Wadau washauri Hamas na Israel kusimamisha vita kupisha mechi ya Simba Vs Al Ahly Oktoba 20, 2023

Sultan MackJoe Khalifa

JF-Expert Member
Nov 24, 2022
5,525
11,319
Tukio kubwa la ufunguzi la soka la kihistoria African football League ambalo ufunguzi wake utafanyika uwanja wa Mkapa Tanzania Oktoba 20, 2023.

Tukio hilo kubwa la michuano mikubwa kuliko yote Africa ambalo litakua na ugeni mzito wa Rais wa FIFA, Rais wa CAF pamoja na marais wa vyama vingine vya soka kutoka nchi mbalimbali.

Wadau mbalimbali wa soka wameshauri machafuko yanayoendelea maeneo mbalimbali Duniani, kuanzia Congo, Ukraine pamoja na Hamas na Israel wasitishe vita ili kutoa nafasi ya kufatilia ufunguzi wa michuano hii mikubwa ambapo timu kubwa Tanzania Simba sports club itamenyana na Club ya Al ahly kutoka nchini Misri.

Mungu endelea kuiweka Simba kwenye mkono wako wa kulia, aamin!
 
Kuna jamaa yangu alinyimwa kadi ya Simba kwa sababu hakuwa na kigezo cha Umbumbumbu.
 
Yes, na Club zingine ndogo ndogo wakiongozwa na Uto ni lazima wawe watulivu, kukaa kwa kutulia ili kujifunza namna pira linavyotakiwa kuchezwa kwa kiwango cha kimataifa. Pale hamna IHEFU.
 
Back
Top Bottom