Wadi mpya Muhimbili 'hazina vyoo'!

Wadi mpya Muhimbili 'hazina vyoo'!

Endelea kusubir ww mtoa Mada magufuli aje kujenga choose...Ukiona anakawia anza kujitolea ata mfuko mmoja wa saruji..poor you
 
Akiongea kwa mbwembwe na Wazee wa Dar, rais JPM aliagiza ofisi za taasisi ya afya ya mama na mtoto zibadilishwe matumizi na kuwa wadi za akina mama walioielemea MNH mpaka kulala chini. Cha kusikitisha ni kuwa hakuna huduma nzuri ya vyoo; kwanza havitoshi (mafundi ndiyo wanajenga), havina hadhi ya kutumiwa na akina mama. Wanatumia vyoo vya nje vilivyo mbali na wadi hiyo mpya! Wamejazana kiasi ya wengine kushindwa kuvumilia na kuachia haja (ndogo) pasipo na choo.

Jamani, kuna magonjwa ya mlipuko. Fanyeni hima.

chanzo: EATV

Kuongea kwa mbwembwe maana yake nini?....Halafu kutokuwa na vyoo hilo nalo ni tatizo la kutuletea hapa? Kama hakuna vyoo vitajengwa tu, hiyo siyo issue...
 
Mkuu kipindupindu hicho kinarejea tena kutokea Muhimbili.
Ndio madhara ya mbwembwe hayo. Hivi dunia ya leo ukiona mtu anahamia kwa matambo nyumba yake mpya lakini kumbe haina vyoo anashusha kwenye mifuko ya rambo utamweka kundi gani?
Kipindupindu kikileta fyokofyoko kitaona.
Magufuli yupo atakishughulikia.

Tuendelee kumuombea tu, kwa sababu kutumbua jipu la kipindupindu ni maumivu kweli kweli.
Magu akiamua kutumbua jipu la kipindupindi avae soksi za mikononi (gloves) asifanye utani wake, mikono peku kama ile siku ya usafi wa sherehe za uhuru wa Tanganyika (Tanzania bara)
magufuli..jpg

guf4.jpg
 
Mbona watu wanakuwa ''wakali'' sana wadau wakijadili ''mizuka'' ya Mh. Rais.

Wadau wanajaribu kujadili utekelezaji wa maelekezo ya Mh. Rais na changamoto zake , kitu ambacho ni chanya (positive) sana.

Maana watekelezaji wanaweza kusubiri tamko lingine lije kutoka kwa Mh. Rais kuwa ''waongeze vyoo, viambaza vya wodi mpya ziwezeshe kupitisha wheel-chairs/vitanda vya wagonjwa (wasioweza kujikongoja) kwa urahisi, lift ziwe zinafanya kazi ktk ghorofa wa wodi'', matenki ya maji n.k
 
Raisi wa nchi ana kazi kubwa sana, hasa kubadilisha negativity walizonazo wananchi wengi.
 
Watumishi walikuwa wanajisaidia wapi?ulienda kufanya nini au kuna ndugu yako amelazwa huko lkn ukaona choo ndo muhimu
 
Mijipu inajipendekeza kupitia njia mbali mbali ila jamii inaitolea nje. Kila maamuzi ya haraka lazima yawe na changamoto vyoo ni issue ndogo inayosolvika kulinganisha na mama mjamzito kulala chini

Mambo mengine tusipoonyesha kuridhika hata Mungu atatulaani.
 
Akiongea kwa mbwembwe na Wazee wa Dar, rais JPM aliagiza ofisi za taasisi ya afya ya mama na mtoto zibadilishwe matumizi na kuwa wadi za akina mama walioielemea MNH mpaka kulala chini. Cha kusikitisha ni kuwa hakuna huduma nzuri ya vyoo; kwanza havitoshi (mafundi ndiyo wanajenga), havina hadhi ya kutumiwa na akina mama. Wanatumia vyoo vya nje vilivyo mbali na wadi hiyo mpya! Wamejazana kiasi ya wengine kushindwa kuvumilia na kuachia haja (ndogo) pasipo na choo.

Jamani, kuna magonjwa ya mlipuko. Fanyeni hima.

chanzo: EATV
Mbon heleweki heading unasema hakuna vyoo, ndani vyoo sio vizuri mara unasema mafundi ndio wanajenga, mbona hatukuelewi ndio maana tunasema bavicha upeo wenu mdogo
 
Akiongea kwa mbwembwe na Wazee wa Dar, rais JPM aliagiza ofisi za taasisi ya afya ya mama na mtoto zibadilishwe matumizi na kuwa wadi za akina mama walioielemea MNH mpaka kulala chini. Cha kusikitisha ni kuwa hakuna huduma nzuri ya vyoo; kwanza havitoshi (mafundi ndiyo wanajenga), havina hadhi ya kutumiwa na akina mama. Wanatumia vyoo vya nje vilivyo mbali na wadi hiyo mpya! Wamejazana kiasi ya wengine kushindwa kuvumilia na kuachia haja (ndogo) pasipo na choo.

Jamani, kuna magonjwa ya mlipuko. Fanyeni hima.

chanzo: EATV
 
Niko hapa MNH naangalia pilika zinavyoendelea. Hakuna nurses wa kutosha kuwa Na ward nyingine ghafla. Hawa kina mama wanaweza kupata tatizo wakiwa wenyewe

Kila hospitali inapojengwa huwa inakusudiwa kuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa kadhaa, ambayo huwa inatajwa kwa idadi ya vitanda yaani bed capacity. Huwezo huu ndio huwa unatumika kudesign majengo na kujua idadi ya human power. Sasa ni wazi tu hapa suala la manesi kutosha itakua shida.
Na kama hilo jengo halina choo kabisa basi ni shida kubwa sababu mama aliyetoka kujifungua kumtembeza nje kufuata choo ni mateso, labda kama wamama waliopelekwa huko ni wale ambao watoto wao ndio wanaumwa na mama ni mzima.

Tatizo lililokua linaikabiri hospitali hii ni idadi kubwa ya wagonjwa kuliko hospital capacity, wagonjwa wanaenda wengi mno kuliko idadi ya vitanda, hivyo wengine wanalazimika kulala wawili wawili, na wengine wanalala chini. Sio kwasababu vitanda hamna bali eneo la jengo haliwezi kuwa na vitanda zaidi ya vilivyopo sababu ya designing.

Sasa juzi raisi kachukua jengo la utawala kawapa wagonjwa. Kitalamu hapa hospitali imeongezewa bed capacity, hili kunusuru wagonjwa kulala chini, no doubt hili ni jambo Jema. Lakini je hospitali hii inahitaji kuongezewa bed capacity? Hapana hii hospitali tayari ni kubwa mno, kinachohitajika ni kuziongezea hospitali za karibu huwezo hili wagonjwa wengi watibiwe kwenye hizo hospitali, ikumbukwe hospitali ya Muhimbili ni final referral hospital, ambapo kimsingi wagonjwa wenye shida zilizoshindikana hospitali za chini yake ndo inabidi wapelekwe hapo. Lakini ilivyo sasa, wagonjwa wengi waliopo pale ni wakawaida, ambao walipaswa kutibiwa kwenye hospitali za pembeni.
Mfano mdogo, kuna wakinamama wajawazito huwa wanapelekwa pale kufanyiwa oparesheni kwasababu hospitali walizotoka hakuna uzi wa kushonea, hakuna dawa za usingizi n.k.

Ni vyema kama nchi, lazima tuwe na njia za kimfumo za kutatua matatizo kwa ujumla wake kuliko Kufanya vitu vinavyoleta furaha haraka na ya mda mfupi.
Binafsi huwa napenda approach ya waziri mkuu ya angalau Kuomba maelezo kutoka kwa watendaji kabla ya kufikia maamuzi.
 
Kumbe ujenzi wa vyoo u naendele Sasa wewe Wataka nini?
 
Hivi Pombe asingeenda kumsalimia kiongozi wa Bakwata hapo muhimbili inamaana wale wazazi wangeendelea kulala chini?
 
Akiongea kwa mbwembwe na Wazee wa Dar, rais JPM aliagiza ofisi za taasisi ya afya ya mama na mtoto zibadilishwe matumizi na kuwa wadi za akina mama walioielemea MNH mpaka kulala chini. Cha kusikitisha ni kuwa hakuna huduma nzuri ya vyoo; kwanza havitoshi (mafundi ndiyo wanajenga), havina hadhi ya kutumiwa na akina mama. Wanatumia vyoo vya nje vilivyo mbali na wadi hiyo mpya! Wamejazana kiasi ya wengine kushindwa kuvumilia na kuachia haja (ndogo) pasipo na choo.

Jamani, kuna magonjwa ya mlipuko. Fanyeni hima.

chanzo: EATV
Wao walikua anajisaidia wapi?
 
Pamoja na jitihada za JPM wapinzani wengine hawana hoja ila kunyea kazi nzuri inayofanywa
 
Umesema hazina vyoo na mafundi ndio wanajenga, sasa hapo tatizo liko wapi so watajenga vitaisha na kinamama wataanza kutuma...kumbuka zilikuwa ofisi na sasa zimekuwa wodi huoni lazma kuna mabadiliko yafanyake ili ofisi hizo zifanye kazi mpya, au ulitaka Magu awe kama Mungu aseme na sasa ofisi ziwe wodi na ghafla kila kitu kiwe sawa..
CCM nao sijui wanatumia kiungo gani ktk kufikiri!
Mleta hoja ana kesi ya msingi kaileta!
Ni kweli watu walitakiwa kupisha utanuzi wa wodi, lkn wagonjwa ku-move in haikutakiwa iwe hapohapo!
Lazima vitu kama maliwato na huduma nyingine ziwekwe sawa kabla ya ku accommodate wagonjwa!
Hapakuwa na udharura ktk kuingia, kwa karne nyingi watu wamekuwa wakilala chini, so nini kinachofanya kama hawakuhamia Jana basi dunia ingeisha!
Ujenzi ktk hali ya utulivu unaleta ubora zaidi kuliko hii zima moto!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom