Maonesho ya Nanenane jijini Mwanza ni kituko cha karne

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,332
Kufuatia maadhimisho ya sherehe ya wakulima almaarufu Nanenane kufana nchini, nami nikapata wasaha wa kuzuru kunako viwanja vya sherehe hizo jijini Mwanza katika eneo la Nyamhongolo kushuhudia ni namna gani kuna mwamko wa wadau na walengwa(wakulima) pamoja na wananchi kiujumla kuhusiana na sherehe hizi katika ukanda huu wa ziwa Victoria.

Shauku yangu ni kutaka kuzuru hapa kwa ajili ya kujifunza na kupata taarifa zitakazonisaidia kujua wapi nitapata kile ninachokitarajia kukipata kupitia maonesho haya.

Njiani napishana na kina mama na kina baba wanaoongozana na watoto wao wakiwa na nyuso zilizojaa furaha na bashasha wengine wakiwa wamebebelea bidhaa wanazoenda kuuza au aidha wametoka kununua, watoto wanaonekana wamedamshi na wanamung'unya peremende huku wazazi pia siyo haba baadhi wamevunja kabati kwa kiasi chake bila shaka wanaelekea au kutoka ninapoelekea pia kama sikosei wazo langu la kuja huku nikiwa kama kijana mfua uji sidhani kama ntalijutia.

Paaar mpaka Makka! Hatimaye safari yangu inanifikisha katika eneo la maonesho, ghafla ile hamu na ghamu inayeyuka kama pande la barafu kwenye jua la alasiri, kidogo nashikwa na butwaa nakuduwaa nikijiuliza hiki kilichopo mbele yangu ni MAONESHO au MNADA?

Baada ya kuchunguza kidogo nabaini kuwa hapa hamna cha geti wala kiingilio, bali nikujipenyeza tu ilimradi usikanyage biashara ya mtu maana eneo halina mpangilio kila mtu kujiamulia tu anavyoona inafaa kiufupi ni changanyikeni, kwa hapo kimoyomoyo nawasifu na kuwapongeza mamlaka ya eneo husika kwa kupoteza mapato na kunipendelea mzururaji wao mwema.

Nikiwa nasonga mbele nabaini kuwa robo tatu ya eneo zima la maonesho limetamalaki Mnada wa nguo, samani za ndani, mabanda ya chakula na vinywaji (baa nyingi maarufu zimehamishia biashara zao hapa), promosheni za vinywaji na mitandao ya simu inaendelea n.k

Lakini kwa mbali kabisa nikiwa naelekea kukata tamaa ya kile kilichonileta katika maonesho haya kukishuhudia ndipo nabaini uwepo wa mabanda machache kadhaa ya taasisi za umma, binafsi na makampuni kadhaa yaliyotambua umuhimu wa sherehe hizi nakuamua kushiriki kutoa elimu, kujitangaza na kufanya mauzo ya bidhaa zao.

Jicho langu kama mwewe linasurvey kwa haraka na kubaini kuwa sekta ya kilimo ambao ndiyo walengwa haswaa wa shughuli wamejitahidi na kongole kwao, ila kinachonisikitisha ni mwamko wa sekta zingine muhimu katika ukanda huu.

Mfano KUKOSEKANA kwa sekta ya UTALII (hakuna banda la utalii lolote, hakuna banda la hoteli hata moja,hakuna watu wa airport,hakuna bidhaa za kitalii,n.k) licha ya mwanza kuzungukwa na vivutio chungu nzima.

Sekta ya MADINI nayo kibla hamna cha banda la maonesho ya madini, wala vito, wala banda la taarifa kuhusiana na madini, licha ya ukanda huu kuwa kinara wa machimbo ya dhahabu na almasi.

Kukosekana kwa banda lolote la asasi za kiraia au NGOs kwa mkoa kama huu unaoongoza kwa utitiri wa mashirika haya ya kijamii ni zaidi ya dharau kwa watanzania na mamlaka pia.

Kongole kwa vyuo viwili pekee vya afya tena vile vidogo vilivyoshiriki na kutoa elimu na vipimo vya afya bure kwa watu wote hasa vijana. Kinyume na hapo hakuna chuo chochote kilichojiangaisha kupeleka banda lake katika maonesho haya licha ya umuhimu wa taarifa na kujitangaza katika kipindi hiki cha udahili ambapo wanafunzi wanahitaji taarifa sahihi juu ya vyuo,uchaguzi wa kozi, ada n.k,

Hakuna banda la kiwanda chochote kile isipokuwa wameleta bidhaa zao kwa walaji na siyo maonesho, sekta zinazoongoza kwa kero hakina MWAUWASA, TARURA, TANESCO hawapo hapa kusikiliza na kutatua kero au kuelimisha wateja wao juu ya huduma zao licha ya kwamba wanajua fika kuwa wanahitajika matokeo yake wamemwachia shughuli yote BOT ajinafasi.

Kufuatia uwepo wa mapungufu lukuki katika maonesho haya na kukosekana kwa dhana nzima ya maonesho, wapare wanakwambia "when in tanzagiza do as Sukuma.." sikupoteza muda nikatoa zangu mia mbili mfukoni nikaitisha boda ya baiskeli pasipo kujivunga nikanunua muwa wa 500 huku natafuna nasindikizia na togwa, wakulugwa asikwambie mtu sherehe ilifana sana huku dereva akinogesha safari na kiredio chake alichoning'iniza shingoni akikanyagia pedeli na mluzi kufuatisha mdundo wa muziki toka kwa manguli kina budagala na best nasso hakika ilikuwa ni unforgettable experience.

Nanenane Oyeeh!! kimasihara naona boya la Sisemu kwenye V eite linapunga, nikamdere tu jinsi alivyo-punga!
 
Nanenane Oyeeh!! kimasihara naona boya la Sisemu kwenye V eite linapunga, nikamdere tu jinsi alivyo-punga!
emoji23.png
Nani huyo anauza Mpunga?
 
Nane nane bora nchi hii ni KANDA YA KASKAZINI.
hii kila mwaka utafikiri ni ya kimataifa.

Zana za kilimo na tech..za kutosha.
Mashirika mengi na makampuni hushiriki.
Mpangilio wa mabanda.
Sehemu za starehe kwa kweli hutajuta kwenda
 
Mwanza inaelekea kuwa kama bukoba. In short imetengwa kiaina na serikali. Sherehe kubwa kama hizi wasukuma na wakuria kuzigeuza gulio LA uchinga ni kosa kubwa.
Kadri siku zinavyoenda mwanza inakosa mvuto na ubunifu.

Ujenzi holela bila mpangilio,
Uchafu kila kona
Joto Kali na mama ntilie kila kona vinaikosesha mwanza heshima.
 
Hapo kwenye kutengwa na serikali ndio penyewe.Ukitaka kuamini hilo angalia hizi taarifa za habari local kuna mikoa kuanzia jtatu mpaka jpili inatajwa tu mara miradi,mara semina,mara fidia,mara wageni ila rock city ikitajwa tu jua ni mauaji au ajali ( mchawi serikali).Ila tutasonga hivyo hivyo kibishi.
 
Yaani mkuu hata Mimi nahisi serikali kuu inasabotage kwa makusudi maendeleo ya kanda ya ziwa. Juzi rais akiwa simba day akaahidi kuviboresha viwanja vya mpira. Akataja kiwanja cha arusha na Dodoma, eti kirumba haimo...!!!

Rais samia na serikali yake ameitenga sana kanda ya ziwa. Mwanza miradi inayoendelea ni aliyoiacha magufuli.

Serikali kuitenga Mwanza ni kosa kubwa.
 
  • Thanks
Reactions: EEX

Na hii ni imekuwa ni kwa miaka.Jiji linazubaa tu lakini miji mingine heka heka kila siku mara wageni,mara mikutano,semina,misaada ,ujenzi.Tutafika tu.Mzee Magu aliliona hili akaitwa mkabila.
 
Mwanza inaelekea kuwa kama bukoba. In short imetengwa kiaina na serikali. Sherehe kubwa kama hizi wasukuma na wakuria kuzigeuza gulio LA uchinga ni kosa kubwa.
Kadri siku zinavyoenda mwanza inakosa mvuto na ubunifu.

Ujenzi holela bila mpangilio,
Uchafu kila kona
Joto Kali na mama ntilie kila kona vinaikosesha mwanza heshima.
Mikdde
 
Back
Top Bottom