. Mkuu Chalinze, umrsema ukweli kabisa, kwenye website ya CCM inaonyesha wana wanachama 6,000,000. Ndani ya hesabu hiyo, na mimi nimo, maana nilipopita JKT niliingizwa kwa lazima, ila amini usiamini, hiyo kadi ya chama sikuwahi kuichukua, kuilipia!, wala kuitolea machango wowote, ndio maana chama kinachojitapa kina wanachama milioni 6!, kisha mgombea wa CCM anakuja kushinda urais kwa kura milioni 5 tuu!.
Tena ni afadhali yangu!, kkuna mwanachama fulani maarufu sana wa CCM, yeye amejiunga upinzani, ila kadi yake ya CCM hakuirudisha kama wafanyavyo wengi wanaiongia upinzani, yeye kaitunza vizuri sandukuni!, kwa maelezo ni "kumbukumbu", na huku nyuma wamejitokeza wasamaria na kuilipia hadi 2015!, ili wamsubirie tuu, akijaza fomu kugombea, pingamizi litapelekwa Tume ya uchaguzi, kumthibitisha ni mwanachama wao, na uthibitisho wa malipo wenye jina lake!.
Pasco.