Wadau: Dowans imechimbia kaburi CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau: Dowans imechimbia kaburi CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 23, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,308
  Likes Received: 418,592
  Trophy Points: 280
  Wadau: Dowans imechimbia kaburi CCM
  Saturday, 22 January 2011 20:24

  Waandishi wetu

  SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya CCM kubariki kampuni ya Dowans kulipwa na serikali, wasomi, wanasiasa wa watu kada mbalimbali, wamelaani hatua hiyo na kusema chama hicho kimeasaliti Watanzania.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wananchi hao walisema tofauti ya msimamo kuhusu Dowans, kati ya CC na UVCCM, ni ishara tosha kuwa malipo hayo yana utata mkubwa na kwamba yanahitaji ufafanuzi wa kina kabla ya kutolewa.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),Dk Bashiru Ally alisema tafauti hiyo ya msimamo inaonyesha kuwa ndani CCM hakuna uelewano na kwamba malipo hayo yakifanyika chama hicho kitabanwa na wananchi.

  “Kimsingi nakubaliana na tamko la vijana wa CCM kuhusu Dowans pamoja na Bodi ya Mikopo ambayo tayari Rais Kikwete ameshaiundia kamati, lakini walichoamua Kamati Kuu ndio msimamo wa Serikali kwani zaidi ya asilimia sitini ya wajumbe wa mkutano huo ni mawaziri na mwenyekiti wao ni Rais,” alisema Dk Ally.

  Alisema ingawa deni hilo litalipwa, CCM ijiandae na hasira za wananchi ambazo zitakishukia chama hicho siku za usoni.

  Dk Ally ambaye ni mtaalamu wa Sayansi ya Siasa alisema msuguano ulioonyeshwa na Kamati Kuu ya CCM, UVCCM na baadhi ya mawaziri katika sakata hilo, inaashiria hata kwenye kikao cha kamati hiyo wajumbe hawakuafikiana kuhusu hukumu hiyo.

  Mfanyabiashara wa Arusha, Evance Mremi, alisema kitendo cha CCM kukubali kuilipa Dowans ni udanganyifu unaofanywa na watu wasiolitakia mema taifa.

  Mremi alieleza kuwa kilichofanywa na CCM, kimekwenda kinyume na matarajio ya wananchi wengi na kwamba kitendo hicho kinaashiria kuwa nchi iko kwenye utawala wa kijeshi.

  “Watanzania hatupendi kulipa deni hilo linaloonekana wazi ni la udanganyifu, hawa wanaotulazimisha, wana maslahi nalo kwa kuwa hayo si matakwa ya Watanzania,” alisema mfanyabiashara hiyu.

  Mbeya

  Mwenyekiti wa mstaafu wa CCM mkoani Mbeya, Allan Mwaigaga alisema kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM kuhusu suala la Dowansa ambao umezaa makundi mawili yanayopingana ambayo ni lile la viongozi na la wanachama.


  Alifafanua kuwa kutokana na mgawanyiko huo, viongozi wa taifa hawasikilizi maoni ya wanachama wala wananchi kwa ujumla.

  “Viongozi wa chama taifa walikuwa na nafasi ya kushinikiza ili wamiliki halisi wa Dowans wafahamike, lakini matokeo yake wamebariki malipo hayo bila hilo kufanyika.


  “Ufike wakati tuwe na uzalendo na nchi yetu, chama ndicho kinachohubiri amani na upendo hivyo kinatakiwa kuilinda na viongozi kuwa wawazi na wa kweli kwa wanachama na wananchi wake,’’ alisema.


  Mwaigaga alisisitiza kuwa suala linalogusa wananchi linatakiwa kushughulikiwa kwa umakini badala ya kufanyiwa ubabaishaji kama masuala ya mchezo wa mpira wa miguu.

  Naye mkazi wa Mwanjelwa, Zawadi John, alisema CCM ilipaswa kuwaelimisha wananchi kuhusu Dowans na siyo kutoa maamuzi.


  Kilimanjaro

  Mwanasiasa mkongwe, Peter Kisumo aliunga mkono msimamo huo uamuzi wa kusitisha malipo hayo hadi shauri lililowasilishwa mahakamani na wanaharakati litakapotolewa uamuzi.

  “Nimefurahishwa sana kwamba Kamati Kuu ilisema kwamba inangoja maamuzi ya kesi iliyofunguliwa na raia mmoja na wanasema ingawa nchi ilikosea, lakini wanatambua kuna raia anapinga mahakamani hilo jambo,”alisema Kisumo.

  Kisumo aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa maelezo ya Kamati kuu yako kiutu uzima zaidi kwamba mkataba wa Dowans ulisainiwa na Tanzania kama nchi na kama mahakama za kidunia zinasema nchi ilikosea, inaweza kujitetea.

  Hata hivyo, baadhi ya viongozi na wanachama wengine wa CCM wakiwamo wenye nyadhifa za juu wanauona msimamo huo wa Kamati Kuu ni sawa na CCM kujichimbia kaburi lake kwa kuwa imeshindwa kusoma alama za nyakati kabla ya kutoa tamko hilo.

  “Siamini kama Chiligati ndivyo alivyotumwa na wajumbe wa Kamati Kuu chini ya Rais Kikwete kusema hayo kwa sababu hakuna Mtanzania yeyote anayekubali malipo hayo yafanyike isipokuwa kikundi cha watu wachache,” alidai kigogo mmoja wa CCM.

  Mjumbe mmoja wa Kamati ya Siasa ya CCM wilayani Mwanga aliyeomba jina lake lihifadhiwe alisema anaamini yaliyotabiriwa kwamba huenda CCM ikafa mikononi mwa Kikwete ndicho kinachoweza kutokea mwaka 2015.

  “Wakati wa kampeni hapa tumepata tabu sana na suala la ufisadi, halafu leo Kamati Kuu inatuongezea mzigo mwingine wa kujieleza kwa wananchi kuhusu Dowans. Sielewi kama viongozi wetu wanaitakia mema CCM,” alisema.

  Mwanasiasa huyo mwenye ushawishi mkubwa miongoni mwa wanaCCM wa kada ya kati, aliwataka viongozi wa kitaifa kutafakari kwa kina sababu za Watanzania kuichukia CCM kiasi cha kuonyesha hasira zao kwenye uchaguzi uliopita.

  Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Mrema alisema hawezi kutoa maoni yake kwa sasa kwani kuna nyaraka muhimu za utafiti anazisubiria ndipo atoe msimamo wake juu ya Dowans.

  Mbunge wa zamani wa Jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM) ambaye alikuwa mmoja wa wabunge wapambanaji wa ufisadi, alisema anachokiona ni kwamba chama chake kimekata mawasiliano na wananchi na hakijui hasira yao.

  “Mimi nadhani CCM wamekata mawasiliano na Wananchi wanaowaongoza kwa hiyo hawajui walivyo na hasira na Dowans, bora wangenyamaza tu wakaiacha serikali ikaacha isubiri hadi hiyo tuzo isajiliwe mahakamani,” alisema Kimaro.

  Kimaro ambaye ni mfanyabiashara mashuhuri nchini alisema kitendo cha chombo cha juu kama Kamati Kuu kujiingiza katika sakata la Dowans bila kueleza kwa kina nini kilitokea hadi wabariki malipo hayo ni sawa na kujitundika kitanzi.

  “Mimi naishauri CCM na serikali watembee vijijini wapiti kwenye vijiwe vyote si vya mkoa Kilimanjaro tu bali nchi nzima ndiyo wataona watu walivyo na hasira na Dowans kuliko hata shida walizonazo za kimaisha,” alisema Kimaro.


  Tanga

  Rashid Mfaume, ambaye alijitambulisha kuwa ni muasisi wa CCM anayeishi jijini Tanga, alisema mtindo wa uendeshaji CCM hivi sasa ni hatari kwa kuwa kila mmoja ana uwezo wa kuzungumza analolitaka bila kusubiri mamlaka husika.

  “Umoja wa Vijana wa vijana wa CCM juzi walitoa maelezo yenye kupinga Dowans isilipwe hatujakaa sawa Kamati Kuu, inatoa msimamo ulio tofauti. Je, huu ni uendeshaji wa chama uliokuwa ukisimamiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere?” alihoji Rashid.

  Dotto Ali mkazi wa Manundu wilayani Korogwe alisema kabla ya UVCCM kutoa tamko la mambo nyeti kama ya Dowans hadharani, kulitakiwa kuwa na utaratibu mawasiliano na mkubwa wake ambaye ni CCM kujua msimamo wake badala ya kuwakaanganya wananchi.

  Katibu wa TLP Mkoa wa Tanga, Rashid Amir,aliwapongeza vijana wa UVCCM kwa kuonyesha hadharani hisia zao juu ya kuchukia malipo ya Dowans na mikopo ya wanafunzi na kwamba wameonyesha kuwa na uchungu na nchi yao.

  “Vijana wa UVCCM wamevumilia hadi wamechoka wakaamua kutangaza msimamo wao kama watoto wa walala hoi. Vijana hao wameona jinsi jahazi linavyokwenda mrama, lakini bahati mbaya bado wakubwa zao CCM hawawajali wananchi,”alisema Rashid.

  Calistus Shekibaha aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo la Korogwe Mji kupitia Chadema aliwashauri vijana hao wa UVCCM kukihama chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani au waanzishe chama chao cha siasa ambacho kitakuwa na huruma kwa wananchi.

  Alisema CCM haina utamaduni wa kusikiliza changamoto wala mawazo yaliyo tofauti na vigogo wake, hivyo hakuna haja kwa vijana wenye mwelekeo wa maendeleo kuendelea kubaki huko.

  “Hawa vijana wa UVCCM ni wanamapinduzi, wanauchungu na nchi yao,wanaona jinsi mambo yanavyokwenda kombo na kubwa zaidi waliona joto ya jiwe wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu uliopita hivyo wameamua kuwa
  wakweli,” alisema.


  Arusha

  Wakizungumza katika mahojiano maalum, Calist Lazaro, Jonathan Lymo na mratibu wa mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Arusha,(ANGONET), John Bayo, walisema, CCM itakuwa inajimaliza yenyewe kuunga mkono malipo ya Dowans.

  Lazaro ambaye ni Kada wa CCM, alisema haiwezekani kampuni ya Dowans kulipwa kwani ilipewa kazi ya kufua umeme na kampuni hewa ambayo ilithibitishwa na Bunge la Tisa

  "Kwanza hawa viongozi wangu waseme, tunamlipa nani na kwa nini, na kama kweli watalipa basi CCM inakufa," alisema Lazaro ambaye alikuwa mgombea wa udiwani Kata ya Sokoni kupitia CCM.

  Lymo alisema, Kamati Kuu ya CCM, ilipaswa kuheshimu maoni ya wananchi walio wengi kwa kuonyesha kuchukizwa na kutaka kutumiwa vibaya fedha za umma.

  Naye Bayo, alisema ANGONET, itasikitishwa kama Dowans ikilipwa kwani tayari ilithibitika mbia wake ni kampuni hewa na hivyo hata wao, uhalali wao una utata.

  "Haya ni matumizi mabaya sana ya fedha za walalahoi, kutoa Sh94 bilioni kwa kampuni ya ujanja ujanja, ni aibu kwa taifa letu...sio busara kabisa kulipa," alisema Bayo.

  Imeandaliwa na Burhani Yakub, Daniel Mjema, Musa Juma, Godfrey Nya’ngoro, Neema Myovela, na Brandy Nelson,
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,308
  Likes Received: 418,592
  Trophy Points: 280
  Kama kuna mahesabu JK aliyakosea ni haya ya DOWANS..........................hivi karibuni atajua TZ ina wenyewe.............hata akijaribu kututisha na udini safari hii hatutababaika..............................ila tutapambana na ufisadi tu...........................
   
 3. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  CCM kwisha kabisa
   
 4. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Tiketi ya kwenda kuzimu siku zote bei yake si ndogo.
  Good luck CCM.
   
 5. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  .............Nimefurahishwa sana kwamba Kamati Kuu ilisema kwamba inangoja maamuzi ya kesi iliyofunguliwa na raia mmoja na wanasema ingawa nchi ilikosea, lakini wanatambua kuna raia anapinga mahakamani hilo jambo,"alisema Kisumo.

  ---Ingawaje sipendi serikali na mawakili wanaoitetea Dowans wachinde .. Kesi hii itaibua mengi ndani ya macho ya mahakama...ukiwemo uwezo wa serikali kuamua mambo ya malipo bila kuwaelimisha au kuwashirikisha kwa kina wananchi...pia serikali haitaweza tena kuendeshwa kimatonya kutoka na athari za kesi hii kama ikiangukia upande wa walioifungua....

  Wanaharakati wa kesi sasa inabidi waangalie move nyingine ya kuibana serikali maana yapo mengi sana ya mtindo wa kiduwanzi/Dowans...

  1. Kama wananchi wanaweza ku-challenge malipo yatakayofanywa na serikali kwa Dowans ni wazi kwamba siku za usoni wataweza pia ku-challenge malipo ya aina yoyote ile yanafanywa na serikali kwenda sehemu yoyote ile....ikiwemo kuchukua mikopo ambayo wananchi hawaiafiki au ambayo hawajui ilichukuliwa kwa ajiri gani... kupokea misaada bila kujua nini hasa dhumuni la misaada hiyo... au masharti yoyote ya misaada na mengine mengi..

  2. Ni wazi kwa kimazingira yalipo itaonekana kwamba watawala hawawezi tena kufanya maamuzi mbofumbofu maana wanajua kwamba watakuwa challenged ku-justify yale wanayofanya, watakafanya au waliyofanya...

  3. Serikali itawawekea shinikizo ma-judge wa kesi hiyo pia wanaharakati ili wakubali deni lilipwe na pia ili iweze ku-enforce hukumu hiyo maana itasema maamuzi ya mahakama yaheshimiwe ni muhimili mwingine wa dola.

  4. Mwisho wa siku Dowans watalipa ingawaje Richmond ni feki na concept ya ufeki (wa Richmond au uhalali wa Dowans kumilikishwa mitambo wakati kwenye kesi ya Texas tayari Dowans wanadai mitambo hiyo ni yao) bado haijaeleweka kwa watanzania na wapiga kura kwa ujumla...

  5. Serikali iache kuwachanganya watu kwa kuwabebesha zigo lisilo stahili....itakuja fikia mahali wananchi watasema HATUTAKI KUCHEZA NA NYANI KWENYE SHAMBA LA MAHINDI VINGINEVYO TUTAFIRISIKIA... Full stop....liwalo na liwe tufanye ya Tunisia.... sijui viongozi watakimbilia wapi?
   
 6. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  natamani hata kulia jamani, hii nchi inaelekea wapi?
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Usilie mama ukilia utaliza wengi...we acha tu
   
 8. b

  binti ashura Senior Member

  #8
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  tutapiga kelele saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana!, lakini pesa zitalipwa tu!. nakumbuka nilipokuwa nasoma darasa latano enzi zile kulikuwa kuna sera moja kwenye kitabu cha kiswahili iliitwa ''muweka nadhili na shetani''. sasa kama nduguyetu aliweka nadhili na mafisadi (mashetani wetu wa uchumi wa nchi) kwanini asiwalipe?

  tatizo letu tuliambiwa kuwa mtu akitumia rushwa ili aingie madalakani, atakuomba rushwa ili akuletee maendeleo!. yote hayo tumeyaona na sasa tusikilizie maumivu.

  kwni ccm ikifa unafikili jk anashida gani ikiwa yeye amemaliza muda wake wa kuwa rais, yeye hajali watakao kuja. kuna mambo tulishaambiwa kuwa tusiwe mbayuwayu tuchanganye na zakwetu kama hatukuchanganya basi tusikilizie maumivu.
   
 9. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  we acha tu, some tymz sipendagi hata kupitasha macho kwenye hili jukwaa maana naweza kupata ugonjwa wa moyo nikisoma haya yanayoendelea kwenye hii nchi.
   
 10. T

  Tata JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Usilie Lady N. Nchi ina mwelekeo mzuri tu mpaka sasa. Hiki tunachoshuhudia ni mchakato wa mabadiliko. Wananchi wanabadilika kutoka kwenye ukondoo wa zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM uliojengwa kwa zaidi ya miongo mitatu na sasa wanaanza kuhoji fikra za kipumbavu za viongozi wao. Kwangu mimi hilo ni jambo jema.

  Taratibu watu watajua kuwa kiini cha matatizo ya nchi hii siyo mipango ya Mungu kama ambavyo viongozi wa dini wababaishaji wakishirikiana na wanasiasa matapeli wakekuwa wakituaminisha. Watajua kiini cha matatizo yetu ni watawala wezi wasio na uzalendo wala uchungu na nchi na wananchi wake.
   
 11. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #11
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Zamani tulikuwa tunaimba PIGA MAGOTI AMIN, PIGA MAGOTI AMIN, IDD AMIN AKIFA MIMI SIWEZI KULIA NITAMTUPA KAGERA AWE CHAKULA CHA MAMBA! AAAAAAAA! CHA MAMBA!

