Hii haswaa ndiyo ukweli wenyewe na ndio maana kuna watu hata huko CCM wanaoeleweka kwa misimamo wanaogopa kuwa wazi kupinga malipo haya simply b'coz inaweza kuwa interprated ni kumpinga JK. Na hii pia inatuthibitishia kwamba JK ni dikteta huko kwenye vikao vyake na likely ni mtu wa visasi kama ilivyowahi kusemwa huko nyuma.
Nyambala, nakubaliana na wewe kwa kiasi. Kuwa mtu wa msimamo ni strength of character kusimamia kile unachoamini no matter what, kama walivyofanya Sitta na Dr. Mwakiembe. Sasa hao unaowaita wana misimamo lakini wanaogopa kumpinga JK kwa kuhofia visasi, ndio msimamo gani huo?!. Huu ni udhaifu, weakness na unafiki wa kisiasa kumuunga mkono mdomoni kwa kitu usichokiamini moyoni.
Niliufuatilia mjadala wa Richmond bungeni mwanzo hadi mwisho, nikakumbuka jinsi watu kama kina Ole Sendeka, Anne Kilango, Selelii na wale waliojiita makananda dhidi ya ufisadi walivyojipambanua kwa michango yao moto na yenye ncha kali na makali kama ya upanga wa makali kuwili!.
Lakini ile e siku Sitta anauhitimisha rasmi mjadala ule pale Bungeni, sikuamini hao makamanda walivyonywea kama vifaranga vya kuku vilivyo lowa maji! na Ole Sendeka aliposimama kuchangia nikajua huyu ndie mwanamume wa shoka, Morani wa Kimasai hawezi kukubali kufa kibudu, nikijua atatoa msimamo wa kupinga mambo hayawezi kumalizwa kirahisi hivyo, lakini alipochangia tuu ndipi alinichosha na kuniacha hoi kabisa alipounga mkono hoja!.
ilicomment humu humu kuwa ule ulikuwa ni utumbo mkubwa zaidi heri wenzake walioamua kujinyanazia kimya. Nilikumbushia lile swali la Mzee Mwanakijiji " Makamanda walioko CCM, wanapigania nini?".
Kwa misimamo hiyo kana wa Ole Sendeka, ndipo nikaelewa pia kuna wabunge machachari, kelele nyingi kumbe ni debe tupu tuu!.
Baada ya mbwembwe zote mle bungeni kwenye suala hili mbona wote wamenywea na kubaki Sitta tuu na Mwakiembe?!, ndio maana nasema, ukiondoa wachache wenye msimamo, wengi wa wabunge wa CCM hawana msimamo ni wanafiki tuu na waganga njaa kwa lengo la kichumia tumbo!.