SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,164
- 7,941
Habari za mipango ya kufanyiwa ukarabati uwanja wa Benjamin Mkapa zimeanza kutolewa zaidi ya miezi 3 iliyopita. Najua serikali ina taratibu zake kuanzia kutafuta pesa hadi wazabuni wa kufanya kazi husika, ila naona kuna hali fulani ya kujikongoja na kujivuta kwenye suala hili. Zamani kabisa niliwahi kutoa angalizo kuwa Simba ijiandae kwa lolote kwenye hili suala. CAF walitoa mwongozo wa mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi mapema yawe yamekamilika (nadhani walitoa hadi mwezi wa 6 au 7). Wote tukiangalia uwanja unavyofanana sasa, kidogo unaweza kuona labda pitch tu ndiyo kidogo imeboreshwa lakini siyo sana, maeneo mengine yote hayajaguswa. Sina uhakika kama kile walichotaka kuwa kimefanyika kweli kimefanyiwa kazi.
Nikiangalia list ya vitu na maeneo yaliyotajwa yanaenda kufanyiwa kazi katika ukarabati huu, sioni ni jinsi gani haya yote yanaweza kufanyika ndani ya miezi 2 tena wakati huo huo uwanja ukiendelea kutumika. Najua Wachina wanaweza kufanya kazi usiku na mchana ila nina wasiwasi sana na hili suala. Pia nitashangaa sana CAF waendelee kuweka rehani maandaliizi ya kiwango cha juu ya uzinduzi na ratiba za mashindano kwa ukarabati huu wa dakika za lala salama.
Natoa tu angalizo maana huu wasiwasi wangu nimekuwa nautoa kwa miezi kadhaa sasa. Tusipokuwa makini, Tanzania itapoteza uenyeji wa uzinduzi wa mashindano haya.