Mkuu Mkorosho, kilichofanyika ni kitu kinaitwa harmonisation ili mifuko yote itumie standard formulat kukokotoa mafao!. Kabla ya hapo Watumishi waserikali kuu kupitia PSPF na Watumishi wa serikali za mitaa kupitia LAPF ndio wenyewe walikuwa walipwa mafao manono, wakati mifuko ya PPF, NSSF na GEPF wao walitoa mafao kiduchu!. Kwa LAPF na PSPF, mtuymishi alikuwa anakatwa 5% ya mshahara wake na mwajiri anamchangia 15%, jumla ni 20%, mwisho wa siku, anavuta bulungutu la ajabu. Mifuko mingine, mfanyakazi anakatwa 10% na mwajiri anachangia 10%, ila kutokana na kikokotoo kupishana, wastaafu wa NSSF, PPF na GEPF ended up with peanut, huku wenzao wa PSPF na LAPF wakitoka na fungu nene, nono!.
Ujio wa mamlaka ya udhibiti mifuko ya hifadhi za jamii, SSRA, ikaamua ku harmonise, kikokotoo kimoja kwa mifuko yote na mafao yanayolingana kwa wote, hivyo waathirika wakubwa wangekuwa wanachama wa LAPF na PSPF mafao manono yao yangeshuka, huko NSSF, PPF na GEPF kiwango kitapanda!.
Kwa vile sheria hii itawahusu wanachama wapya tuu!, you can never miss what you never had!.
Pasco.