Wadi mpya Muhimbili 'hazina vyoo'!

idoyo

JF-Expert Member
Jan 13, 2013
3,050
1,402
Akiongea kwa mbwembwe na Wazee wa Dar, rais JPM aliagiza ofisi za taasisi ya afya ya mama na mtoto zibadilishwe matumizi na kuwa wadi za akina mama walioielemea MNH mpaka kulala chini.

Cha kusikitisha ni kuwa hakuna huduma nzuri ya vyoo; kwanza havitoshi (mafundi ndiyo wanajenga), havina hadhi ya kutumiwa na akina mama. Wanatumia vyoo vya nje vilivyo mbali na wadi hiyo mpya! Wamejazana kiasi ya wengine kushindwa kuvumilia na kuachia haja (ndogo) pasipo na choo.

Jamani, kuna magonjwa ya mlipuko. Fanyeni hima.

Chanzo: EATV
 
Akiongea kwa mbwembwe na Wazee wa Dar, rais JPM aliagiza ofisi za taasisi ya afya ya mama na mtoto zibadilishwe matumizi na kuwa wadi za akina mama walioielemea MNH mpaka kulala chini. Cha kusikitisha ni kuwa hakuna huduma nzuri ya vyoo; kwanza havitoshi (mafundi ndiyo wanajenga), havina hadhi ya kutumiwa na akina mama. Wanatumia vyoo vya nje vilivyo mbali na wadi hiyo mpya! Wamejazana kiasi ya wengine kushindwa kuvumilia na kuachia haja (ndogo) pasipo na choo.

Jamani, kuna magonjwa ya mlipuko. Fanyeni hima.

chanzo: EATV
Umesema hazina vyoo na mafundi ndio wanajenga, sasa hapo tatizo liko wapi so watajenga vitaisha na kinamama wataanza kutuma...kumbuka zilikuwa ofisi na sasa zimekuwa wodi huoni lazma kuna mabadiliko yafanyake ili ofisi hizo zifanye kazi mpya, au ulitaka Magu awe kama Mungu aseme na sasa ofisi ziwe wodi na ghafla kila kitu kiwe sawa..
 
Kulala chini ktk wodi ambayo ina choo au kulala ktk kitanda safi ktk wodi ambayo iko mbali na choo bora nini????
 
Kama wanavijenga mbona sioni tatizo watumie hivyo hivyo vichache kuliko kurudi kulala chini. Vikikamilika mambo yatakaa sawa.

Eatv na mzee Mengi acheni kumpiga vita rais.
 
Umesema hazina vyoo na mafundi ndio wanajenga, sasa hapo tatizo liko wapi so watajenga vitaisha na kinamama wataanza kutuma...kumbuka zilikuwa ofisi na sasa zimekuwa wodi huoni lazma kuna mabadiliko yafanyake ili ofisi hizo zifanye kazi mpya, au ulitaka Magu awe kama Mungu aseme na sasa ofisi ziwe wodi na ghafla kila kitu kiwe sawa..
Qunfaya yaquun
 
Kama shetani aliweza kukuachia common sense nadhani utafahamu, kipi cha muhimu kati ya viwili, kulala sakafuni ukishea kigodolo na watu wanne kwenye chumba ambacho kina flush toilet au kulala peke yako kwenye kitanda chenye godolo zuri huku mkishea toilet.

Kupambana kihoja na Serikali ya Rais Magufuli lazima kwanza ujivike ujinga au upumbavu kama wewe siyo mpumbavu au mjinga!

Kwa sasa hata wajinga pia wamekuwa watoa ushauri kwa serikali ya Rais Magufuli!

Wapumbavu wameamua kujilipua ili upumbavu wao ufahamike kwa wengi hapa Jamiiforums!

Wengine kwa sasa wanatafuta shule zinazofundisha ujinga ili wakasome na wapate hoja za kuweza kupambana na utendaji wa serikali ya Rais Magufuli!

Awamu hii ya tano tutaona na kusikia mengi!
 
Watu wengine......we jamaa mleta uzi ovyo sana mara havitoshi mara ndo kwanza wanajenga mbona hujielewi
 
Umesema hazina vyoo na mafundi ndio wanajenga, sasa hapo tatizo liko wapi so watajenga vitaisha na kinamama wataanza kutuma...kumbuka zilikuwa ofisi na sasa zimekuwa wodi huoni lazma kuna mabadiliko yafanyake ili ofisi hizo zifanye kazi mpya, au ulitaka Magu awe kama Mungu aseme na sasa ofisi ziwe wodi na ghafla kila kitu kiwe sawa..
wakina mama wanalalamika. tena mmoja kasisistiza, 'maamuzi yawe yanafanyika kwa umakini'
 
Pole Magufuli kwa kazi ngumu ya kuwahudumia watz waliokwisha zoea rushwa ndo wafanye kazi.
 
Akiongea kwa mbwembwe na Wazee wa Dar, rais JPM aliagiza ofisi za taasisi ya afya ya mama na mtoto zibadilishwe matumizi na kuwa wadi za akina mama walioielemea MNH mpaka kulala chini. Cha kusikitisha ni kuwa hakuna huduma nzuri ya vyoo; kwanza havitoshi (mafundi ndiyo wanajenga), havina hadhi ya kutumiwa na akina mama. Wanatumia vyoo vya nje vilivyo mbali na wadi hiyo mpya! Wamejazana kiasi ya wengine kushindwa kuvumilia na kuachia haja (ndogo) pasipo na choo.

Jamani, kuna magonjwa ya mlipuko. Fanyeni hima.

chanzo: EATV

Waliokuwa wanafanya kazi humo walikuwa wanaenda kujisaidia wapi? Lakini kama umesema 'havitoshi' ni jambo jingine maana umesema 'mafundi ndio wanajenga'. Ndio maana ya kuwapa watu changamoto.. ulitaka Magufuli awajengee na vyoo? Yeye katoa agizo ni jukumu la watendaji wengine kuhakikisha agizo la Rais linatekelezwa na linatekelezeka.
 
Tatizo watu sio wabunifu, wanasubiri JPM aje kuwaambia la kufanya.

Watumie vyoo vya muda mfupi wakati ujenzi wa vyoo vya kudumu unaendelea, acheni ugoigoi
 
Kulala chini ktk wodi ambayo ina choo au kulala ktk kitanda safi ktk wodi ambayo iko mbali na choo bora nini????
Mijipu inajipendekeza kupitia njia mbali mbali ila jamii inaitolea nje. Kila maamuzi ya haraka lazima yawe na changamoto vyoo ni issue ndogo inayosolvika kulinganisha na mama mjamzito kulala chini
 
Back
Top Bottom