Wafadhili wakata ufadhili wao BENJAMIN MKAPA FOUNDATION | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafadhili wakata ufadhili wao BENJAMIN MKAPA FOUNDATION

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by omarilyas, Feb 22, 2009.

 1. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimepata taarifa kuwa wafadhili kadhaa wakubwa wamekata msaada wao kwa taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation. Ni wazi hili litakuwa pigo kubwa kwa Mzee Ben lakini pia kwa watanzania ambao walikuwa wakifaidika na mfuko huu. Kwa upande mwengine nadhani hili linaweza kuwa ujumbe makini kwa waheshimiwa wengine kuangalia matendo yao wanapokuwepo madarakani.

  Naogopa kuwa kimbunga hiki kinaweza kuwakumba waheshimiwa wengine wengi ambao wakiwa madarakani waliweza kuwavutia wafadhili/wawekezaji kadhaa katika miradi mbalimbali ya kijamii kama vile mashule, zahanati, ufadhili wa masomo, miradi ya vitabu n.k Sasa hawa jamaa wakiamua kuendelea na kimbunga hiki kilichoikumba Benjamin Mkapa Foundation naamini wahanga watakuwa wengi na wengi wao wasio kuwa na hatia yoyote.

  Tulijadili hili kwa umakini zaidi ya ule ushabiki wetu tuliozoea

  Omarilyas
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Source please....
   
 3. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Hii stori naona kama haijakaa bado vizuri. Zaidi ya kutaja source na kutaja wafadhili waliojitoa, ni vyema pia kujua wamejitoa kwa sababu zipi. Tukumbuke kuwa kama alikuwa na wafadhili wengi wa marekani, hivi sasa foundation nyingi zimekatiwa funding kutokana na global economic crisis. Mkikumbuka ile ponzi scheme ya Madoff, waliumia wengi ambao walikuwa wafadhili. So mi sioni kama tunaweza kusema mapema hivi kuwa eti ni ishara ya wafadhili kukosa imani na Ben. Let's wait for things to play out, lakini asante mkuu kwa taarifa zako.
   
 4. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  bado nyeti.......

  omarilyas
   
 5. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nina list ya Foundation na watu binafsi wote walioumizwa na Mardoff scandal sijaona CLINTON GLOBAL INITIATIVE na BILL AND MELINDA GATE Foundation...

  Umeshawahi kuona nikiibuka tu kuanzisha topic kama sina uhakika na source zangu....

  omarilyas/tanzanianjema
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kama ni kweli mie naona ni poa tu!

  Maana niliona kama ni ubaguzi wa wafanyakazi...mtu unamleta Daktari unamlipa mara 3 ya wengine..kwa pesa ya Foundation ya Mkapa..je wengine watajisikiaje?

  This was another experiment which was doomed to fail!

  Serikali itoe tu posho zaidi kuwalipa wafanyakazi wote kwa usawa ktk maeneo magumu na sii kuwabagua wengine kwa scheme kama Mkapa Foundation!

  Kwa nini serikali isitoe sera tu kuwa ktk zile wilaya za mbali..mfanyakazi atalipwa 50% zaidi ya mshahara wa Wilaya zilizo karibu na Dar, au miji mingine?

  Or kwa wote watakaoenda ktk hizi Wilaya...wasamehewe kodi as an incentive?
   
  Last edited: Feb 23, 2009
 7. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Omarilyas mkuu, heshima kwako, nilisema kuwa ni muhimu tujue hao wafadhili ni akina nani. Umetaja wafadhili wawili
  - Clinton Global Initiative - kwanza tuelewe ya kuwa Clinton hatumii pesa zake bali anatumia nafasi yake na umaarufu wake kukusanya pesa kutoka wafadhili na kuwapa charity mbalimbali. Na yes, wafadhili wa Clinton Foundation wamekuwa affected with the Madoff ponzi scheme
  - Bill and Melinda Gates Foundation - sina taarifa ya wao kuwa affected directly
  Kama una majina mengine tutaweza kuendeleza mjadala.
  BTW kama una taarifa zaidi basi itakuwa vizuri ukiweza kutueleza sababu zilizotolewa na wafadhili hawa kusimamisha ufadhili wao.
  Shukrani
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sierikali ya Norway ilitoa $ 3 millions au zaidi ktk kuanzisha Mkapa Fellows Foundation (MFF)..wafadhili wengine sijui walitoa kiasi gani!
   
 9. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ninayo list ya wafadhili wa Bill Clinton Foundation walioitoa hivi karibuni.....nikapata muda nita-owanisha na wale walioliwa na Mardoff...

  Lakini ukweli ni kuwa Mzee wetu jina limeharibika sana kutokana na scandals za nyumbani...Na maoni haya nimeyasikia kwa watu (wa ughaibuni) waliokuwa wakimwagia sifa sana enzi zile za mwisho wa utawala wake

  Omarilyas
   
 10. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na Norway kwa pamoja na nchi zingine za scandinavia ndio zipo mstari wa mbele katika kumshurutisha JK kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika "WOTE" wa UFISADI nchini.....

  omarilyas
   
  Last edited: Feb 22, 2009
 11. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #11
  Feb 22, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mnataka sababu? LOL
   
 12. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kama ni noma acha iwe noma ahsanteni wazungu kw akukataakuchangia fisadi mkuu
   
 13. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mwanahaki, mkuu, ni vyema kuestablish fact from wishful thinking...
   
 14. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2009
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  ..facts nilizonazo kuhusu BMAF ni kuwa mpaka sasa, Mkapa fellows(madaktari, nurses,etc walioajiriwa chini ya taasisi ya BMF huko wilayani) waliandikiwa baru muda mrefu tu,miezi zaidi ya 4 iliyopita wakitakiwa kujiunga na ajira za halmashauri walizokuwa wanafanyia kazi. Initiqal plan ilikuwa fellows wanapewa contract ya 3 years na BMF, baada ya hapo watakuwa absorbed kwenye govt system,Norway walitoa hela ya 3 years, with a promise ya kutoa more for 7 years folowing evaluation ya mradi. mradi ulianza around June 2006.
  Kimahesabu the first three years zinaelekea ukingoni,though kuna batches nyingine kama mbili hivi zilifuata,sasa hapa ndio tunaweza kuanza kujiuliza maswali,ikiwa already watu wanaambiwa waingie halmashauri vipi kuhusu hawa walioajiriwa 2007 na 2008 ambao hawajamaliza contracts zao kulikoni.
  Pia ninazo taarifa za kuaminika kutoka kwa fellows kuwa hawajaplekewa hela za ku implement activities for months now.Utaratibu ni kuwa wanapelekewa hela kila miezi mitatu for supervision activities etc
  .....nitaendelea kuchangia hasa kumjibu mzalendo halisi ,if this was really an experiment doomed to fail or not?
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Which is which-maoni au ukweli?
   
 16. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ife tena ife kifo cha asili kabisa. Wakati inaanzishwa nilishiriki vile vikao vya awali, nikiwasilisha taasisi moja hivi. Pale tulipinga sana kwani ilionyesha wazi inge shake sana human resource ya Wizara ya Afya. Ni wazi madaktari na manesi lazima wangetimkia kufanya kazi Foundation. Nilichowashauri ni kwamba hata kama short run wanataka hiyo nguvu kazi basi kuwe na mipango ya kusomesha wengine ili waweze ku replace hasa clinical officers na nurses ambao katika establishment ya afya wanahitajika sana. Yule mzungu aliyekuwa amewakilisha hakukubaliana na mimi na wala sikuungwa mkono na uongozi wa wizara.

  Cha kusikitisha hii fund ilingia kwa mgongo wa wizara ya Afya na Dr. Mliga alikuwa yuko mstari wa mbele sana kuhakikisha inapita, ukiachilia mbali Dr. Mwele Malechela akiwa kama mmoja wa task force iliyoundwa. Kwa kitendo hicho nilionyesha moyo wa kishujaa na kukataa kwenda ku facilitate one of the session katika kikao cha maoni ya wadau.

  Mwishowe ilipewa jina La Ben Mkapa Foundation and so madhara wameshayaona. Kwa wakati ule tu Sekta ya afya ilikuwa na upungufu wa specialist, normal doctors, nurses, etc yaani ni mateso makubwa. Tulishauri njia mbalimblai za kunusuru lakini hakuna utekelezaji kwani pale wizarani viongozi wanakimbizania na shilingi za miradi tu. Nashauri mageuzi yafanyike pale Wizarani hasa kile kitengo cha Traininig anachoongoza Dr. Mligah.

  Sina hakika kama ile Human Resource for Health Task force ya Wizara (ina wadau mf. WHO, WB, Unicef, Muhimbil, etc) bado inafanya kazi.

  Ukweli tumeweka mno mbele maslahi binafsi ndiyo maana hatuendelei.
   
 17. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Maane,

  Hiyo ya shilingi kwa maslahi binafsi kuwekwa mbele ya maslahi ya nchi umeongea pointi kubwa sana ya kizalendo!

  Sera tu..serikali itoe sera mpya over incentivisation ya wafanyakazi wake ktk maeneo magumu na siyo experiments za mda mfupi without sustanability strategies!
   
 18. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mzalendohalisi,
  Nilifanya review of Health Workforce Performance. Nikatoa policy recommendations kibao, ikiwemo remuneration, incetives to remote areas, etc. Nilijaribu kwenda hata details ku suggest kind of incetives for general attraction to the health sector na specific kwa remote areas ili hata kule Mtwara na Kigoma wafaidike na huduma za afya. Sijui ile report ilifunikiwa chunguni au kwenye pipa, au tusema iliwekwa kwenye tanuru la moto!!!! Wakati huo ndiyo wanakimbizana na establishment of BMF na miradi mingine mingi ya HIV/AIDS. Nilichoka kabisa. Mkijadili jambo leo mkipeana deadline, yaani hakuna utekelezaji. Utafuatilia kwa simu mwishowe utachoma mafuta we na kupoteza tym yako lakini hakuna kitu.

  Nasema tunahitaji reforms katika utumishi wa UMMA zaidi. Hayo mambo ya OPRAS (Open Performance Review Appraisal System) hayajasaidia kitu chochote kwani wengi bado hawatimizi makubaliano ya mikataba hiyo kati ya mwajiri na mafanyakazi.

  Naona ni vema miradi itengwe kabisa na wizara husika ili zibaki kuwa na ile central role ya formulation of policies, strategies and guidelines. Kazi hii umesahaulika kabisa imebaki kukimbizana na miradi, vikao, semina n.k. Yaani waachie wadau watekeleze sera hizo.
   
 19. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Lakini lazima wafadhili waangalie kuwa within Mkapa foundation kuna watu walikuwa wanapata riziki zao mle nkwa kufanya kazi kwenye foundation, wasjitoe tu kwa sababu Mkapa yuko kwenye list za scandals.
   
 20. m

  msabato masalia Senior Member

  #20
  Feb 23, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Maane,hiyo chenji ilikuwa inatolewa kwa Drs,nurses,lab tech.....waliomaliza internship tuu.Hakuna mtu aliyekuwa ameajiriwa serikalini akaacha ili ahende BMF,wasinge kubali kwani BMF ilikuwa kuvutia vijana ,ndio maana wakasema work for 3 yrs then get absorbrd into the district.Nia ni kwamba vijana wakimaliza intern wasikimbilie Botswana na baada ya miaka mitatu kwasababu utakuwa around 30s then utakuwa ushaanzisha mradi wa nguruwe na kuku hapo kituoni mwisho unaona bora tu ubaki.
   
Loading...