Tetesi: Wachezaji watano wa Simba wasimamishwa kupisha uchunguzi kwa kichapo kikali cha goli 5 kutoka kwa Yanga

Wachezaji watano wa Simba Sc akiwemo Henock Inonga, Cloutos Chama, na Shomary Kapombe wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yao baada ya kufungwa na Yanga SC mabao 5-1 siku ya jumapili

Wachezaji hao wanatuhumiwa kuihujumu timu kitendo kilichopelekea kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao

Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao cha bodi ya wakurugenzi ya Simba kilichofanyika jana jijini Daresalam

Chanzo cha uhakika kutoka Simba SC kuwa uongozi umeshapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma dhidi ya wachezaji hao na sasa imeanza uchunguzi wa kina ili kujiridhisha

Wachezaji hao watakua nje ya kambi ya timu mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika

Chanzo hicho kimesema huwenda leo klabu ya Simba ikatoa taarifa ya wazi kwa Umma juu ya maamuzi waliyofikia kuhusu wachezaji hao wau wasitoe ila wahusika wamepewa taarifa

Maamuzi mengine yaliyofikiwa na bodi ni kufutwa kazi kwa kocha mkuu Robertinho, msaidizi wake pamoja na kocha wa viungo.

View attachment 2806921
Moderators waniombe Radhi kwa kufuta Uzi wangu wa Juzi kuwa Inonga, Kapombe, Manula, Chama na Baleke Wameihujumu Simba SC na Kufungwa 5 kwa 1 na Yanga SC
 
Kwa Mpira WA Simba na Yanga sishangai Hilo kutokea rejea ya Shishimbi Yanga hivi vilabu vina mambo mengi Sana nyuma ya pazia
 
Moderators waniombe Radhi kwa kufuta Uzi wangu wa Juzi kuwa Inonga, Kapombe, Manula, Chama na Baleke Wameihujumu Simba SC na Kufungwa 5 kwa 1 na Yanga SC
Kama wamesimamishwa kweli na uliowataja ndo wahusika mods wanapaswa kukuomba radhi hadharani na kukupa heshima yako ya kuiinua JF kwa kuleta taarifa kabla ya habari rasmi.
 
Kama kuna kiongozi yoyote wa simba alikua anafikiri ataifunga yanga nayeye aondoke haraka.Kwani wakikubali kua yanga iko vizuri zaidi kuliko simba ili wapate nafasi yakujipanga upya watapungukiwa nini.Wanakimbilia kuwaza hujuma wakati mpira wenyewe unaonekana tulizidiwa kila mahali.Ata kama kuna hujuma na viongozi watakua wanahusika pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Scout Mkuu hajatimuliwa?
FB_IMG_16993648999722030.jpg
 
View attachment 2806905
Wachezaji watano wa Simba Sc akiwemo Enock Inonga na Clatous Chota Chama wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yao baada ya kufungwa na Yanga SC mabao 5-1 siku ya Jumapili.

Wachezaji hao wanatuhumiwa kuihujumu timu kitendo kilichopelekea kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao

Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao cha bodi ya Wakurugenzi ya Simba kilichofanyika jana jijini Dar es salaam

Chanzo cha uhakika kutoka Simba SC kimeiambia Kishamba Media kuwa uongozi umeshapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma dhidi ya wachezaji hao na sasa imeanza uchunguzi wa kina ili kujiridhisha

Wachezaji hao watakua nje ya kambi ya timu mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika

Chanzo hicho kimesema huwenda leo klabu ya Simba ikatoa taarifa ya wazi kwa Umma juu ya maamuzi waliyofikia kuhusu wachezaji hao au wasitoe ila wahusika wamepewa taarifa

Maamuzi mengine yaliyofikiwa na bodi ni kufutwa kazi kwa kocha mkuu Robertinho, msaidizi wake pamoja na kocha wa viungo.

Kishamba Updates
ni kweli?
 
Back
Top Bottom