  Sasa tunatakiwa kuimba Piga Magoti CCM Piga Magoti CCM, Li CCM likifa mimi siwezi kulia, nitalizika kaburini! kaburiniii! kiwe historia ya mafisadii! iii! mafisadi!
   
 12. T

  Tata JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Binti ashura ungekuwa karibu ningekupa kiss kubwa sana. Mambo uliyoongea yamenikuna. Huyu huyu JK alishasema kuwa kuna asilimia kumi na tano ya watanzania wanaompinga, nyingine kumi na tano wanamuunga mkono bila maswali na iliyobaki yaani asilimia sabini wanafuata upepo tu. Hawajui wala hawajali kinachoendelea.

  CCM wanajua kuwa hawa wanaopinga malipo ya DOWANS ni wale asilimia 15% tu. Hivyo wana uhakika kuna asilimia 15% ya watanzania wanawaunga mkono kwenye malipo hayo na kuna asilimia 70 ambao wanafuata upepo tu na hawajui kinachoendelea.
   
 13. T

  Tata JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Don't count them off so easily my friend. They are still very much alive and kicking. Wanasubiri tu mgao wao wa DOWANS ili wajiandae kuchakachua matokeo ya uchaguzi wa 2015 na kuendelea kutawala nchi.
   
 14. c

  care4all Senior Member

  #14
  Jan 23, 2011
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Arbitration:
  All disputes arising in connection with this Contract or the execution thereof shall be settled by way of amicable negotiation. In case no settlement can be reached, the parties shall refer any dispute or difference arising out of relating to this Contract to arbitration in accordance with the Arbitration Rules of the International Chamber of Commerce (ICC). The award by the said Commission shall be deemed as final and binding upon both parties.


  kwenye mikata mingi ya kimataifa utakuna na vipengere vinavyo fanana na hicho hapo, so kama mambo yako unafanya kisiasa au kitoto wakati unajua ulichosaini kwenye mkataba lazima ujue in the end utakikalia kidole na jamaa ndo kesha vuna hivyo.... mgao wa umeme upo palepale, Mwakyembe si alishasema?

  Sasa tupange kete upya vinginevyo tutafute mwekezaji wa kiwanda cha vibatari
   
 15. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kama vile ulikuwa kwenye akili yangu, ni maandalizi ya 2015 haya!
   
 16. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Gazeti la The citizen la leo 23 January, ukurasa wa 12 lina katuni yenye swali moja muhimu kuhusu kamati kuu ya CCM kuunga mkono malipo kwa DOWANS.

  Ujumbe ni rahisi: Ni maskini, mzee akijiuliza kama haya yote yanastahili kupelekwa ICC. Lakini, iweje CCM ijadili na kupitisha malipo ya DOWANS na hakuna lolote walilosema juu ya malipo ya wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki?

  Nami sasa naamini kutowalipa Wastaafu wa EAC ni uhuni wa serikali.
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,308
  Likes Received: 418,592
  Trophy Points: 280
  Dowans kuhatarisha uhalali wa serikali


  "Kama watalipa faster faster (haraka) watakuwa wameongeza upana wa hoja yangu, badala ya kuliomba bunge kumpigia kura Ngeleja ya kujiuzulu, nitaliomba bunge kadri litakavyoona inafaa, lipige kura ya kutokuwa na imani na serikali," alisema David Kafulila.

  Na Tumaini Makene

  SAKATA la Kampuni tata ya Dowans bado tete na
  bichi sasa imeelezwa kuwa kama halitafanyiwa kazi kwa umakini litaipotezea serikali uhalali wa kisiasa wa kuongoza wananchi walioiweka madarakani.

  Iwapo serikali itafikia uamuzi wa kuilipa mabilioni ya fedha kampuni hiyo bila ukweli kuwekwa bayana ili kuondoa 'mazonge mazonge' yanayolizunguka sakata hilo, utakuwa uamuzi mbaya, ukifananishwa na kujitia kitanzi.

  Kwa mujibu wa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), Bw. David Kafulira, kama serikali itaendelea na mipango yake ya 'fasta fasta' kuilipa Dowans sh. bilioni 94 kama ilivyoamuriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) kabla ya mkutano ujao wa bunge, ijiandae kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nayo.

  Akizungumza jana Dar es Salaam, katika mkutano wa wabunge wasiokuwa katika kambi rasmi ya upinzani bungeni na waandishi wa habari, Bw. Kafulila alilifananisha sakata hilo na kashfa maarufu ya Goldenberg nchini Kenya.

  Alisema "inashangaza kuona serikali inakuwa na speed (kasi) ya ajabu kutaka kuilipa Dowans eti kwa sababu ni suala la kisheria, mbona hatujaona speed hiyo katika kuwalipa walimu waliokuwa wakiidai serikali kisheria pia, au kwa nini hatuoni kasi hiyo katika kuwalipa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanaoidai kisheria.

  "Serikali itambue wazi kuwa hili si suala la lelemama wala masihara...Ngeleja (William, Waziri wa Nishati na Madini) asicheze na moto wa Dowans, chimbuko lake ni kubwa liliwahi kuiangusha serikali, alipojiuzuru waziri mkuu. Asikurupuke kufanya maamuzi. Maana hata ndani ya serikali inaonekana hawana mwafaka juu ya suala hili," alisema na kuongeza;

  "Serikali iwe makini kuna mazonge mazonge mengi katika hili, ukweli haujajulikana. Serikali inapoteza legitimacy (uhalali) wa kisiasa wa kutawala, suala hili litaiondoa CCM madarakani kama kashfa ya Goldenberg ilivyoitafuna na kuiondoa KANU na Moi (Rais Mstaafu wa Kenya, Daniel Arap) madarakani.

  "Kashfa ile nchini Kenya ilianza miaka ya 1993 huko, hivi hivi, lakini ikaja ikaiangusha KANU na Moi. Unajua unapopoteza uhalali wa kisiasa wa kuongoza unaweza kusababisha machafuko, hasa katika wakati huu ambapo kuna tatizo kubwa la uadilifu wa viongozi. Waache hoja iende kwenye mkaa wa moto wa bunge, kisha ndiyo walipe."

  Ingawa alisema mpaka sasa hajajibiwa rasmi kama hoja yake itawasilishwa katika mkutano wa pili wa Bunge la 10 uliopangwa kuanza Februari 8, Bw. Kafulila aliongeza kuwa iwapo serikali itaamua kufikia maamuzi ya kuilipa Dowans, itakuwa imepanua wigo wa hoja yake binafsi, kwani ataliomba bunge 'kadri linavyoona' lipige kura ya kuiangusha serikali.

  Mpaka sasa hoja yake hiyo, ambayo aliiwasilisha ofisi za bunge Desemba 10 mwaka jana na kujibiwa Desemba 14 kuwa inafanyiwa kazi, ina sehemu mbili, mgawo wa umeme unaoendelea kuathiri uchumi na hukumu ya ICC iliyoiamuru TANESCO kuilipa Dowans sh. bilioni 94 kwa kuvunja mkataba wa kuzalisha umeme.

  "Hatuwezi kuendeshwa kwa mambo ya mission town (ujanja ujanja wa mjini), kama watalipa faster faster (haraka) watakuwa wameongeza upana wa hoja yangu, badala ya kuliomba bunge kumpigia kura Ngeleja ya kujiuzulu, nitaliomba bunge kadri litakavyoona inafaa, lipige kura ya kutokuwa na imani na serikali.

  "Ipunguze speed ya kulipa, mbona hatuioni speed ya namna hiyo sehemu nyingine...pia kama bunge litaona kuna haja ya taarifa ya Mwakyembe kusomwa yote pia hakuna shida," alisema Bw. Kafulira.

  Akiunga mkono hoja ya Bw. Kafulira kuwa kamwe nchi na Watanzania wasitarajie kuendelea kiuchumi kwa matatizo ya umeme yaliyopo nchini, Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Bw. Mohamed Habib Mnyaa, alisema kuwa uzalishaji na mahitaji (matumizi) ya umeme ni moja ya vigezo vinavyotofautisha mtu mmoja mmoja au nchi moja na nyingine, katika maendeleo ya kiuchumi.

  "Kwa maana ya kiinjinia ukiuliza maana ya maendeleo ni nini, utaambiwa katika sentesi moja tu, kuwa mtu au nchi inayotumia umeme mwingi;

  "Kafulila hapa kasema kuwa mahitaji ya umeme Tanzania ni megawati elfu moja mia tano, lakini wenzetu South Afrika (Afrika Kusini) mahitaji yao ni megawati arobaini na mbili elfu (42,000), tofauti hiyo ndiyo iliyopo pia katika pengo la namna nchi hizi kila moja kimaendeleo," alisema Bw. Mnyaa ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dkt. Mwakyembe.

  Machafuko Arusha na Katiba Mpya

  Mapema, Mwenyekiti wa kamati ya wabunge wasiokuwa katika kambi rasmi ya upinzani bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF) alisema kuwa machafuko ya Arusha yamesababishwa na serikali kushindwa kutimiza wajibu wake, hasa wa kuwasiliana na raia wake katika namna nzuri, kuepusha madhara.

  Alisema ingawa mauaji hayo si mara ya kwanza kutokea nchini, akikumbushia mauaji ya Zanzibar na Mwembechai, Bw. Hamad alionekana kushangazwa na tabia inayoota mizizi ya viongozi kutowajibika linapotokea suala la uvunjifu wa utawala bora, hali ambayo itaifanya nchi isitulie.

  "Tunapenda kutoa pole kwa wafiwa. Mola awalaze marehemu mahala pema peponi. Tumejifunza mengi kutokana na hilo, ingawa si mara ya kwanza...sisi tulipoteza takribani vijana 43 ingawa matangazo yake yalikuwa kama amekufa mtu mmoja, Mwembechai pia walikufa watu wengi...kote huko hakukuwa na publicity (haijatangazwa) kama ya Arusha.

  "Ninachomaanisha kusiwe na double standard katika mambo haya...suala la Arusha kuna pande mbili, serikali na raia wake...raia wana haki zao na serikali ina majukumu yake...serikali inapaswa kuboresha mawasiliano na raia wake ili kuepusha madhara...huwezi kuruhusu maandamano leo halafu asubuhi ghafla unakataa.

  "Lakini pia serikali inaweza kuja na sababu nzito isiyoweza kusema hadharani hasa wakati huu ambapo dunia ina mambo ya ugaidi na vitu vingine, lakini ni jukumu la serikali kuboresha mawasiliano kwa namna ambayo hata raia wanaozuiwa waridhike kuwa kuna suala la msingi.

  "Lakini la pili, kuna suala la kuwajibika...kuna matatizo ya serikali au viongozi kuwajibika, hili limekuwa tatizo la msingi sasa nchini, serikali lazima iwajibike, kutowajibika kunaifanya nchi isitulie maana kuna watu wanakuwa hawajaridhika," alisema Bw. Mohamed.

  Akizungumzia suala la katiba mpya, Bw. Hamad ambaye alikuwa Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika bunge lililopita, alisema kuwa ni muhimu kuwa na katiba itakayotokana na wananchi, ambayo pia haitaacha kipengele muhimu cha kuwahusisha wananchi kila serikali inapotaka kufanya maamuzi makubwa nchini.

  Alitolea mfano wa Tanzania Visiwani, ambako Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, haiwezi kufanya jambo lolote kubwa linalogusa maslahi ya wananchi bila kuitisha kura ya maoni ya Wazanzibar wote, kwani ndivyo marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanyika mwaka jana, yanavyosema.

  "Pia wananchi wapewe nafasi ya kusema ili iandikwe katika katiba wanataka mfumo wa aina gani wa serikali nchini. Suala hili sioni likizungumzwa katika mijadala inayoendelea...hatuwezi kuacha suala hili katika sera za vyama vya siasa, CUF wanasema serikali tatu, CCM serikali mbili kuelekea moja, NCCR nao tatu.

  "Masuala ya msingi kama haya yanapaswa kuwekwa katika katiba si ilani ya vyama, ukienda Marekani au Uingereza leo yako mambo ya msingi ambayo hata akija nani hawezi kuyabadili anavyotaka kwa sababu tayari wananchi wa Marekani au Uingereza walishaamua," alisema Bw. Hamad akiwa na matumaini makubwa kuwa katiba mpya itapatikana.
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,308
  Likes Received: 418,592
  Trophy Points: 280
  Dawa ya huu upuuzi wa DOWANS ni maandamano nchi nzima ya kushinikiza Bunge limshtaki JK afunguliwe mashtaka, afukuzwe kazi na kazi ya kuliunda upya taifa hili ianze...............................................
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,308
  Likes Received: 418,592
  Trophy Points: 280
  Mtikila apongeza UV-CCM kuhusu Dowans


  Na Grace Michael

  MWENYEKITI wa Democratic Party, Mchungaji Christopher Mtikila amesema kuwa kitendo cha ujasiri kilichofanywa na Umoja wa Vijana wa
  Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) cha kupinga kulipwa kwa mabilioni ya fedha kwa Dowans kiwe daraja kwa Watanzania wote katika kuhakikisha fedha hizo hazilipwi.

  Mbali na hilo, pia amewataka Watanzania kutoogopa kupinga suala hilo kwa kuwa hakuna sheria yoyote inayoweza kuwabana wakati wa kudai maslahi ya taifa na haki za Watanzania.

  Mchungaji Mtikila aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hukumu ya fidia ya sh bilioni 94 za Watanzania kwa Dowans, kitendo ambacho alisema ni 'uporaji wa nchi kwa bastola ya Dowans'.

  UVCCM wanapaswa kupongezwa kwa kile walichokifanya kwa kuwa wanawakilisha mawazo ya Watanzania wazalendo, hivyo tukitumie kitendo hicho kama daraja muhimu la kutuunganisha sisi wana wa Tanganyika katika vita ya ukombozi ili kuangamiza magenge ya uporaji wan chi yetu,� alisema Mchungaji Mtikila.

  Alhamisi iliyopita, UV-CCM ilitoa msimamo wake kuwa Dowans wasilipwe fedha na serikali, bali waisaidie kuipata kampuni ya Richmond iliyohamishia mkataba wake ili iwalipe fedha hizo.

  Vijana hao walipendekeza suala la Dowans lirejeshwe bungeni kwa majadiliano zaidi, ili kuchukua hatua dhidi ya yeyote aliyehusika na madudu hayo.

  Alisema kuwa wananchi wanapoamua kulinda maslahi ya taifa lao huwa hawafungwi na sheria kwa kuwa sheria ni chombo kinachoweza kutumiwa kwa ajili ya kudhulumu haki au kutoa haki, hivyo katika mapambano ya haki sheria hukaa pembeni.

  Alisema kuwa ibara ya 27(2) inataka wazawa wa nchi kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa, hivyo akawataka wananchi kujiuliza Dowans inaiuzia bidhaa gani taifa kwa hayo mabilioni ya fedha.

  Uzalendo tunaolazimishwa na katiba ni kuipuuza mahakama ya kimataifa na kuwashughulikia waliohusika na uporaji kuanzia wa IPTL, SONGAS, AGGREKO, DCP, EPA, Kagoda Agriculture Ltd, hujuma za mitandao ya simu za mikononi,� alisema.

  Kutokana na hali hiyo alisema kuwa umefika wakati kwa Watanzania 'kuhamia barabarani kama familia moja' kwa ajili ya kuondoa utawala uliopo kwa kuwa unadidimiza haki za wananchi.

  Alisema kuwa Dowans italeta ukombozi katika nchi hii kwa kuwa hata Rais Jakaya Kikwete anahusika kwani alipotuhumiwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa hakuweza kukanusha tuhuma hizo.

  [​IMG]   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,308
  Likes Received: 418,592
  Trophy Points: 280
  Mtikila hapo amechemsha.......kwa sababu hawa UVCCM bado hawajatambua ya kuwa kiini cha DOWANS ni ufisadi ambao JK anauendesha pale Ikulu..........................................kwa hiyo kauli yao inaficha maovu na kamwe haiwezi kuisafisha serikali wakati JK anaendeleza kuigeuza Ikulu kuwa ni pango la mafisadi........................................

  Majawabu ya ufisadi ambao JK anauendesha pale Ikulu ni raia wote kuingia mtaani kwa maandamano yasiyo na kikomo kama yale ya Tunisia kushinikiza JK aachie ngazi na asipofanya hivyo................................kulishinikiza Bunge limshtaki, limchunguze na hatimaye kumfukuza kazi..................................

  Vinginevyo tutaendelea kutwanga maji kwenye kinu tu.........................................na hata ukiwatoa akina Ngeleja na wengineo bado mzizi wa ufisadi ambao ni Jk mwenyewe utaendelea kuzalisha wafanikishaji wengine wa ufisadi tu...........................na wala siyo vinginevyo.......................
   
Loading...