Wachina wamchapa makofi mkuu wa kituo cha polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachina wamchapa makofi mkuu wa kituo cha polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sweke34, Jun 22, 2011.

 1. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  VURUGU kubwa zilizuka juzi kwenye kituo cha Polisi Babati Mjini mkoani Manyara baada ya wafanyakazi wa kampuni inayojenga barabara ya Chico, raia wa China kumpiga mkuu wa kituo hicho, ASP Shaaban Minginye na mkuu wa polisi jamii mkoani humo, ASP Morris Okinda.

  Tukio hilo lililodumu kwa saa mbili kati ya saa 12:30 jioni hadi saa 2:30 usiku liliwalazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto zilizorushwa hewani ambazo hata hivyo zilijibiwa na Wachina hao wakitumiia bastola nao, hali iliyoweka rehani amani mjini Babati.

  Wachina hao wanadaiwa kufanya vurugu hizo na kuwashambulia ASP Mingiye na Okinda kwa madai kuwa polisi walimwachia dereva wa basi la abiria aliyelikwaruza gari lao na kusababisha ajali.

  Kitendo hicho cha kuwapiga makonde viongozi hao wa polisi mkoani humo kiliamsha hasira za wananchi ambao walianza kumshambulia mmoja wa raia hao wa China.

  Mwananchi ilishuhudia raia huyo wa China, Chang Charles akipigwa na wananchi hao waliochukizwa na kitendo chao cha kuwapiga polisi ambapo alijaribu kutumia mtindo wa kujihami 'kung fu' huku akitoa sauti za, 'huu, haa', lakini alipigwa ngumi iliyomjeruhi usoni

  Katika tukio hilo, ASP Minginye alipigwa vibao na ngumi na raia mmoja wa China ambapo raia watatu wa China walijeruhiwa vibaya na wananchi na kulazwa kwenye Hospitali ya Mrara mjini Babati na hali zao zilielezwa kuendelea vizuri.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Liberatus Sabas alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kwamba raia 10 wa China wanashikiliwa kwa kuhusika na vurugu hizo.


  Alisema chanzo cha vurugu hizo ni raia mmoja wa China, (Chang Charles) kumpiga mkuu wa kituo cha polisi Babati, baada ya kuliachia basi la abiria lililogonga lori linalomilikiwa na kampuni hiyo (Chico), kitendo kilichofanya wananchi kumpiga Mchina huyo.

  "Hali hiyo ilijitokeza baada ya basi la abiria aina ya Scania, mali ya Kampuni ya NBS lililokuwa likitokea Kahama kwenda Arusha kukwaruzana na gari la kampuni hiyo ya Kichina lililokuwa linatumika katika ujenzi wa barabara ya Babati-Singida,"alisema.

  Alisema baada dereva wa basi hilo kulikwaruza gari la kampuni ya Chico aina ya Ford, tukio hilo liliripotiwa kituo cha polisi Babati na dereva wa basi kutakiwa kuwapeleka abiria Arusha ili kesho yake arudi kituoni hapo.


  “Baada ya dereva wa basi kuruhusiwa na kuondoka raia mmoja wa China alianza kurusha mawe kwenye basi hilo na kuvunja taa na kioo cha mbele na kumpiga mkuu wa kituo, ndipo abiria waliposhuka na kuanza kumshambulia Mchina huyo,” alisema Kamanda Sabas.


  Alisema baada ya vurugu hizo lilizuka kundi lingine la raia wa China lilijitokeza na kuanza mapambano na wananchi na ndipo katika vurugu hizo askari polisi wakapiga risasi hewani na mabomu ya machozi ili kuwatawanya na kujaribu kusitisha vurugu hizo.


  “Hadi hivi sasa Jeshi la Polisi linawashikilia raia 10 wa China wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo na tunatarajia kuwafikisha mahakamani leo (jana), ili wakajibu mashtaka ya uaribifu wa mali na kufanya vurugu,” alisema Kamanda Sabas.Kamanda Sabas aliwataja Wachina hao wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Chang Charles, Luan Hiten(23), Wang Sheng(23), Sing Yun(24), Sing Jin (23), Lin Jun (37), Whang Puong(23) Lu Gang (23) na Sio Jing (23).

  Alisema katika vurugu hizo, askari polisi mmoja ambaye hakumtaja jina alijeruhiwa jichoni na Wachina hao na raia watatu wa China walijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mrara wakipatiwa matibabu.

  Aliwataja raia hao wa China waliojeruhiwa kuwa ni Young Gris, Luan Hiten na Chang Charles ambao alisema hali zao zinaendelea vizuri, baada ya kupatiwa matibabu.
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Safi sana kumbe nao kuna wanaoweza kuwapiga! nilifikiri wao wako above the law kwa kuua raia bila sababu. Na upande mwinngine wananchi wanaki helelhele wangewaacha wapigwe vizuri ili liwe fundisho.
   
 3. LD

  LD JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa sababu hawa wachina walijiona wao wapo juu ya sheria na kupiga gari ya abiria wa Tanzania kwa mawe, wananchi walifanya vizuri kuwatetea raia na Polisi wao.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Vurugu zimezuka pale wachina walipoanzisha kichapo kwa ujinga wa olisi kama kawaida kule rushwa
  hayo yalitokea pale mkoani manyara wakati wafanyakazi wa kampuni ya chico inayodhaminiwa na wachina hao
  kuanzisha kichapo cha nguvu nje ya kituo cha polisi na wakati wakifikiria hilo mkuu wa polisi akajitokeza kuomba amani nae akala vibao vya kumtosheleza kisanga kilikuwaje pata habari

  lori lilitokea arusha kuelekea manyara liligonga gari ya wachina hawa na dereva kwa pamoja wakaelekea kituonidereva wa gari la wachina wakaoamba dereva wa lori lililowagonga asitoke mpaka kieleweke kuhusu gari lao..wakiwa wanaelekea kwa mabosi wao gafla wakaarejea na kukuta lori halipo wala dereva hapo ndipo wahina waakatandaza kungfu na maandazi yote kwa jumla na hata mkuu wa polisi wa manyara shemeji yangu shaabani minginye asp alipokaribia nae wakampa zakinshonshu hapo akaamua kulala mbele na kurudi na askari ambao wakaanza kuwasha bastola angani na wao wakaanza kujibu

  ...hali hii iliendelea kwa masaa mawili mpaka walipoamua kutumia mabomu ya machozi huku babati nzima ikiwaka moto..wachina hao wamedai wamechoshwa na ushenzi wa rushwa zinazokithiri vituoni na kusema sasa imefika wakati na wao wasonge front kutoa kichapo popote kwenye hakli inapoitajika

  habari zaidi soma nunua mwananchi soma pge 4
   
 5. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Taabu ya kuruhusu MGENI aingie hadi BESROOM kwako:) Wamewafuga kwa kuwapatia preferential treatment (kwa karata ya WAWEKEZAJI) sasa wanaanza kuwadunda wenyewe! Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.....Tafakari
   
 6. x

  xavi Member

  #6
  Jun 22, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa wachina wanahaki ya kutoa kichapoo kwa hao polisi manake polisi hawa kuwa tendea haki ili bidii wafatilieee hao walio wagongaa!polisiii rushwa sio nzuriii jamanii!
   
 7. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ukifanaya urafiki na simbafahamu siku moja atang'ata mkono wako!
  Polisi nashirikiana wa waharifu kwa kukubali kupokea rushwa, sasa inapotokea mharifu kamdhulumu mhalifu mwenzake hiyo ndiyo matokeo!
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Too bad. Wachina hao hawatakiwi kuchekewa hata kama askari wana makosa kuachia lori hilo. Sheria mkononi si ndiyo tunayoikataa kila siku?
   
 9. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Waache wafundishwe adabu na Mambwana zao kwani kule Mara siwalituulia ndugu zetu kwa kuwalinda hao hao wawekezaji wao, sasa leo wanakula kisago kutoka kwa mabwana zao waacheni wauliwe nataka hata wakalipue kituo chote hao wachina, kwanza jeshi la Polisi tanzania halina faida yoyote kwa watanzania wamezidi kutunyanyasa na kutuibia pesa kwa kutulazimisha kuwapa zetu na mali zetu. Hasa wale wanaotembelea Bajaji sijui bodaboda wezi sana wakikuona umebeba kafurushi kidogo wanakusimamisha na kutaka kukunyany'anya majambazi yasiokuwa na aibu
   
 10. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  huo ndio utamu wa rushwa!
  ukilitazama kwa ndani sana utapata picha kuwa kuna uhusiano na kujuana sana baina ya wachina hao na polisi waliopigwa.
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nadhani hawa polisi wakipigwa mitama na makofi ndo huwa wanakuwa na akili timamu ya kufanya kazi.

