Wachawi/wanga huwa wanapata faida gani kusumbua watu...

Huyo atakuwa alitumwa na Lucifer hizo roho za watu - kuna kipindi huwa zinahitajika huko kuzimu, sasa ukishapewa kazi hiyo lazima uifanye vingineyo makubwa yanakukuta kulingana na kiapo ulichoapa. Uwezo wa kuchimbua bila jembe huo anakuwa kashakupatia tayari.

Hapo pia huchimbui randomly hapana, kuna roho zingine hazihitajiki kabisa hata kule kuzimu (Reject). kunakuwa na namna ya ku-pinpoint.
Acha kuwa mbishi,yeye alisema anatumia hivyo viungo kulogea,hata Kagera ndo hivyo mtu akishwa zikwa lazima mlinde kaburi kwa siku saba,msipofanya hivyo mtakuta kaburi limedidimia hapo tayar kashachukuliwa.
 
how are they going to prove, watakachofanya ni kuwatumia wanakijiji kunituhumu tu bila ushahidi wowote ule, hata wakinipeleka mahakamani nitawashinda day one.
Ushahidi upo tu mwingi mkuu,labda wewe umekaa mjini tangu uzaliwe au Ulaya lazidi ushahidi wa haya mambo upo sana.
 
Asante mkuu,
Hapa kwa elimu uliyotoa, Mwanga ndie muhusika mkuu.
Mwanga ananufaika vipi na huo usumbufu...
Mwanga ana nufaika kwako kwa kitendo chake cha kukuchezea wewe usiku ukiwa umelala yeye ndio anapo pata faida. Mwanga ninaweza kumfananisha sawa na Mchezaji wa mazingaombwe au Mwizi. kwa ufupia Mwanga ni Mwizi na mchawi ni Jambazi. Mwizi hadhuru anaiba tu lakini Jambazi anadhuru na kuweza kukutoa hata roho yako.
 
Mwanga ana nufaika kwako kwa kitendo chake cha kukuchezea wewe usiku ukiwa umelala yeye ndio anapo pata faida. Mwanga ninaweza kumfananisha sawa na Mchezaji wa mazingaombwe au Mwizi. kwa ufupia Mwanga ni Mwizi na mchawi ni Jambazi. Mwizi hadhuru anaiba tu lakini Jambazi anadhuru na kuweza kukutoa hata roho yako.
mkuu, kati ya wachawi na wanga wapi ni wengi katika jamii zetu.
 
Raha ya wachawi ni ile kuishi, falme ya ulimwengu usionekana, hilo tu kwao hujisikia raha sana, wewe wakati unafikilia uweke ngazi upande juu ya paa la bati mchana, yeye hukuangalia tu, usiku yeye hupanda bila ngazi kwenye paa lako lile lile. Wakati unawaza nauli ya kwenda kwenu Singida toka Dar, yeye anaenda singida bila basi, na anarudi kwake dar, na alfajiri anatoka kwake kana kwamba amelala humo, hata ikitokea dharula usiku, ukaenda kumgongea kama jirani yako, hutomkosa hata kama alienda Tabora usiku huo. Mchawi anaweza kuwa kiongozi huko kwenye Dunia ya kichawi, huku kwenye ulimwengu unaonekana ni kapuku tu, pia unaweza kuwa na mke mchawi akakuta ni mke wa mtu kwenye ulimwengu wa kichawi. Wewe unachoshwa tu kila siku kagoli kamoja jumatatu, lingine mpaka baada ya wiki moja, na hii hata upande wa wanaume wapo waume za watu kwenye ulimwengu usionekana wa Kichawi. Katika hizi simulizi za kichawi kuna mada iliwekwa hapa kuhusu kijiji cha Gambushi huko Mwanza, kuwa kijiji hicho ikifika saa 12 jioni ukipita na gari mpaka kwanza uombe uruhusiwe ndipo upite, la sivyo, ukijaribu kuipta bila ruhusa saa hizo mpaka saa 12 asbuhi gari yako itazima vituko utavyoviona usiku hutorudia tena ukaidi. Sasa mchawi ile kukuona wewe ukisumbuka kwake ni burudaaani, kama wewe unavyofaidi kwenye huu ulimwengu unaonekana unavyoshudia Simba na Yanga zikipambana, sasa huburudika bila pesa. Ila yote kwa yote wachawi wa wanaishi maisha haya wengi wao ni maskini sana, maana uchawi huendanda na uchafu, kulamatapisha, usaha, damu ya mwanadamu, wakati utajiri unachochoe zaidi usafi, kula vizuri, ili uendane na hali yako.
 
Stori za kichawi nyingi huwa ni kuonyesha wakipiga mikwara bila kuchukua hatua...

mfano:
Mtu kalala usiku eti mchawi anatembea juu ya bati ila haingii ndani...
sasa anapata faida gani...

Mtu umelala kitandani unajikuta uko juu ya bati, au uvunguni kisa wachawi wamefanya yao..
anafaidika nini...

Unaamka asubuhi unakuta umechanjwa chale badala ya kuuliwa kabisa kama ndio ilikuwa nia.
Sasa maana yake ni nini...

Wengine unasikia mtu anatembea ndani ukiwasha taa haoekani...
sasa anatembea ili iweje...


Wachawi wanamambo ya ajabu sana...
Kusumbua watu ndo faida yake
 
tunasikia raha sana,that is a game,hatun football so we enjoy miili yenu by mwenyekiti wa wachawi tanzania
 
Uchawi una algorithm ngumu sana, jiulize kwa nini mganga akufanyie wewe dawa za utajiri ila yeye hawezi kujifanyia? vivyo hivyo hawezi kukuroga wewe bila sababu akifanya hivyo damu yako inaweza kumsumbua sana. Mchawi hawezi kukubia hela yako mfukoni kama umeihesabu, ama anaweza kuingia ndani kwako akakuchezea kama unavyosema lakini hawezi kuiba chochote hata senti moja ingawa of cause anaziona.

Uchawi una principals zake!! ambazo mchawi lazima azifuate na asipofanya hivyo basi kazi ya uchawi inakuwa haiwezi na uchawi wake unamgeukia yeye kumwadhibu. Dawa za kichawi lazima zipate nguvu mpya, kutoa kafara za ndugu wa damu kama mtoto wa kuzaa, baba ama mama mzazi ni muhimu ili ku-recharge dawa yake.

Kuacha uchawi pia si kazi rahisi, once your in there is no simple way out!! lazima atoe kafara nyingi na kuyaua mauchawi yake yote ili yasimgeuke, sababu once yakijua anataka kuya-dump nayo yanaanza kujihami inakuwa vita takatifu.
umeeleweka ila si wachawi wote wanatoa kafara
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom