omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 145
Nimepata taarifa kuwa wafadhili kadhaa wakubwa wamekata msaada wao kwa taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation. Ni wazi hili litakuwa pigo kubwa kwa Mzee Ben lakini pia kwa watanzania ambao walikuwa wakifaidika na mfuko huu. Kwa upande mwengine nadhani hili linaweza kuwa ujumbe makini kwa waheshimiwa wengine kuangalia matendo yao wanapokuwepo madarakani.
Naogopa kuwa kimbunga hiki kinaweza kuwakumba waheshimiwa wengine wengi ambao wakiwa madarakani waliweza kuwavutia wafadhili/wawekezaji kadhaa katika miradi mbalimbali ya kijamii kama vile mashule, zahanati, ufadhili wa masomo, miradi ya vitabu n.k Sasa hawa jamaa wakiamua kuendelea na kimbunga hiki kilichoikumba Benjamin Mkapa Foundation naamini wahanga watakuwa wengi na wengi wao wasio kuwa na hatia yoyote.
Tulijadili hili kwa umakini zaidi ya ule ushabiki wetu tuliozoea
Omarilyas