Yafahamu makundi 3 ya vyombo vya habari

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Gatezi hili kitaaluma linaitwa "Pro government News paper" na lipo kwenye kundi la "Pro government media".
Hili ni kundi la vyombo vya habari ambavyo huandika maudhui ya kuiunga mkono serikali, haviwezi kukosoa hata kama serikali itaonekana kukosea.

Kundi hili huliambii chochote kuhusu serikali iliyopo madarakani, kwake uongo wa serikali ugeuzwa kuwa ukweli, ukweli dhidi ya serikali hugeuzwa kuwa uongo.

Vipo tayari kutumia propaganda yoyote ile ili kuhakikisha kuwa raia wanaamini kuwa serikali ipo sahihi kwa kile ifanyacho hata kama kwenye uhalisia wananchi wanaona jambo fulani ni uongo au halipo sawa.

Ingawaje vyombo hivi sio vyote vinavyomilikiwa na serikali au chama kilichopo madarakani vingine ni vya watu na taasisi binafsi na vinaweza kuwa na maslahi ya namna fulani na mfumo wa serikali iliyopo madarakani.

Kinyume cha kundi hili la vyombo vya habari kuna kundi lingine kinzani ambalo kitaaluma linajukana kama "Ant government Media".

Kundi hili lipo kwa ajili ya kuibua maovu ya serikali, kuishinikiza serikali kufanya mageuzi katika baadhi ya mambo na kuwaamsha raia waione serikali iliyopo madarakani ina madhaifu ambayo yanapaswa kurekebishwa.

Kadhalika kundi hili nalo linaweza kutumia mbinu zile zile muda mwingine kugeuza ukweli wa serikali kuwa uongo, na uongo dhidi ya serikali kuwa ukweli.

Kundi hili la vyombo vya habari pia linaweza kuwa halimilikiwi na vyama vya upinzani bali watu au taasisi zenye mlengo wa kimageuzi.

Kundi la tatu ni kundi la vyombo vya habari vyenye mlengo wa katikati "Neutral Media" visivyo na upande wowote wa kuunga mkono.

Kipaumbele cha vyombo hivi ni ukweli wa habari, huichukua habari katika mizania sawa kwa kila upande kisha kumpelekea mlaji wa habari ikiwa kwenye usawa pasipo kuongeza chumvi, wala kuipamba habari husika.
Vyombo vya habari vya taifa kama vile redio, magazeti, na runinga vinapaswa kuwa katika mlengo huu ili kumpa raia maudhui yenye usawa, haki, ukweli na uhakika yaweze kudumisha umoja wa kitaifa.
Pia kundi hili la linajumuisha vyombo vya watu binafsi na taasisi ambavyo vinafuata misingi ya taaluma ya habari inavyotaka katika kuripoti habari katika mizania sawa "balance".

Mtihani unaobaki ni kwa mlaji wa habari ambaye ni msomaji, mtazamaji na msikilizaji wa vyombo husika kuchagua habari ipi aifuatilie katika chombo gani ili kuiamini na namna gani aweze kuringanisha maudhui ya habari hiyo na ya vyombo vingine ili kupata uhalisia.

Peter Mwaihola
IMG_17059099041313819.jpg
 
Back
Top Bottom