, tunataka viongozi wa hivyo. Sio mtuletee Aya za kutia watu hofu wasitetea haki ndani ya jamii zao.

WAFUATAO NI MANABII WALIOONJA JOTO LA JIWE JELA KWA KUTETEA HAKI;

1. Nabii Jeremia
Yeremia ni mtoto wa Hilkia, kuhani katika mji wa anathothi, huko nchi ya Benjamini, yaani ni Mbenjamini. Baada ya Mfalme Sedekia na maofisa wake kumuasi MUNGU, Nabii Yeremia anatumwa kwenda kumpa unabii kuwa nchi yake itavamiwa na kupigwa na Wakaldayo kwa sababu ya uovu wa utawala wa Sedekia na maofisa wake.

Licha ya kuonywa lakini Mfalme Sedekia na maofisa wake wakakaidi,
Badala yake wakamsweka korokoroni. mahabusu kama sio jela.

Yeremia 37;
15Maofisa hao walimkasirikia sana Yeremia wakampiga, kisha wakamfunga gerezani katika nyumba ya katibu Yonathani iliyokuwa imegeuzwa kuwa gereza.

16Yeremia alipokuwa amefungwa gerezani kwa muda wa siku nyingi,
17mfalme Sedekia alimwita na kumkaribisha kwake. Mfalme akamwuliza kwa faragha wakiwa nyumbani mwake; “Je, kuna neno lolote kutoka kwa Mwenyezi-Mungu?” Yeremia akamjibu, “Naam! Lipo!” Kisha akaendelea kusema, “Wewe utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babuloni.”

18Halafu Yeremia akamwuliza mfalme Sedekia, “Nimekukosea nini, au nimewakosea nini watumishi wako au watu hawa, hata unitie gerezani? 19Wako wapi manabii waliokutabiria wakisema, ‘Mfalme wa Babuloni hatakushambulia wewe wala nchi hii?’

2. NABII MIKAYA
Huyu sio maarufu lakini naye ni miongoni mwa manabii waliopo kwenye Biblia waliokaa Jela kwa kusema ukweli pasipo kuficha. Hata Mfalme Ahabu mwenyewe alikuwa akimfahamu kwa kusema ukweli na kumchana makavu, jambo ambalo Mfalme alikuwa halipendi.

1 Wafalme 22:
7Lakini, Yehoshafati akasema, “Je, hapa hakuna nabii mwingine wa Mwenyezi-Mungu ambaye twaweza kumwuliza shauri?”
8Naye mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Yupo, bado mmoja, Mikaya mwana wa Imla. Yeye twaweza kumwuliza shauri la Mwenyezi-Mungu. Lakini namchukia sana kwa sababu yeye, kamwe hatabiri jambo jema juu yangu, ila mabaya tu.” Yehoshafati akamwambia, “Si vizuri mfalme kusema hivyo.” 9Basi, Ahabu, mfalme wa Israeli, akamwita mtumishi mmoja, akamwamuru, “Haraka! Nenda ukamlete Mikaya mwana wa Imla.”

16Lakini mfalme akamwambia, “Nitakuapisha mara ngapi kwamba unaposema nami kwa jina la Mwenyezi-Mungu, ni lazima uniambie ukweli mtupu?” 17Ndipo, Mikaya akasema, “Niliona watu wote wa Israeli wametawanyika milimani kama kondoo wasio na mchungaji. Naye Mwenyezi-Mungu akasema, ‘Watu hawa hawana kiongozi; basi warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.’”

18Hapo, mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kamwe hatatabiri jema juu yangu ila mabaya tu?” 19Kisha Mikaya akasema, “Haya sikia neno la Mwenyezi-Mungu: Nilimwona Mwenyezi-Mungu ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni limesimama kando yake, upande wake wa kulia na wa kushoto; 20ndipo Mwenyezi-Mungu akauliza, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu aende akaangamie huko Ramoth-gileadi?’ Kila mmoja akajibu alivyofikiri. 21Kisha pepo mmoja akajitokeza mbele ya Mwenyezi-Mungu, akasema, ‘Mimi nitamshawishi.’ 22Mwenyezi-Mungu akamwuliza, ‘Kwa mbinu gani?’ Naye akajibu, ‘Nitakwenda na kuwafanya manabii wake wote waseme uongo.’ Mwenyezi-Mungu akamwambia, ‘Wewe utamshawishi na utafaulu; haya, nenda ukafanye hivyo.’ 23Basi, ndivyo ilivyo: Mwenyezi-Mungu amewafanya hawa manabii wako wote waseme uongo. Mwenyezi-Mungu amenena mabaya juu yako!”

24Hapo, Sedekia, mwana wa Kenaana, akamkaribia Mikaya, akampiga kofi shavuni na kumwuliza, “Tangu lini Roho ya Mwenyezi-Mungu ikaniacha mimi, ikaja kunena nawe?” 25Mikaya akamjibu, “Siku utakapoingia katika chumba cha ndani kujificha, ndipo utakapojua.” 26Naye mfalme wa Israeli akatoa amri, “Mkamateni Mikaya; mrudisheni kwa Amoni, mkuu wa mji, na kwa Yoashi mwana wa mfalme. 27Waambie wamtie gerezani na kumlisha mkate kidogo na maji, mpaka nitakaporudi salama.” 28Ndipo Mikaya aliposema, “Ukirudi salama basi, utajua kwamba Mwenyezi-Mungu hakunena nami.” Kisha akaendelea kusema, “Sikilizeni enyi watu wote!”

3 NABII YOHANA MBATIZAJI
Mathayo 14:
3 Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumweka gere zani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, kaka yake.
4 Kisa che nyewe ni kwamba Yohana alikuwa amemwambia Herode kuwa, “Si halali kwako kumwoa huyo mwanamke.” 5 Herode alitaka sana kumwua Yohana lakini akaogopa watu kwa maana walimtambua kuwa ni nabii.

6 Lakini siku ya kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya watu walioalikwa akamfurahisha sana Herode.

7 Naye akaahidi kwa kiapo kumpa huyo binti lo lote atakaloomba. 8 Kwa kushawishiwa na mama yake, huyo binti akasema, “Nipatie kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.”

9 Mfalme akajuta; lakini kwa ajili ya kile kiapo alichoapa mbele ya wageni, aliamuru kwamba ombi lake litekelezwe. 10 Akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani, 11 na kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.

4. PAULO NA SILA
Matendo ya mitume 16
19Matajiri wa yule msichana walipoona kwamba tumaini lao la kupata mali limekwisha, waliwakamata Paulo na Sila, wakawaburuta mpaka hadharani, mbele ya wakuu. 20Wakawashtaki kwa mahakimu wakisema, “Watu hawa ni Wayahudi na wanafanya fujo katika mji wetu. 21Wanafundisha desturi ambazo sisi raia wa Roma haturuhusiwi kuzikubali wala kuzifuata.” 22Kundi la watu likajiunga likawashambulia; na wale mahakimu wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakaamuru wapigwe viboko. 23Baada ya kupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wa gereza akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzi mkali. 24Kutokana na maagizo hayo, huyo askari aliwaweka katika chumba cha ndani kabisa cha gereza na kuifunga miguu yao kwenye nguzo.

Kutokana na muda na wengi hampendi makala ndefu basi naweza wataja kwa ufupi tuu waliowahi kuonja joto la mahabusu,
5. Yusufu mwana wa Yakobo
6. Daniel Mwonaji
7. Mtume Petro
8. Mtume Yohana(aliyeandika kitabu cha Ufunuo) Huyu alifungwa kifungo cha nje, katika kisiwa cha Patmo huko aishi peke yake na wanyama wa mwituni.

Linapokuja swala la haki, na ukweli lazima watu walitetee ili kuiepusha jamii na uharibifu. Wazazi, viongozi wa madhehebu na viongozi wa serikali ni lazima tuhakikishe haki inasimamiwa.

Ni yule Mtibeli,
Kuhani katika Hekalu Jeusi,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro
 
Ndio maana mimi siku zote huwa naseme hamna jipya katika dunia ya leo zaidi ya teknolojia.

Ukiwa muumini mzuri wa historia, jamii itaamini wewe ni kiona mbali lakinii kumbe ni historia tu ndio inakuongoza kutafsiri matendo na kujua nini kitatokea baadae.

Halikadhalika, ukiwa muumini mzuri wa maandiko matakatifu, jamii itakuona kama Nabiii kumbe unatumia maandiko kutafsiri unayoyaona na kujua nini kinaweza kutokea.

