Kwa kweli siku hizi siwaelewi CCM wanavyoendesha mambo yao they are not systematic as it was used to be.
Hawawezi kuwa systematic kwa kuwa kila mtu anapalilia mraba wake, na wao pia wanasoma alama za nyakati.
Wapo wanajenga hoja kwa kuangalia Urais wa 2015 na Ubunge wa 2015.
Wapo wanaotetea malipo kwa kuwa walibebwa na mafisadi kwenye mbio za kuingia mjengoni kwenye uchaguzi wa 2010. Lakini hata ukiwa na mahela kiasi gani, bado huwezi kupambana na nguvu ya umma ambayo imepewa elimu ya uraia na imeelewa adui yao ni nani.
Ndiyo maana kila mtu anakuja na tamko la kivyake. Nape Nnaye anasema haamini kama lile tamko alilotoa Chiligati lilikuwa ni la CC anayoifahamu yeye, anahisi labda Bob Chiligati alijitengenezea version yake. Kwa lugha nyepesi ni kwamba Nape ametofautiana na CC.
UVCCM wanasema serikali isilipe mpaka kwanza RICHMOND ajulikane ni nani na ikiwezekana ashitakiwe.
Mwakyembe/Sitta wanasema hakuna kuilipa Dowans, kampuni ambayo ni ya kitapeli.
Wabunge wa CCM wanasema ikiwezekana serikali isikubali kulipa na watafute njia za kisheria za kumaliza kadhia hiyo.
Jumuisho: Kikwete ndio kinara wa hilo zigo la Dowans, maana hana mashaka ya kujipendekeza kwa wapiga kura kwa kuwa anajua huu ni muhula wake wa mwisho, so hata CCM ikipoteza uchaguzi wa 2015, yeye hatakuwepo. JK ndio Rais, Ngereja na Werema wasingekuja na kauli zao bila ya baraka za Ikulu. Pia JK ni mwenyekiti wa CC, kwa hiyo CC isingekuja na kauli ile ambayo inachimba kaburi la CCM na huku wakiona wazi kwamba wananchi hawataki kusikia habari hizo.
Tumshukuru Kikwete kwa kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM, maana ametusaidia sana kuimrisha upinzani na pia kuimaliza CCM. Ile ndoto kwamba CCM inaweza kutawala kwa miaka 100 ijayo, inapotea taratibu na sasa life span ya CCM inazidi kuwa fupi sana.