Mechi ya Simba vs Al Ahly kuangukia Ijumaa Kuu ya Pasaka ina maana kubwa sana kiroho

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,129
7,896
Ijumaa hii ya 29/03, Simba anacheza na Al Ahly ya Misri katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya CAFCL. Ijumaa hiyo hiyo ni mwanzo wa maadhimisho ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo. Kuna mfanano mkubwa kati ya sikukuu ya Wayahudi inayoitwa Passover na sikukuu ya Wakristo ya Pasaka. Sitaenda deep sana kuelezea mfanano huo ila unaweza kugugo kama umevutiwa na mada hiyo.

Passover ni sikukuu ya maadhimisho ya Wayahudi kutoka katika utumwa baada ya miaka 400. Namba 4 imetajwatajwa sana hivi karibuni na wanajimu na wazee mbalimbali wa Simba. Kuna wanaokumbushia 1974 Simba walipoingia kwa mara ya kwanza nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika na huu ni mwaka 2024, miaka 50 kamili ikiwa imetimia. Pentekoste, tukio lingine muhimu sana katika Ukristo lilitokea siku 50 baada ya kufukuka kwa Yesu Kristo, tukio ambalo nalo linaadhimishwa siku 50 baada ya Pasaka. Maandiko pia yanasema kabla ya kukamatwa na kusulubiwa, Yesu alikwenda mlimani akafunga kwa siku 40, usiku na mchana na akashinda jaribio la shetani. Angalia hizi namba ninazoorodhesha kwa umakini sana na umuhimu wa matukio haya.

Kwa maana hiyo Ijumaa ya Pasaka na Passover ni siku ya matumaini. Ni siku ambayo Wayahudi walianza kushuhudia Unabii wa ukombozi wao ukienda kutimia. Ni siku waliyotazamia Ukombozi wao. Kwa Wakristo pia ni siku waliyotegemea Ufalme wa Mungu ukienda kudhihirishwa.

Jumamosi ya Pasaka na Passover, hizi ni siku za hofu. Wayahudi walikuwa wameshatoka katika nyumba zao wakikimbia majeshi ya Farao yaliyokuwa yanawafuata nyuma. Kwa wafuasi wa Yesu walishuhudia Ukimya wa Mwenyezi Mungu. Jumamosi ya Pasaka inajulikana kama ni siku ya ukimya na upweke.

Kwa kumalizia, wakati Wayahudi waliongozwa na Nabii Musa, Simba wana mchezaji kipenzi cha mashabiki wengi, Musa Phiri aliyetolewa kwa mkopo.

Nyongeza: Simba inahitaji mabadiliko makubwa ya kiuongozi na kiutawala ili ifike nchi ya ahadi!
 
Kwa mujibu wa majira ya wasabato na waislam, siku hubadilika pale jua linapozama. Ndio maana Sabato huwa inaanza Ijumaa baada ya jua kuzama. Hivyo kwavile mechi ya Simba inachezwa saa tatu usiku, hiyo mechi inachezwa ndani ya siku nyingine ambayo ni Jumamosi.
 
na hata hizo siku zinatofautiana kila zinapokuja, usifikiri jumamosi hiyo ya simba anayocheza itafananana na jumamosi zingine, japo zote ni j mosi ila kuna viji tofauti vidogo sana vinajitokeza.

sijui niendelee?
 
Zianishe hizo viji tofauti hivyo
 
kinajimu mechi ya simba inachezwa jumamosi, na Yanga anacheza jumapili.

sijui niendelee?

Kwa mujibu wa majira ya wasabato na waislam, siku hubadilika pale jua linapozama. Ndio maana Sabato huwa inaanza Ijumaa baada ya jua kuzama. Hivyo kwavile mechi ya Simba inachezwa saa tatu usiku, hiyo mechi inachezwa ndani ya siku nyingine ambayo ni Jumamosi.
Utaratibu na kalenda ya sasa unatambua siku inaanza na kuisha muda gani?
 
Kwa kumalizia, wakati Wayahudi waliongozwa na Nabii Musa, Simba wana mchezaji kipenzi cha mashabiki wengi, Musa Phiri aliyetolewa kwa mkopo. Nyongeza: Simba inahitaji mabadiliko makubwa ya kiuongozi na kiutawala ili ifike nchi ya ahadi!
Hii Ijumaa Kuu ipo kwa Simba tu au hata kwa Al Ahly? Wao wana Moses nani?
 
Hii Ijumaa Kuu ipo kwa Simba tu au hata kwa Al Ahly? Wao wana Moses nani?
Al Ahly wanawakilisha kizazi cha Farao. Musa yuko upande wa pili. Pia Al Ahly wanajiita shetani, nimeacha vitu vingi sana maana watu hawapendi kusoma mada ndefu
 
Back
Top Bottom