Wadau: Dowans imechimbia kaburi CCM

Wadau: Dowans imechimbia kaburi CCM

Mzee The Finest, hoja kama hii ilihitajika imeshatekelezwa tangu majuzi Tanzania.
 
Mzee The Finest, hoja kama hii ilihitajika imeshatekelezwa tangu majuzi Tanzania.

Ngoja kikao cha Bunge kinachoaanza Februari 8 yatakayojitokeza huko ni makubwa zaidi, nafikiri hii ishu isingekuwa kubwa kama ingepita kwenye Bunge, sasa walipokosea ni pale walipoipitisha nje ya Bunge tena wakitaka ilipwe fasta fasta wewe uliishawahi kuona nchi gani inalipa deni haraka haraka hata marekani ambaye ni mdeni namba mmoja huwa hawi na spidi ya kulipa deni kama tulivyo kwenye Dowans.

Kama wana haraka ya kuwalipa Dowans basi wawalipe kwanza wastaafu wa EAC, walimu wanaodai malimbikizi yao ya mishahara, halafu wakimaliza waje wawalipe wananchi fidia ambayo wanaidai Serikali, mbona deni ambalo walikuwa wanadaiwa na Brazil walipokopa kwao kujenga barabara ya Dar- Dodoma hadi leo hii walikuwa hawajalipa mpaka tumesamehewa deni baada ya Rais wa Brazil kuja hapa nchini
 
Bila maandamano nchi nzima kushinikiza JK na genge lake la mafisadi kuachia ngazi au Bunge kuwafungashia virago vyao ....................we are doomed.....................
 
Bila kuingia barabarani hawa watu watatufilisi. likipita la Do-Ones watakuja na ishu nyingine na safari hiyo watachote mihela mingi kuzidi hii, si wameshaona wadanganyika hawana lolote...!
 
Nadhani ubashiri wangu kuwa hili Dowans litaiyumbisha nchi unatimia kama JK hajatoa msimamo wake nadhani 2011 itakuwa mwaka mgumu kwake kiutawala.
 
Nadhani ubashiri wangu kuwa hili Dowans litaiyumbisha nchi unatimia kama JK hajatoa msimamo wake nadhani 2011 itakuwa mwaka mgumu kwake kiutawala.

Atatoa vipi msimamo wake wakati kamati ya CC chini ya Uenyekiti wake umeidhinisha Dowans walipwe hapa hakuna la zaidi ila kuishinikiza Serikali iliyopo madarakani kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nayo
 
Bila kuingia barabarani hawa watu watatufilisi. likipita la Do-Ones watakuja na ishu nyingine na safari hiyo watachote mihela mingi kuzidi hii, si wameshaona wadanganyika hawana lolote...!

If only i was a sniper unatafuta mmoja baada ya mwingine unawadungua maana hicho ndicho kilichobaki tumeishachoka aarrghhhh!!!!!!
 
Natamani sana kuwepo kwenye mazishi ya CCM 2015, kwani naamini kabisa kuwa tutakizika 2015.
 
Atatoa vipi msimamo wake wakati kamati ya CC chini ya Uenyekiti wake umeidhinisha Dowans walipwe hapa hakuna la zaidi ila kuishinikiza Serikali iliyopo madarakani kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nayo

Lakini yeye ni rais ana executive powers ni vema akatafakari vizuri hili swala kwani sio la kubeza.
 
Nadhani ubashiri wangu kuwa hili Dowans litaiyumbisha nchi unatimia kama JK hajatoa msimamo wake nadhani 2011 itakuwa mwaka mgumu kwake kiutawala.

Msimamo gani unaoungoja kutoka kwa the most hopeless president ever wakati yeye ndio alikuwa mwenyekiti wa kamati ambayo maazimio yake ni ule upupu aliousoma yule mzee anayezeeka viba\ya chiligati? Payee wa hiyo 94b ni mmoja wa wajumbe wa kamati kuu, did you expect something different? Then basi tumerogwa wote maskini.
 
Mkuu sikatai yeye ni mwenyekiti wa ile kamati na kukaa kwake kimya kunamaanisha amekubaliana na maamuzi ya kamati yake. Ila vilevile usisahau yeye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa akikaa kimya tutaelewa Rais amekubaliana na msimamo wa chama chake hivyo basi nadhani ni wakati muafaka wananchi waamke kupinga hilo.
 
Mtikila apongeza UV-CCM kuhusu Dowans

Na Grace Michael
Majira

MWENYEKITI wa Democratic Party, Mchungaji Christopher Mtikila amesema kuwa kitendo cha ujasiri kilichofanywa na Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) cha kupinga kulipwa kwa mabilioni ya fedha kwa Dowans kiwe daraja kwa Watanzania wote katika kuhakikisha fedha hizo hazilipwi.