Hivyo, ukitaka kujua nini yatakuwa matokeo ya kumfunga Mbowe, soma historia ya wanaofungwa kwasababu za kisiasa na pia uyarejee maandiko matakatifu.

Na ukitaka kujua kwaninii haya yanatokea na kwanni watawala hujaa viburi mpaka yatimie(waanguke), soma zaidi maandiko matakatifu na pengine huntamshangaa Mama maushingi kuwa na moyo mgumu kwani inabidi iwe hivyo kabla ya anguko lake na la chama kutokea.
 
Robert, nimelisoma andiko lako lote, huku nikiwa bado na shauku ya kuendelea kusoma zaidi.

Umenena vyema. Umeweka falsafa yako ya jumla, ukalipa andiko lako nguvu kubwa kwa kutolea uthibitisho kutoka kwenye biblia, ambao ni mwongozo mkuu wa kazi yake kwake aitwaye Askofu, padre, nabii, mtume au mtumishi.

Hakika, neno la Mungu kwa kadiri ya Biblia au msahafu, siyo kitabu cha historia, bali ni neno na ujumbe unaoishi. Biblia na msahafu, ni neno lenye majibu ya wakati wote. Viongpzi wa dini wamegeuza neno la Mungu kuwa ni ujumbe wa historia.

Mungu aliwaleta manabii wake Duniani na hata mwanaye wa pekee, siyo kutengeneza historia bali kumwonesha mwanadamu kwa nafasi yake aliyopo anavyostahili kutenda wakati wote.

Nabii mwenye Roho wa Mungu, akisoma aya hizo za Biblia, anastahili kuja na maswali kadhaa:

1) Je, mimi ndiye Yeremia au Mikaya wa leo?
2) Nani mfalme Sedekia au Ahabu wa leo?
3) Nini ujumbe wangu kama nabii kwa mfalme
4) Nini gereza langu la leo? Ni pesa, woga, unafiki au mahabusu za akina Kingai?

Hawa manabii, watumishi, mapdare na maaskofu wa kuhimiza tu sadaka na michango, ni manabii wa malimwengu na siyo manabii wa Mungu.
 
Robert, nimelisoma andiko lako lote, huku nikiwa bado na shauku ya kuendelea kusoma zaidi.

Umenena vyema. Umeweka falsafa yako ya jumla, ukalipa andiko lako nguvu kubwa kwa kutolea uthibitisho kutoka kwenye biblia, ambao ni mwongozo mkuu wa kazi yake kwake aitwaye Askofu, padre, nabii, mtume au mtumishi...
 
Ndio maana mimi siku zote huwa naseme hamna jipya katika dunia ya leo zaidi ya teknolojia.

Ukiwa muumini mzuri wa historia, jamii itaamini wewe ni kiona mbali lakinii kumbe ni historia tu ndio inakuongoza kutafsiri matendo na kujua nini kitatokea baadae.

Halikadhalika, ukiwa muumini mzuri wa maandiko matakatifu, jamii itakuona kama Nabiii kumbe unatumia maandiko kutafsiri unayoyaona na kujua nini kinaweza kutokea.

Hivyo, ukitaka kujua nini yatakuwa matokeo ya kumfunga Mbowe, soma historia ya wanaofungwa kwasababu za kisiasa na pia uyarejee maandiko matakatifu.

Na ukitaka kujua kwaninii haya yanatokea na kwanni watawala hujaa viburi mpaka yatimie(waanguke), soma zaidi maandiko matakatifu na pengine huntamshangaa Mama maushingi kuwa na moyo mgumu kwani inabidi iwe hivyo kabla ya anguko lake na la chama kutokea.

Kula tano mkuu.
 
Umeandika vizuri sana, naliona anguko la watawala wa Sasa, tunachopashwa kuomba kama Taifa ni kuomba anguko lisilo na fujo Wala mauaji, lakini anguko no dhahiri, maamdishi yapo ukutani, shida hakuna wa kuyatafsri. ' MENEME TEKELI NA PERESI''
 
Umeandika mengi lakini ya napnyesha upeo mdogo. Wa uelewa manabii wa agano la kale ndio waliowateua wafalme na kuwaweka madarakani . Hivyo kukemea wafalme kwao ilikuwa sawa sababu ndio waliweka madarakani

Yohana mbatizaji hakumuweka Mfalme Herode madarakani akajitia kumuonya akamkata kichwa
 
Back
Top Bottom