Wachawi wanatumia sura yangu kwenda kurogea. Wakuu Nisaidieni

Kyenyabasa

JF-Expert Member
Mar 8, 2023
249
711
Wachawi wanachukua sura yangu wakati wa Usiku kwenda kuwanga.

Nashangaa naambiwa mi mchawi wakati sijawahi kuwa mchawi nilipofatilia nikaambiwa wachawi ndo wanatumia sura yangu na kunishikisha uchawi bila Mimi kujua.

Wakuu akina Mshana jr na wengineo nisaidieni nitumie mbinu gani kujikinga!?
 
Wamekufanya mchawi kivuli, yaani analoga mwingine unaonekana wewe ambae haujui hata uchawi upoje. Ni ngumu kujisafisha kwa Jamii kukuelewa ukishapata tuhuma hizo.
Tafuta namna ya kukata hio connection then hama mtaa huo. Jitahidi uwe msafi kiroho Ili wasiweze kukutumia tena.
 
Kutakuwa na shida mahali.

Hicho kitu niliwahi kukisikia miaka ya nyuma sana.

Mama mmoja alipokuwa anaenda kuroga nyumba fulani alikuwa anatoka kwake anapita njia inayotoka nyumba nyingine ili ionekane mlozi ni mwenye kutokea njia hiyo.

Alipobanwa sana yule mchawi alikiri, ni hadith ndefu.

Upande wako yawezekana kuwa hivyo pia..

Unaweza pata hata madhara kwa hilo.

Sisi tunamwamini Mungu, tafuta watumishi wa kweli ili mfanye maombi.

Pole
 
Back
Top Bottom