Ni Tanzania pekee ambapo Mungu ni kwaajili ya viongozi; hata watende ubaya gani utasikia Mungu ameamua. Masikini mwovu hana Mungu, ni mali ya jela

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Kati ya jambo ambalo sitadhubutu kumuhusisha Mungu nikatika ukatili wa kiongozi dhidi ya anaowaongoza.
Naamini hakuna Mungu wa viongozi waovu bali Mungu ni wa wenye haki. Naamini haki ya kuishi Ben Sanane na wengine wengi ni haki ya kila mmoja na Mungu hakuwahi kuamua vinginevyo. Naamini haki ya kutendewa wema haiwezi ijapokuwa na wanadamu kwa madaraka yao.

Sasa hivi Tanzania kumeibuka kundi la watu ambao kama familia yake haikuathirika na jambo flani yeye uliunga mkono na kushangilia kwamba ni kazi ya Mungu. Wapo viongozi wa dini na wanasiasa wanaona kwa macho ya nyama makosa yakitendeka lakini wanasema mwachie Mungu.

Unajiuliza kazi ya mahakama Duniani ni nini? Kama tunaamini kumwachia Mungu inatosha kwanini maskini waendelee kusota magerezani? Kwanini tuamini kwamba Mungu wa Tanzania siyo wa maskini bali yupo kwa ajili ya matajiri na viongozi? Kuliko tumsingizie Mungu si bora tukae kimya?

Tusipojifunza kukemea uovu katika jamii inayotuzunguka wasio na haki watazidi kufanya maamuzi yakutoshirikiana na Mungu wa viongozi na matajiri na kuamua kushirikiana na Mungu aliyepo mahakamani kama ambavyo Ulaya na nchi nyingine wamefanya. Hakuna haki Ulaya inapatikana kwenye nyumba za ibada, haki inapatikana kwa tafsiri ya maandishi ambayo ni sheria.

Kama tukiendelea kuishi kwa ubaguzi nakutumia vitabu vitakatifu kutoa tafsiri kulingana na uwezo wa kiuchumi wa waumini wetu basi ipo siku nyumba za ibada zitafungwa
 
Mkuu ni ushauri mzuri kwetu sote. Ijulikane kuwa anayekaa kimya huku akitazama/akishuhudia jirani yake akifanyiwa uovu/ukatili ajue naye ni mshirika kamili wa ouvu huo!
 
Hata Dhahabu ikigunduliwa kwako ni mali ya serikali ila bangi mali yako.
 
Kati ya jambo ambalo sitadhubutu kumuhusisha Mungu nikatika ukatili wa kiongozi dhidi ya anaowaongoza.
Naamini hakuna Mungu wa viongozi waovu bali Mungu ni wa wenye haki. Naamini haki ya kuishi Ben Sanane na wengine wengi ni haki ya kila mmoja na Mungu hakuwahi kuamua vinginevyo. Naamini haki ya kutendewa wema haiwezi ijapokuwa na wanadamu kwa madaraka yao.

Sasa hivi Tanzania kumeibuka kundi la watu ambao kama familia yake haikuathirika na jambo flani yeye uliunga mkono na kushangilia kwamba ni kazi ya Mungu. Wapo viongozi wa dini na wanasiasa wanaona kwa macho ya nyama makosa yakitendeka lakini wanasema mwachie Mungu.

Unajiuliza kazi ya mahakama Duniani ni nini? Kama tunaamini kumwachia Mungu inatosha kwanini maskini waendelee kusota magerezani? Kwanini tuamini kwamba Mungu wa Tanzania siyo wa maskini bali yupo kwa ajili ya matajiri na viongozi? Kuliko tumsingizie Mungu si bora tukae kimya?

Tusipojifunza kukemea uovu katika jamii inayotuzunguka wasio na haki watazidi kufanya maamuzi yakutoshirikiana na Mungu wa viongozi na matajiri na kuamua kushirikiana na Mungu aliyepo mahakamani kama ambavyo Ulaya na nchi nyingine wamefanya. Hakuna haki Ulaya inapatikana kwenye nyumba za ibada, haki inapatikana kwa tafsiri ya maandishi ambayo ni sheria.

Kama tukiendelea kuishi kwa ubaguzi nakutumia vitabu vitakatifu kutoa tafsiri kulingana na uwezo wa kiuchumi wa waumini wetu basi ipo siku nyumba za ibada zitafungwa
Acha unyonge kenge wewe
 
Back
Top Bottom