  Wachinabila shaka watakuwa wamejifunza kutoka kwa Robert Kisena mgombea ubunge wa ccm maswa jinsi nalivyomshughulikia ocd wa maswa.

  Nadhani hata hii ya wachina RPC Sumary atasema ni mambo yao binafsi kati ya huyo ocd wa babati na hao wachina.

  Soo litaisha juu kwa ju na wachina wataendelea kuwafundisha kungfu kila wakileta ujinga.Sasa vibarua wa chico mkazi wanayo, kama polisi wanakula mitama na mateke huku wakiwa na bunduki, itakuwaje kwao?? kazi kweloi kweli bongo nchi tambarare.
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,682
  Trophy Points: 280
  Polisi wakidundwa mi nafurahi sana kwa sababu hii mipolisi yetu ni mikatili kuliko ibilisi sasa wakipata wababe wao mi raha tupu
   
 13. F

  Froida JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Polisi wananiudhi kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu lakini kamwe sitapenda kuona polisi wa kitanzania akiwa kwenye crown ya nchi anapigwa na mgeni kwao hakuna anayeweza kufanya hivyo hawa wachina nadhani wanaona wana haki miliki ya nchi wapuuzi wakubwa
   
 14. a

  andry surlbaran Senior Member

  #14
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  imekaa kimbea sana hii!
   
 15. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Wachina hawana haki yoyote ya kumpiga mtu yeyote ndani ya nchi hii kama ilivyo kwa Mtanzania yeyote haruhusiwi kumpiga Mtanzania mwingine kwa sababu yoyote ile! Kitendo hicho hakivumilki na ni udhalilishaji wa Jeshi la Polisi na Serikali ya Tanzania kwa ujumla. Wachina wamekuwa na kawaida ya kupiga Watanzania kila wanapokuwa na miradi ya ujenzi, kwa mfano katika mradi wa Maji kutoka ziwa Victoria kwenda Shinyanga na Kahama waliua Mtanzania mmoja pale Shinyanga kwa madai kuwa ni mwizi.

  Mimi mwenyewe siku moja niliwakuta wamechimba barabara katika eneo la Majengo Mapya mjini Shinyanga bila kutoa njia ya mchepuo kwa watumiaji wa barabara. Iliniuma sana kiasi cha kuamua kuonana na foreman wa eneo lile. Yule bwana niligundua hata Kiingereza alikuwa hajui na hapakuwa na mkalimani wa kumweleza shida yangu, nilijitahidi kutumia lugha ya ishara kwa kutumia mikono yangu. Baada ya muda mfupi nilimwona anapasha mikono hewani ili anishushie kipigo, niliamua kuondoka na akawa ananinyoshea kidole kuashiria maneno kama 'bahati yako umeondoka'. Zipo taarifa nyingi sana za Wachina kuwachapa makonde waTZ katika maeneo mbalimbali ya nchi hii.

  Kama kweli polisi walidai rushwa, sheria za nchi zipo wangefuata utaratibu kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika kwa msaada zaidi ili haki itendeke, kitendo cha kujichukulia sheria mkononi hakikubaliki kwa mtu yeyote ndani ya nchi hii hata kama ni Mchina! Polisi wachukue hatua kali dhidi yao hawana kinga yoyote ya kisheria hivyo wanashitakiwa kama Mtanzania yeyote aliyefanya makosa ya jinsi hiyo. Wakienda jela watajifunza!
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hii imekaa vyema sana, wachina wameonyesha njia nini cha kuwafanya hawa Polisi wetu wachafu
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Kumbe dawa ya uchafunimakofi tu watanzania tutembee na bastola wakirusha juu na sisi tunarusha kama wachina
   
 18. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kwa nini Polisi haikuwapiga Wachina risasi za moto?? Ninaamini kabisa kitendo cha Wachina kufyatua risasi mbele ya polisi na Raia wema kilitosha kabisa kuwatuliza na risasi za Moto. Sasa uzembe wa polisi wakapata kisago cha ngumi baada ya kumwacha mwenye silaha akusogelee. Polisi wamezoe raia wasio na silaha kuwaonea.

  Hayo ndiyo malipo ya kuabudu wageni badala ya wenye nyumba.
   
 19. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,682
  Trophy Points: 280

  Eti polisi wanadai bunduki zao zikilengwa kwa watu weupe hutoa maji badala ya risasi lakini kwa wabongo zinarindima kama kawa.
   
 20. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  risasi mnanikumbusha ndugu zangu n.mara na arusha je wao walikuwa nazo duh!
   
Loading...