Mbali na hilo, pia amewataka Watanzania kutoogopa kupinga suala hilo kwa kuwa hakuna sheria yoyote inayoweza kuwabana wakati wa kudai maslahi ya taifa na haki za Watanzania.

Mchungaji Mtikila aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hukumu ya fidia ya sh bilioni 94 za Watanzania kwa Dowans, kitendo ambacho alisema ni 'uporaji wa nchi kwa bastola ya Dowans'.

UVCCM wanapaswa kupongezwa kwa kile walichokifanya kwa kuwa wanawakilisha mawazo ya Watanzania wazalendo, hivyo tukitumie kitendo hicho kama daraja muhimu la kutuunganisha sisi wana wa Tanganyika katika vita ya ukombozi ili kuangamiza magenge ya uporaji wan chi yetu,” alisema Mchungaji Mtikila.

Alhamisi iliyopita, UV-CCM ilitoa msimamo wake kuwa Dowans wasilipwe fedha na serikali, bali waisaidie kuipata kampuni ya Richmond iliyohamishia mkataba wake ili iwalipe fedha hizo.

Vijana hao walipendekeza suala la Dowans lirejeshwe bungeni kwa majadiliano zaidi, ili kuchukua hatua dhidi ya yeyote aliyehusika na madudu hayo.

Alisema kuwa wananchi wanapoamua kulinda maslahi ya taifa lao huwa hawafungwi na sheria kwa kuwa sheria ni chombo kinachoweza kutumiwa kwa ajili ya kudhulumu haki au kutoa haki, hivyo katika mapambano ya haki sheria hukaa pembeni.

Alisema kuwa ibara ya 27(2) inataka wazawa wa nchi kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa, hivyo akawataka wananchi kujiuliza Dowans inaiuzia bidhaa gani taifa kwa hayo mabilioni ya fedha.

Uzalendo tunaolazimishwa na katiba ni kuipuuza mahakama ya kimataifa na kuwashughulikia waliohusika na uporaji kuanzia wa IPTL, SONGAS, AGGREKO, DCP, EPA, Kagoda Agriculture Ltd, hujuma za mitandao ya simu za mikononi, alisema.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa umefika wakati kwa Watanzania 'kuhamia barabarani kama familia moja' kwa ajili ya kuondoa utawala uliopo kwa kuwa unadidimiza haki za wananchi.

Alisema kuwa Dowans italeta ukombozi katika nchi hii kwa kuwa hata Rais Jakaya Kikwete anahusika kwani alipotuhumiwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa hakuweza kukanusha tuhuma hizo.
 
Yani hii serikali ya ccm!! We subiri tu dawa yao iko jikoni.wa@+&%*se¡¡¿ng"=e sana hawa.
 
DOWANS KABURI LA DHAHABU KWA CCM NA MAFISADI WAKE WOTE:

Kwa maoni yangu: Dowansi ni KABURI LA DHAHABU kwa CCM na Mafisadi wote nchini lililoletwa na Mwenyezi Mungu kutuokaa jumla Watanzania baada kusikia kilio chetu cha dhati dhidi ya dhuluma nyingi chini kwa miaka mingi.

Jamani kweli Mungu yupo, hasinzii wala hapuuzi hata sauti zetu sie akina Matonya wa ulimwengu huu!!!

Watanzania, Mungu yupo na anatupenda sanaaa hivyo tuache kumkasirisha kila mara kwa kukubali mtu kutugawanya kwa misingi ya imani zetu!!!
 
Hivi hawa wazee si ndio wale walioitwa Dimond Jubilee na kujipachika cheo cha wazee wa D'salaam siku mkwere alipokuwa anamnanga mgaya au sio hao?????
Tatzo lao wakiambiwa wachague siment na bati kwa bei ya Ts. 5000 hawataki wanaogopa vita....wajifunze kuwa ssim ni genge la wahuni na ssm ile ya Mwalimu ilishakufa tangu octoba 1999. Chini ya serikali hii ambayo wengi waliichagua wasitegemee chchte
 
hawa wazee walikuwa wafanyakazi wa EAC,achana na wale wanywaji kahawa wa mitaa ya twiga na jangwani.
 
Je DOWANS wasipolipwa, CCM itakufa?

CCM watapata wapi pesa za kuangamiza upinzani?

CCM itapata wapi pesa za kuwanunua baadhi ya Viongozi wa Upinzani ili kudhoofisha upinzani?
 
Back
Top Bottom