Wadada: Hizi Makeup, give us a break

Wadada: Hizi Makeup, give us a break

12227150_1060788230633340_5907759800622460534_n.jpg
12079545_780285498783592_2939407029926687649_n.jpg
12234941_523678341133261_9101921961191569919_n.jpg
Kwa muda mrefu nimekua nikiwavumilia sana na hizi poda zao, yaani unakuta mdada kapaka poda mpaka unashangaa huyu hakuwa na kioo ajione alivotoka?

Yaani hana hata urafiki na majirani angalau wangemwambia akazipunguze tu basi?Leo nimesikitika zaidi na naandika huu uzi kwa mfadhaiko sana nilipokutana na mdada kapaka poda kama Maiti!

Walahi mnaweza cheka lakini kwa poda ile jamani hapana unaweza kuota usiku hasa kama uliyekutana naye anafanana na ndugu/rafiki ambaye unamfahamu na kwa bahati mbaya akatutoka!

Sasa wadada jamani msidhani wanaume wanazipenda hizo poda na wala msidhani mnavutia sana mkipaka sana mnaongeza joto tu hapa mjini!

Kitu kingine ni hizo lipstick!Jamani give us a break tuna vitu vingi tu vya kushangaa yaani unakuta eti ndo kumechisha wigi, lipstick, wanja, kucha, hadi nyusi? Aaah jamani hampendezi kuweni tu original and simpe i swear mtapendeza sana.

Message Sent na yaweza kuwa delivered pia maana yule niliyekutana naye anaonekana mjanja tu siamini kama hayupo humu JF!
 
Kuna kipindi nlikuwa na date binti flan hivi maeneo ya kitaa. Kila tulipokuwa tunaagana after any meeting,ilikuwa lazima anihug. Mimi hupendelea sana kuvaa nguo nyeupe,hasa t-shirts.

Kuna siku ilikuwa nafanya usafi wa nguo zangu,nkakuta almost all of my t-shirts zina marangi rangi mekundu sehem za mabegani kuelekea mgongoni. Nikajiuliza sana,ila kwavile mizunguko yangu huwa mingi nkahisi kunasehemu niliegemea tu.

Ilinichukua muda sana kuja kutambua kuwa zile ni rangi toka kwenye uso wa yule binti kila alipokuwa akini hug.

Dada zangu,mpendeze msipendeze ilo niswala lenu binafsi, mimi naomba mjali na mavazi yetu sisi mnaotu-hug.

#Analyse.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom