Habari humu.
Kichwa cha habari chahusika.Sioni shamrashamra za hii sikukuu pia hata matangazo sisikii.Je inawezekana na mwaka huu maonesho yakapotezewa na ukizingatia kuna kazi ya sensa na makazi.
Ni maonesho muhimu sana kwa wakulima na wafugaji na huwa yanatoa fursa kubwa za kibiashara kwa watu wengi kutoka sehemu mbalimbali.
Mwaka jana kulikuwa na sababu zilitolewa za kutofanyika kwa maonesho haya sasa sijui mwaka huu.
Kilimo ndio sehemu ya ajira kwa watanzania wengi milioni 60 na zaidi sasa itakuwa kitu cha ajabu kutoyawekea umuhimu haya maonesho.
Naona kama kuna danadana kuhusu kitu hiki muhimu
Nchi yetu haina uwezo wa kutoa ajira kwa watu wake wengi hatuna viwanda vya kutosha na vingi vimekufa hivyo kilimo ndio kiwanda pekee kilichobaki cha kutoa ajira kwa wananchi walio wengi.
Nchi za ulaya na asia zinajivunia uwezo wao wa viwanda vingi vya uzalishaji na kupunguza tatizo la ajira tofauti na nchi zetu za kiafrika vijana hawana kazi wasomi wanazunguka na bahasha kutwa.. panya rodi mtaani wanaibuka kila siku hii ni kutokana na kutokuwa na ajira na kazi ambazo zinatokanana viwanda vya uzalishaji bidhaa.
Juzi nimesikia kuna kiwanda cha sukari cha mfanyabiashara mmoja kinatarajia kufunguliwa ni taarifa nzuri hiyo kwa taifa letu vijana watapata ajira kwa kiasi angalau ingawa bado tatizo ni kubwa.
Hayati JPM alisisitisa sana suala la viwanda aliona umuhimu wake kwa watanzania basi serikali nayo isisitize suala la kilimo kama ajira ya watu wengi naona kama hakuna nguvu kubwa huku.